Kwa wale waliowahi kutunza siri nzito kwa muda mrefu tukutane hapa

Kwa wale waliowahi kutunza siri nzito kwa muda mrefu tukutane hapa

Mimi siri yangu ambayo iko moyoni na inanitesa ni kumla mke wa jirani yangu na kumpa mimba(Zamani lakini) mpaka leo nikimwona jamaa huwa najutia sana, kweli kutoka moyoni najutia sana kitendo kile japo mkewe alikuwa mzuri sana
Mtoto yupo wapi??? Me kuna manzi aisee nusu Nile maana mumewe alikuwa hashindi nyumbani kabisa na ndoa ilikuwa changa sema niliwazaa Sana nkaona sio poaa
 
Mim siwezi kutunza siri, memory ya kuhifadhi data ya kichwa changu kina mambo ya msingi sana ya kuhifadhi..

Siri kesho yake unakuta nimesha sema..

Mim nilisha wahi kumwona mama na mtoto wake wa kike wanamfukia kitoto kichanga.. Usiku hawakuniona kesho yake mapema nikaenda kulisanua..

Nikaja nikumwona msichana mmoja jirani alikuwa akiishi na mdogo wake wa kike dada mtu alikuwa ni fundi wa kushona alikuwa mjamzito ila hakuna aliekuwa anafahamu hakuwa anatoka nje ya nyumba hadi siku anajifungulia nyumbani mdogo wake yupo shuleni, mtoto akamtupa chooni nikashtuka nikalisanua

Kuna jamaa mmoja alikuwa na grosary yake ya kuuza pombe, ilikuwa karibu na kituo kikubwa cha polis, kumbe nyuma yake mchizi alikuwa anauza madawa ya kulevya, wacha nije nilisanue, kumbe pimbi alikuwa na connection na askari wa pale akaja kunshtukia wacha ale sahani moja na mim, wacha nilisanue karibia kituo kizima cha polis walihamishwa na ule mkoa nikahama mazima
 
Kuna kitu tofauti Mungu kakiweka ndani yako/Pia mwonekano wako ndio maana wanakuja tu siyo Bahatimbaya

Mimi unakuta Mtu mzima au Hata wazee anakuja kuomba Ushauri au analalamika kwangu na anafunguka kweli,Maskini wa Mungu sina Elimu kubwa wala Maendeleo/Mali nyingi na wengine Wananiogopa ata namna ya kuanza kuongea nami Bc nikijiangalia najishangaa Najitafakari sina lolote wala Chochete.
Labda kweli ila siri nyingine zinanizidi uwezo.
 
Binadamu katika mazingira mbali mbali,ukumbana na majanga mbali mbali ambayo mengine ni hatari kabisa,
Kuna waliowahi kushuhudia mtu kiauawa na kukaa kimya
Kuna waliowahi kuona mtu anamloga mwingine wakatunza siri,
Kuna waliowahi kuona mwenzao anaibiwa wakakaa kimya,
Kuna waliowahi kushuhudia mtu anabakwa wakakaa kimya,
Kuna waliowahi shuhudia mtu au mke wa mtu anatembea na mwanaume mwingine wakakaa kimya,

Mi siri yangu ambayo sitakuja kuisema ni kamba nilimfumania mjomba mkubwa akiwa anatembea na mke wa mjomba mdogo alafu wakajua kwamba nimejua sikuwahi kuisema ilikanusha, yapata miaka 20 sasa,
Leo kuna rafiki yangu amenambia kwamba akiwa mdogo alimuua mtu akiwa Croatia mwaka 1994 , na hakuna aliyejua,

Mwingine (dr) akasema kuwa amewahi kumuinject mgonjwa UKIMWI kupitia syringe, na akakaa kimya maana alilipwa Hela ya kutosha


Najua na wee una siri umetunza tudokeze
Mungu wangu hiyo ya mwisho jamani Du.[emoji2955]
 
Dahh hakika kuna watu usiwaambie siri kuna jamaa mmoja anaitwa uncle mecky huyu bwana huwa anajulikana kwa Umbea viunga vya dar kuna siku alimkuta jamaa mmoja anatembea na mke wa Jirani yake, jamaa alivoona vile akamvuta uncle mecky pembeni na kumpa million 1 ili atunze siri, basi uncle mecky akamhakikishia jamaa hatasema. Baada ya week jamaa akasikia uncle mecky anaumwa sana kalazwa hospital akaona akamuangalie basi vile anafika hospital anauliza kwa Dr mgonjwa anaumwa nini akajibiwa ana joto tu Kali lkn kapimwa hana maradhi yyt. Mecky akamuita jamaa ebwana eeeh chukua hii million yako utakuja kuniua maaana nimevumilia huu Umbea nimeshindwa mpk joto limepanda mwilini
Duh!! Hii chai mzee baba utatuua [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna siri nyingine ninazo hadi nikianza kuziwaza naogopa mwenyewe.
Watu wamekua wakijiamini Sana wakikaa na Mimi kuongea mambo yao.
Nyingine nashindwa kuzibeba hadi nakua Kama mgonjwa ila ndo inakua siri tena nashindwa kuzitoa.
Kuna muda natamani ni mwambie MTU asiongee au kufanya kitu mbele yangu sababu ananipa mzigo wa kuanza kufikiria ila nakaa tu.

Wengine nawaulizaga hivi unajiamini nini kufanya/kuongea hiki mbele yangu.
Baby nimeanza kukuogopa!
 
Back
Top Bottom