Kwa wale waliowahi kutunza siri nzito kwa muda mrefu tukutane hapa

Mimi siri yangu ambayo iko moyoni na inanitesa ni kumla mke wa jirani yangu na kumpa mimba(Zamani lakini) mpaka leo nikimwona jamaa huwa najutia sana, kweli kutoka moyoni najutia sana kitendo kile japo mkewe alikuwa mzuri sana
Mtoto yupo wapi??? Me kuna manzi aisee nusu Nile maana mumewe alikuwa hashindi nyumbani kabisa na ndoa ilikuwa changa sema niliwazaa Sana nkaona sio poaa
 
Mim siwezi kutunza siri, memory ya kuhifadhi data ya kichwa changu kina mambo ya msingi sana ya kuhifadhi..

Siri kesho yake unakuta nimesha sema..

Mim nilisha wahi kumwona mama na mtoto wake wa kike wanamfukia kitoto kichanga.. Usiku hawakuniona kesho yake mapema nikaenda kulisanua..

Nikaja nikumwona msichana mmoja jirani alikuwa akiishi na mdogo wake wa kike dada mtu alikuwa ni fundi wa kushona alikuwa mjamzito ila hakuna aliekuwa anafahamu hakuwa anatoka nje ya nyumba hadi siku anajifungulia nyumbani mdogo wake yupo shuleni, mtoto akamtupa chooni nikashtuka nikalisanua

Kuna jamaa mmoja alikuwa na grosary yake ya kuuza pombe, ilikuwa karibu na kituo kikubwa cha polis, kumbe nyuma yake mchizi alikuwa anauza madawa ya kulevya, wacha nije nilisanue, kumbe pimbi alikuwa na connection na askari wa pale akaja kunshtukia wacha ale sahani moja na mim, wacha nilisanue karibia kituo kizima cha polis walihamishwa na ule mkoa nikahama mazima
 
Labda kweli ila siri nyingine zinanizidi uwezo.
 
Mungu wangu hiyo ya mwisho jamani Du.[emoji2955]
 
Duh!! Hii chai mzee baba utatuua [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Baby nimeanza kukuogopa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…