Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Me nakumbuka mitaa ya kiyungi long time agoo
 
ww km c wa tabora kaa kmy na kinyamwenzi kinausika hapa km wa kikwete auwezi kufahamu
Kwani kuuliza vibaya ? Una uhakika gani mimi sio wa Tabora ? Nilicho uliza hizi habari wanazo ongelea wadau ni ya miaka ipi
 
Wale wanawake wa kihaya Mwanza road bado wapo ? Wanaendelea kugawa utamu ?
 
Kwani kuuliza vibaya ? Una uhakika gani mimi sio wa Tabora ? Nilicho uliza hizi habari wanazo ongelea wadau ni ya miaka ipi
Achana naye huyi mnyamwezi
je angekuwa ndiye mwenye Forim si wengi tungefukuzwa?
Mada anazoziongelea ni za miaka ya 90 kuja mbele
wakati Mwanaisungu kaja pale nje ya geti kuweka kaukumbi ka Disco mwaka 1982 kanikuta
na kalikuta Disco la TH (Tabora Hotel ya Railways) linapiga
Isevya malambo ya minga na maji kutuama hata uwanja wa Ally Hassan Mwinyi haujafikiriwa
leo watu wanataka wa Tabora tu
 
Habari za familia ya dr. Kobelo inasikitisha sana, tulikaa nao mtaa mmoja kota za boma road (tridep), mtoto mkubwa alikuwa akiitwa Tobby wa pili Steve, mdogo sikumbuki jina lake.
Toby na Steve walisoma na wadogo zangu, walikuwa na akili sana hawa watoto, niliondoka kwenda chuo, mzee naye akahamishwa, baada ya chuo post yangu ya kwanza ya kazi ikawa Tabora, makazi yangu yakawa bachu ground, kumuulizia Toby nikaambiwa yupo mahabusu kwa kesi ya mauaji kama sikosei, wakati huo dr. Kobelo ana dispensary yake bachu karibu na mgahawa wa mikendo.
dr. akawa kashikwa masikio na barmaid wa Georgies bar, dr. alikuwa cha pombe sana. akirudi nyumbani anatembeza kichapo kwa mkewe, inasemekana watoto uzalendo uliwashinda wakaamua kumdunda mpaka kumvunja mguu, Steve naye akaingia mahabusu kwa kesi hiyo.
Nilihama tbr, baada miaka kadhaa nikarudi na kukuta Toby katoka lakini tayari ni chizi, niliumia sana! kuna siku alinikuta nipo ziro bar, kaja na fuko lake la makopo, pamoja na uchizi wake lkn alinikumbuka tukaongea vizuri tu
Mama yao alikufa kwa ajari ya kugongwa na pikipiki maeneo ya chuo cha ualimu.
 
Joyce Masamalo nilikuta naye hivi karibuni, yupo TRL Dodoma.
 
Wale watoto Wa OCD mabauncer!
Dah! Ntuzu umenikumbusha hao mabouncer, kila siku ni kupiga chuma tu, tulikuwa tukiwaogopa si mchezo, ikiwa kumbukumbu yangu ipo sawa nyumba yao ilikua karibu na mzunguko wa bomani
 
Du,nawakumbuka hawa vijana,wape pole sana,sisi Wa cheyo a NBC flats hatunaga vya kusema,tuwaachie Wa kiyungi,isevya,mwanza rd na huko uswazi
 
Dah! Ntuzu umenikumbusha hao mabouncer, kila siku ni kupiga chuma tu, tulikuwa tukiwaogopa si mchezo, ikiwa kumbukumbu yangu ipo sawa nyumba yao ilikua karibu na mzunguko wa bomani
duuh!!! wee jamaa hatufahamiani kweli, nimeishi kwenye zile flats za Tanesco na Posta jirani kabisa na makazi ya OCD. kichekesho ni kwamba nilikuwa na kaka zangu nao ni wazee wa mazoezi sasa wakawa wanatambiana nani ni mbabe zaidi....kuna bro wangu akawa anabeba chuma za mazoezi na kukimbia nacho akipandisha vilima vya cheyo kuonyesha kwamba yuko fit zaidi.

Namkumbuka mzee mmoja anaitwa Muungwana alikuwa na guest zake kadhaa pia mzee Mwenda na mzee Pancheta maeneo ya Mwanza road.
 
mboka manyema a.k.a western province, wale wa kanyenye naona siku hizi imekuwa kama sinza au tbt noma sana, kama hujaenda since 2005 ukienda now utashangaa
 
Vipi yule mwarabu wa meya bado yupo.? Nilipofika tabora kwa Mara ya kwanza nililala ronaldo guest house ipo bachu.
 
Daah inauma sana ni watu ambao nawafahamu,
Mboka pia kuna ushirikina sana
 
Mwalimu chiboni nadhani baada ya kuhama Mwenge alienda kufundisha shule moja inamilikiwa na shirika la Reli nchini "Shule ya Msingi Reli" mahali ilipo stesheni ya ITIGI. kwa wasiofahamu, mwl huyu ni mmoja wa watu waliohusika kwenye utunzi wa vitabu vya kiingeleza shule ya msingi. (kama sio madarasa yote basi ni darasa la tatu na la nne)

Mwalimu Maduhu na lafudhi yake ya kisukuma alikuwa mwalimu mzuri lakini pia bingwa wa mboko.
 
Duu sitasahau ugomvi wa Tabora boys na milambo wakigombea mademu wa kazima Enzi hizo kazima kulikuwa
na warembo....mwenye no ya evelini kisenge tafadhali....fungulia dog ya mwanaisungu club.tuliopo Dar tutafutane jamani

Ipo haja tuanzishe organization yetu tukumbushane maisha yakivyokuwa and then tucheki th way forward. Nikiangalia Tabora inazidi kuchoka siku hadi siku.
 
Undeni waaasap group mtaonana wote ndo tulichofanya sie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…