zamani kuna mtu aliibiwa redio akaenda kwa mganga ambaye ni jirani yetu.mganga akamwambia aje na watu wote anaoishi nao .Baada ya watu wote kufika mganga akawaambia kila mtu anyanyue begi , wakanyanyua mmoja baada ya mwingine ikafika zamu ya mama mzazi wa mteja wake alikua ni mzee, kabla ajanyanyua begi mganga akasema subiri akaenda ndani na begi alivyorudi akamwambia yule mama anyanyue begi,mama wa watu akashindwa mganga akamwambia mteja wake nadhani umemuona aliye kuibia redio,mteja akasema haiwezekani mama yake aibe redio akamwambia mganga afungue bengi, mganga akagoma mteja akafungua begi kwa lazima, ndani ya begi wakakuta matofali ya blocks.Mganga alikula kichapo.