Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Umelonga mjuba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie wajeda wengi ni washirikina.nimekutana nao chimbo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 

Sio kweli...mie nna miaka kumi toka nianze ujasiriamali...ukitaka ujimix nenda huko😅! Mie hata shipa la kuwaza kwenda huko halijawah amka
 


Yaani mie quartely najifanyiaga assessment wapi nikp dhaifu wapi nikp fresh..kwa mfanyabisshara yoyote yule..ukiamua kuwa honest kbs na mwenendo wa maisha yako utajua wapi unakosea...

Kuna bishoga alishika hela kubwa sana...ghafla hela imekata..kabla y kukata nilimwambia oya njia unazopita jitahidi urekebishe ( alikua anaibia sana client wake) nikajua iko siku atarudi back sq 1! Ameanguka hana pakishika..hataki kuangalia alipoangukia...amechanganyikiwa anashinda kwa hao waganga...wengine wanamla kbs uwiii...namwambia rekebisha hili na hili na kubali kianza na moja haelewi anaamini amelogwa🤧🤧! Haiwezekana aje bibi au mtu asieyeelrwa hesabu ukampgia mahesabu kila mtu ukamuongea hela za juu nature ikakuacha! Never
Be honest to yourself mambo yataenda tu iwe isiwe!..na usipende kutafuta sababu kusingizia jambo au mambo..no..be honest utagundua wapi unafeli
 
Naja pm[emoji41] kumbe rahisi hivyo [emoji2]
 
Kwa hyo mzee Tigo haikusalimika..
Ulipanda cheo na kwenda Ngome kwa gharama ya Tigo dah aisee
 
Michango ya WADAU ndio iliyonileta hapa
 
Kuna rafki yangu alimtia mimba mwanafunzi....eehh mwanafunzi kipindi Cha magufuli ichi ichi dodoma katika mji fulani....basi acha wazazi na mkuu wa shule + mratibu wakachachamaa wanataka mtu aende jela..... solution ya kwanza mwamba ikabidi akimbie mji akaenda kwa baba ake Tanga....kufika kule akaeleza yaliyomtokea....baba ake akampeleka kwa mtaalamu..kijana akafanyiwa ufundi wa viwango vya SGR,,,basi after one week akarudi mjini,,,,uku anawasiwasi...tukamuuliza mzee hujitaki wadau walikua wanakusaka Kama Ruby mzee,,akasema nimepikwa kwa fundi uko na akatuhakikishia kua tutaona miujiza,,,,,basi ikapita siku ya kwanza simu ya pili akapigiwa simu na mama mwenye mtoto... kubabake...ikabid atuonyeshe wajuba...tukamwambia pokea...maana simu haitamfanya akamatwe papo kwa papo...alivopokea...uyo mama aliongea kwa upole utafkiri katekwa...akasema mwanangu Aya mambo ya kawaida .watu wanataka kutuchonganisha..njoo nyumbani tuyajenge...mmmh wajuba tukamwambia unaeza kua mtego maana mganga wako hatumuamini...mwamba akamwambia yule bi mkubwa kua ana mashaka na usalama wake,,,,bi mkubwa akamwambia yashaisha...basi akamwambia ataenda keshokutwa..hii ilikua lengo tukachunguze ili mjuba asishikwe....siku ya pili acha yule Mama akawape kichambo mwalimu mkuu na mratibu kua yule mtoto ni wake hivo wasifatilie mambo yasiyowahusu,,jioni baba mwenye nyumba akaenda kumuwakia mkuu wa shule kua ajikite kwenye kusimamia walimu wake na sio mtoto wake mmoja aliepewa mimba...mkuu wa shule akachokaa...maana Ni wiki tu walikua bega kwa bega kumtafta mhalifu...tulivoskia ivo visa tukamwambia mjuba tia maguu sir tutakua around incase limetokea lolote....basi siku ilipotimia jamaa kutia miguu Yani walimpokea utafkiri nabii na kuku akachinjiwa ..akaombwa msamaha kwa usumbufu waliompa... jamaa akastaajabu...basi Ni miaka 4 Sasa na jamaa alimuo yule binti na Wana watoto wawili now.....waganga wa Tanga kwa kweli mmenishinda tabia🙌🙌🙌🙌🙌🙌
 
Kudadeki Kuna watu nyoko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie kwa waganga siachi kwenda madhari mambo yangu yananyooka na hivyo baba yangu aliniambia nitafute hela kwa njia yoyote ile hata uchawi ilimladi nisikubali kuwa kapuku na kweli bana kuliko kuiamini mizimu ya wazungu na warabu ni bora niabudu mizimu ya kwetu africa tu na imenisogeza kweli si haba
 
Daa nmecheka sana aisee[emoji23][emoji23][emoji23] et "basi siku ilipotimia jamaa kutia miguu Yani walimpokea utafkiri nabii na kuku akachinjiwa ..akaombwa msamaha kwa usumbufu waliompa"... jamaa akastaajabu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mganga wa juu hapo ndo yule wanaomtumia simba s.c?

Au modds mnasemaje?
 
Nayaomba hayo majina ya Mungu yenye nguvu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nakumbuka nilikua nmemaliza chuo nshakaa mwaka bila kazi...siku hiyo katika cv nilizopeleka nkasikia nmeitwa interview....nmekaa zangu kijiweni jamaa akanijia anasema anipeleke kwa mzee wangu tukawafunge macho watahini nipate kazi...siku hiyo ilikua ngumu sana maana ndo golden chance sitaki ipoteza..ila kilichonizuia ni toka nazaliwa sijawahi ona wazazi wanaongelea hilo swala...kesho yake nikaenda kwe interview na kupita...sasa nawaza tu kama ningemuamini yule mtu nadhan mda huu ningekua nishawajua vigagula wote mjini....Tusimame katika Yesu yeye hashindwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…