Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Mie sina hamu nao maana nilishapigwa dvd yangu ya kwanaza kumiliki, wakati huo DVD ndo zinaingia ingia, yani baada ya kuyumba ki biashara, nikakimbilia huko nikaambia nitoe hela ambayo sikua nayo. NikauliZwa nina nini cha kunidhamini nilijibu DVD, basi bwana nikapigwa mazima, issue sikufaanikiwa.
 
Msema kweli mpenzi wa mungu.nilishakwenda kwa mganga.kwa ajili ya demu.tulikuwa wapenzi ghafla aka badilika.akawa mgumu kinomaaa.hanipendi tena.niliumia.kuna rafiki yangu yeye ni mganga nikamueleza akasema tulia atarudi.
Tukafanya Mandingo mixer kuoga njia panda usiku.kuchoma sana UDI.kupasua Nazi n.k
Kiukweli demu alianza kubadilika na kuanza kuongea na Mimi.Mara salam n.k.
Siku zikapita tukarudi tena kwenye penzi.ila hatukudumu tuliachana.
Ushauri kama MTU hakupendi ACHANA NAE.MADAWA HUISHA NGUVU.
Hivi unaanzaje kwenda kwa mganga kwa akili ya mwananke,hivi watu kama nyie ndo huwa mnajinyonga au Julia mkiachwa,make mwenyewe akisepa kwao siwezi kumfuata MTU hakutaki
 
Nilipelekwa na mganga mtoni maeneo ya Msambiazi kwenye zile kona,mganga akaita mamba mtoni akaniambia nimkalie kichwani,wakati akifanya hivyo alikuwa amenishika nisikimbie.
Yaliyotekea ...nilijikuta kibenderani (polisi)nahojiwa kwa kosa la kushambulia na kutaka ku uwa

Sijawahi kucheka tangu nizaliwe. Teh teh Teh Teh Teh Teh Teh Teh Teh
 
ilikuwa ni darasa la sita mwanafunzi mwenzetu aliiba box la kalamu lote tena la mwanafunzi aliyekua mtoto wa mwalimu ikapita msako mkali hazikupatikana mwalimu akasema kesho asubh wote tuandike jina la mtu unaemhisi

Basi jioni tukajipanga wanaume kadhaa kama kumi na saba tukashauriana tuende kwa bibi mmoja ni mtaalamu huyu jamaa aliyeiba tutampata fasta

kikundi kikatimia tukatoroka moja kwa moja safari ikaanza tufafika kwa mtaalam na sare zetu za shule tukaingia wote kwa pamoja akaanza kutoa misauti yake akatueleza muna shida tofauti au ni moja mmoja akajibu ni moja

akasema haya mmoja aelezee jamaa akatiririka vya kutosha akasema andikeni majina yenu na ya baba yenu na shule mnayotoka kisha munipe ukishanipa unageuka nakuondoka hadi nyumbani kwako huyo mwizi asubuhi atapiga kelele nakuzirudisha mwenyewe sitawatoza hela nawasaidia tu kama wajukuu zangu tukafanya kama alivyosema

kumbe pale jirani kuna mwalimu wetu yupo karibu na yule bibi jioni akamfuata akampa na yale majina asubuh tupo paredi tukaanza kuitwa jina mmoja baada ya mwingine tukijiangalia ni wale wote tuliokuwa kwenye tukio ohoo kilochofuata siwezi ata elezea ngoja niishie tu hapa

na hapo ndipo nilopotokea kuwachukia hadi leoo
Mkuu yaelekea mlipigwa dozi ya aina yake.somo zuri
 
Kila mtu huwa ana imani yake

Kila mtu ana mbinu zake za kutatua matatizo yake.

Wapo ambao wakipata shida kidogo tu ni kwa babu sangoma wanakimbilia.

Tujuzane, vipi gharama huko? Shida zinatatulika? Permanently or temporarily?

Na pia nasikia every dark magic comes with a price, ni kweli..? Ni price zipi mnalipa kupata magic nyeusi hizo

Tujuzane

Binafsi mimi sijawahi kukanyaga kwa sangoma na sitakaa nikanyage huko
Umesema tuliowahi kwenda kwa wganga wa kienyeji tukutane hapa ukimanisha na ww ni mwenyeji huko,tena nunasema hujawahi kwenda hapo hapo unataka tarifa za huko hapohapo unasema hufikiliii kwenda huko,una hakili au una matope ya nn tukupe taarifa ili hali hufikilii kwenda?na haujawahi jipange upya mkuuu.
 
ilikuwa ni darasa la sita mwanafunzi mwenzetu aliiba box la kalamu lote tena la mwanafunzi aliyekua mtoto wa mwalimu ikapita msako mkali hazikupatikana mwalimu akasema kesho asubh wote tuandike jina la mtu unaemhisi

Basi jioni tukajipanga wanaume kadhaa kama kumi na saba tukashauriana tuende kwa bibi mmoja ni mtaalamu huyu jamaa aliyeiba tutampata fasta

kikundi kikatimia tukatoroka moja kwa moja safari ikaanza tufafika kwa mtaalam na sare zetu za shule tukaingia wote kwa pamoja akaanza kutoa misauti yake akatueleza muna shida tofauti au ni moja mmoja akajibu ni moja

akasema haya mmoja aelezee jamaa akatiririka vya kutosha akasema andikeni majina yenu na ya baba yenu na shule mnayotoka kisha munipe ukishanipa unageuka nakuondoka hadi nyumbani kwako huyo mwizi asubuhi atapiga kelele nakuzirudisha mwenyewe sitawatoza hela nawasaidia tu kama wajukuu zangu tukafanya kama alivyosema

kumbe pale jirani kuna mwalimu wetu yupo karibu na yule bibi jioni akamfuata akampa na yale majina asubuh tupo paredi tukaanza kuitwa jina mmoja baada ya mwingine tukijiangalia ni wale wote tuliokuwa kwenye tukio ohoo kilochofuata siwezi ata elezea ngoja niishie tu hapa

na hapo ndipo nilopotokea kuwachukia hadi leoo
Hahahah nimecheka sana
 
Haya mambo ni ya ajabu, unaweza ukawa na malaria ya kweli, kila wakati naambiwa malaria yapo, ukihama nyumba ukaenda nyumva yenye mazingira yaleyale malaria inatoweka. Ujue mchawi anaweza kutengeneza malaria hata HIV amini usiamini .Ni sayansi ya hali ya juu
 
Dooh nimegundua waenda kwa waganga wengi kumbe ni wanaume,kumbe nanyi mmo lkn hamvumi ,Mungu tuepushe na wanaume wa namna hii lol[emoji23][emoji2]
 
Dooh nimegundua waenda kwa waganga wengi kumbe ni wanaume,kumbe nanyi mmo lkn hamvumi ,Mungu tuepushe na wanaume wa namna hii lol[emoji23][emoji2]
Wanaume wanajitokeza bila kujishtukia ndiyo maana.... wakati wanawake hawajitokezi kutoa ushuhudaa

ni sawa na mada za ngono utakuta men wanachangia zaid ya women
 
Jamani kuna mdada mmoja namtaka lkn ananizingua saaanaaa.kila nikimwita anakuja mpk chumbani lkn ukimgusa hataki ku do.eti anasema hajisikii kufanya kuna kitu kinamsumbua kichwani.hana hamu ya kufanya mapenzi.lkn najiulza hanipendi au vipi huu ni muda mrefu hata miezi 555 inafika.natamani niende kwa babu nikamfanye anipende.naomba ushauri.auntie namba za babu
 
Mimi nimeanza kuhudhuria kwa babu nimwezi wa tatu sasa na matatizo yangu yametatuliwa on sport,nilikua nikiandamwa na majanga ambayo yalikua nje ya uwezo wangu ikafikia hatua kwamwezi napata hasara inayozidi kipato kwamaana kwamba badala ya kusonga mbele nikawa narudi nyuma tena kwahatua ndefundefu,baada ya kumpata mtaalam huu ni mwezi wa tatu naelekea mwezi wanne bila majanga hivyo hawa kina Mshana jr wanamsaada wao
 
Nipe namba ya uyo babu
 
Uchawi upo na uganga upo.....na hata hao viongozi wa dini wengine waganga wanajificha kwenye kivuli hicho cha dini na mnaenda......lakini pia muelewa uganga ni mpana sana......au ndo akifanya mganga ni uchawi lakini akifanya kiongozi wa dini ni miujiza.......
 
Viongozi wa dini wengi tu wanaenda kwa waganga kuongeza nguvu na kuogopwa na waumini wao....sema wao huduma yao wanapewa kwa usiri sana na wanajuana vizuri tu kuhusu tabia zao.
 
Mimi binafsi nimeenda kwa mganga wa kienyeji baada ya mzee wangu kuumwa kidonda mguuni kwa miaka miwili mfululizo akiwa analazwa miezi miwili au mitatu kisha anapewa ruhusa anarudi nyumbani wiki moja.

Tulizunguka makanisa yote unayoyajua na usiyoyajua mpaka ndani ya Dar hii, tulienda mpaka kanisa wanaliita la wanigeria huko Kinondoni lakini hollah.

Basi baada ya kuhangaika sana tukapata ushauri twende kwa mganga, ambapo kwa hatua tuliyokuwa tumefikia ilikuwa tuna uwezo wa kufanya lolote ili kuokoa roho ha mzee.

Basi tukaenda kwa mganga, akatueleza shida ilianzishwa na mzee wetu ambaye alimroga mwenzie katika ugomvi wa mashamba hivyo huyo mwenzake alipojua kuwa ni mzee wetu kafanya hivyo ikabidi alipize kisasi. Mganga alichinja mbuzi, akampa damu kidogo mzee kisha akampa dawa ya kunywa na kuoga kwa wiki moja.

Ndani ya siku mbili mzee alisimama mwenyewe na kuanza kutembea, tokea pale niliamini uchawi upo. Mara ya pili nilienda kwasababu ya ishu za kazini, huo mkasa nitawapa badae kidogo.

We umewahi kwenda mganga? Ulikuwa na shida gani? Ulitibiwaje?
 
Back
Top Bottom