Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Mimi nakumbuka nilienda kwa mganga ili nifaulu mtihani wa kidato cha Nne ..Maana nilikaa miezi . Baba aliniambia niende kwa mganga ili nifualu mitihani yangu ...Mwisho wa siku niliambulia patupu bora hela ningefuga mbuzi
 
Nipm mkuu tushare kitu
 
Zamani sana nikiwa kijana mdogo form one!
Nipo nazunguka zumguka zunguka mjini nikakutana na wafanya mazingaombwe!
Yaani wakunja gazeti wanakoroga koroga hivi zinatoka noti mpyaaaa

Basi bwana si nikaingiwa na tamaa ya kupata zile noti [emoji23]

Wakasema anayetaka anyooshe mkono! kucheki kuna wazee wa maana wamenyoosha mkono Mimi ni nani nisinyooshe mkono!

Nikanyoosha, wakawa wanapita wanasema wanaweka dawa viganjani halafu hakuna kufumbua kiganja na kwakua ilikua jioni wakatuelekeza kwenye jengo flani ambapo walikua wamepanga kama ndio eneo ambalo mgao wa hizo fedha unaenda kufanyika!

Kufika pale akawa anaingia mmoja mmoja huko ndani!
Ikafika zamu yangu nikakuta ndani Kuna shilingi shilingi za kutosha!
Nikaambiwa ile upate hela yako unabidi utoe hela zako zote ulizonazo mfukoni Kwani ukiziacha zitavutwa!

Nikasema sina kitu kabisa!
Mgannga akanitishia kweli ila wapi!

Akaniambia ili nipate ninazozihitaji nije kesho!

Sikurudi tena!!
 
.
Ulikutana na mganga wa kienyeji alivalia kofia ya uchungaji.
.
Ni wengi na utawatambua kwa matendo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ha ha ha nimewahi kusikia stori kama hii bila kuondoa neno hata moja
 
Kwanini MGANGA WA KIENYEJI HAKUAGIZI SAMAKI???
Tuanzie hapo kwanza[emoji1321]
.
Mkuu samaki hana damu ya kutosha kwa kafara.
.
Kama ni mganga kweli anatakiwa kufanya kafara kwa kuchinja mnyama ili damu imwagike.
.
Kumbuka kwamba ulimwengu wa roho unatawaliwa na damu kwahiyo ili kuyaita majini yakafanye kazi yako, lazima uyape damu then unanuizia unachotaka kisha majini yanaenda kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna dawa hapo.Wangapi wanaachana na kurudiana bila madawa?
 
Tulienda kuroga ili timu ya mtaani ishinde ligi. Hatukushinda.
Wale wazaramo walinambia Kama hatuendi kwa mganga kuroga basi hawachezi mpira,nami nilikua kiongozi wa timu.
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Aisee, uliutumia ule msemo wa wahenga;Wajinga ndio waliwao.Ulianza anzaje???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…