Kwa wale waliowahi kutunza siri nzito kwa muda mrefu tukutane hapa

hapa tutadanganyana tu.... siri ya kweli na ya kuitwa siri... hata humu huwezi kuiandika... sikatai zipo siri, ila hapa mi naamini wapo waliopata kuua,hawawezi kusema, kukanyagwa walau mara moja kinyume na maumbile, nao wapo...

siri ni hizo,siyo za kupekua simu... kama ni mdada pengine kuna kitu ulikifanya ukajutia, au mpaka sasa unajutia na umekifanya kuwa siri... mambo ya namna hiyo....

Japo nakumbuka JF ya miaka mingi nyuma, kuna jukwaa nilikuwa, na nikamkuta mmama au mdada labda, akijielezea kuwa alikuwa na kazi, ila alitaka cheo, na ijapokuwa vigezo alikuwa navyo, ila hakuwa peke yake waliokuwa wanafit kwenye hiyo position..
Alijaribu kwa kumuendea boss husika ambaye bila kusita alimwambia nafasi hiyo ataipata, ili mradi awe tayari kuliwa uroda..
Kitu ambacho baada ya kusita na kujishauri sana, alikifanya... lakini ilikuwa ni siri yake kwa muda mrefu kama alivyojieleza, na ijapokuwa anaishi vizuri na maslahi ya cheo hicho anayaona, lakini alikiri JF kuwa alikipata kwa njia hiyo.

Unaweza kupima siri ni kitu cha namna gani.. siri ni kile ambacho kinakugusa wewe binafsi...
 
hii leo utaikuta imesambaa whatsapp, maana ni kichekesho sio siri tena
 
Mmmmh hii fix kabisa.
 
hahaaa
 
Heri kuuza Figo kuliko kutatuliwa aisee,hata kubeba zege au machinga alishindwa kauza bikira kwa laki NNE unusu hata mwezi ufiki,
hahaa laki 4 '' huyo ilikuwa ni kawaida yake kuliwa" asikushangaze "
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbona kawaidaa tuu mzee...!!
 
Siri yoyote inayonihusu mimi binafsi au familia yangu siwezi kuisema mpaka naingizwa kaburini ila siri za watu wengine na zisizoathiri taswira yangu moja kwa moja naweza kuzihadithia kwa hadhira.

Tabia za utotoni za kupenda kucheza na kula kwa 'watu', ila nimeitwa jikoni nikanawe paaaap nikamuona mama wa rafiki yangu (jirani) anatoa mkono 'sirini' kisha anaunyunyizia katika bakuli la mchuzi la baba wa rafiki yangu yule (wa utotoni).

Daaaah nilipata mshtuko na yule mama pia alishtuka sanaaa...!, 'nikajibaraguza' palee, nikaingia jikoni, nikanawa nikarudi sebuleni then huyooooo nikapitiliza mbio mpaka nyumbani wala sikwenda kula.

Sikuwahi kumsimulia jambo hilo yule rafiki yangu mpaka leo hii ingawa urafiki wetu ulikatishwa baada ya wao kuhamia mkoani mwanza baada ya kuwa tumemaliza std 7. Wanawake,! Mungu anawaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…