Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

mitaa ya nation n'gambo kariakoo na cheyo tuliosoma boys tunahusika sana
Nakumbuka enzi za kutoroka shule kwenda kuangalia mpira kwa Mrema na Sonda..zile bar sijui bado zipo?
 
Mgulunde cup au Ummiseta ilikuwa balaa,Mihayo wana jamaa anaitwa Zai,Tabora boys kuna Renatus Njohole na Wilfred Kidau,Uyui yuko Ally Mayai na kipa aitwaye Dave halafu Kazima kuna kajamaa walikuwa wakikaita Nteze,Milambo kuna foward alikuja chezea Shinyanga shooting alikuwa na matege hivi.Kwa kweli ilikuwa zaidi ya burudani.
 
Baadae Tabora Boys tukawa na Akilimali Yahya..acha kabisa Ummiseta ilikuwa Ummiseta kweli.
 
mwanaisungu namkumbuka Caft, alimaliza wadada wa uyui na uhazili mwisho akaja kufa na gonjwa hili, nakumbuka discko toto badala ya kwenda kanisani unaenda isungu, daah! pale Tabora miaka ile wasichana wa uhazili ndio wazuri aisee maisha haya?! Namkumbuka Major, Juma Nge, Salum Stuwa, Uther ndio walikuwa mabrother man wa town, loo.. maisha yale ya utoto yalikuwa matamu sana.
 
Nakumbuka nilivyoingia milambo high school nikapita mitaa ya chem chem kila nyumba nasikia harufu ya pilau ukiangalia nyumba zilivyopinda nilichoka.
Mwaka gani huo meti??
 
Mitaa ya mihogoni/chemichemi...usiku usiku...hatareee...wajero alikuwa anahusika

Gest uwanja wa mpira milambo[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kudhalishana tu
 
Ila Tabora wale wanawake chotara wa kinyamwezi na kiarabu walikuwa wanajua kupika vitumbua.hasa mama Moza ile mitaa ya subeti karibu na kanisa la morovian.
 
Kwa mimi wa Nzega naikumbuka HINDOCHA, ilikua bas flan hiv Leyland inaondoka Nzg alfajir kuelekea Tabora ndo ilkua basi pekee kipind hcho,
 
Kwa mimi wa Nzega naikumbuka HINDOCHA, ilikua bas flan hiv Leyland inaondoka Nzg alfajir kuelekea Tabora ndo ilkua basi pekee kipind hcho,
[emoji23][emoji23][emoji23]nzega ndio om mkuu nimesoma nyasa one ,
 
Nakumbuka enzi za kutoroka shule kwenda kuangalia mpira kwa Mrema na Sonda..zile bar sijui bado zipo?
Nilikuwa na demu pale kwa mrema siku moja madafu akanikuta ilikuwa bonge la noma pale shule.
 
Nilikuwa na demu pale kwa mrema siku moja madafu akanikuta ilikuwa bonge la noma pale shule.
Hahahaa,we jamaa umenikumbusha Madafu na amri zake za kila mwanafunzi awe kanyoa nywele ndani ya nusu saa..

Ila uzuri wa Madafu ilikuwa ukiongea nae herufi kubwa hana nongwa sio kama Ndugu D hahahaaa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…