Nakumbuka ilikuwa mwaka 2000 tulikuwa border ya Mozambique na Tanzania,kunajamaa tulikutana nao Wa Tanzania walikuwa wanavuka mto Ruvuma kuingia Mozambique,mmoja wao akawa amekuja upande Wa mozambique kuja kuangalia Usafiri huku wenzake kawaacha upande. Wa pili Tanzania,hawa jamaa walikuwa wakataa mbao.
Basi ikawa Usafiri kakosa na giza limeingia maana kuvuka mwisho ni saa 12jioni,basi tukawa tumekaa upande Wa Mozambique ofisi za uhamiaji huku tunaota moto na kupiga stori,alikuwepo askari mmoja wanawaita guardafrontere, yaani askari wa mpakani alikuwa amelewa ndiye aliyekuwa analinda ofisi au mwenyeji wetu, basi hawa wabongo wakapanga wakaibe mtumbwi wavuke usiku kama saa.
Tatu, na mvua ilikuwa inanyesha, huku askari yuko tungi amelala hajui kinachoendelea,baada ya kama nusu saa nikaona wanaludi mmoja,mmoja kimya huku wamelowa kuwauliza kulikoni?j Jamaa wanasema mtumbwi umepinduka wao wamejiokoa lakini jamaa mmoja mbogo amezama, ishu ikaja tumwambie askari huyu aliyelewa?nikawaambia wote tutafungwa na askari wa mozambiki hawana dogo Maadam kafa Mwenyewe tukae kimya, basi kesho Yake jamaa waliondoka na kuniacha peke yangu nilikuwa na ishu ya kukaa kama wiki pale.
Kati ya wale jamaa waliondoka mmoja si akasimulia kwenye kwenye Gari alilokuwa anasafiri nalo kwamba kuna jamaa anaitwa fulani amezama Jana usiku, kesho yake jioni ikabidi Ndugu zake waje, walipofika kuulizia kama Ndugu yao kazama, kila mtu anashangaa,mbona huku kuko shwari mpaka askari, hakuna anayejua zaidi ya Mimi, ikabidi waondoke warudi tena Tanzania, yule jamaa aliyezama alikuwa na wafanyakazi wake aliokuwa ameongozana nao,wakawa wanamsubiria nao hawajui kitu ,ilibidi serikali iingilie kati kumtafuta jamaa, walikuja kumpataa baada ya siku 10 huku na Mimi nimeshaondokaa, siri ni kitu kinachoweza kukuokoa