Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Hahahahaha... nashukuru mungu alinijalia kumbukumbu tehtehteh.... huwaga nakumbuka komenti tu ileee uzi ulikua unahusu makabila

cc Smart911
Haha mdogoake stori moja kusimulia Mara kumi inachosha na inapoteza mvuto
 
Mbona umepaniki... tulia kidogo basi,
kuwa mkubwa sio tatizo,maana kwa kipindi hicho tu kuwa High level inatosha kuonyesha kuwa ulikuwa mkubwa tu,Ila hapa tunakumbushana tu utamu wa Tabora hususani kwa watu tuliokuwa hatujuani .
Haujakosea, akina kalovya ndipo walipokuwa wanakaa, na ni kweli HK alikuwa ana dada zake na kaka yao mkubwa( majina nimesahau).Nilichogundua ni kuwa, ulikuwa shabiki wa Basketball lakini haukucheza.nimekuwekea picha ya miaka hiyo uangalie na kutambua wachezaji( Wengi wao wametajwa kwenye uzi huu.Ukizungumzia High level, walikuwepo akina Salehe Kimenya na wengineo.Hakuna sehemu nimeleta ubishi, rudia post yangu.naamini sote tulikuwa watoto wa "DUGU" PATEL, R.I.P, chini ya mkuu msaidizi Mwl.Mkatakona R.I.P na walimu kama , Mr Mbosori R.I.P, Mr Machibwa,Mr Mrisho (Mtaalam wa Hesabu),Mwalimu mmoja wa Biology, alikuwa na jina gumu tukampa nickname Agama Agama nk hawa wote walikuwa baadhi ya walimu wa O level.
SaleheSaleheKimenya amesoma na mdogo wangu hapo Uyui baada ya mimi kutoka. Ila Salehe hakucheza Basketball.
 
ni kweli kabisa, Salehe hakucheza Basketball, alikuwa mshikaji tu, ila watu waliosoma A Level na walicheza Basket ni kama Onesmo,Anthony Gutta, kiobya,Arnold Kiejo,Kamwanga nk
 
Nakumbuka nilivyoingia milambo high school nikapita mitaa ya chem chem kila nyumba nasikia harufu ya pilau ukiangalia nyumba zilivyopinda nilichoka.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kama tabora ttc sisi pale kulikuwa na kiongozi mnaa
 
Siku ya jtano usiku bendi ya tabora jazz ilikua inatoa burudani pale unyanyembe social hall karibu na soko kuu mida ya saa nne usiku utasikia ukiw mitaa ya Chemchem near Kwa wanaume Milambo School nyimbo zinasikika "Ooooh najuta ....nifanye nini sasa....pole kaka mimi ni bado msichana....!"

Kulikua na mabasi ya kwenda Urambo yana carrier juu, road ikiwa ni vumbi nasikia siku hizi ni lami enz hizo stend mpya haijafunguliwa na mh Ben Mkapa aliyekuja kuifungua baadae sna akiwa anatembelea mkongojo kipindi hicho.

Redio za FM ilikua hakuna had baadae sana ikaja RFA na hizi za CG FM na VOT, voice of Tabora zikafuata.

Ukitembea njiani unaangukiwa na maembe aliyoacha Mwarabu ile njia ya karibu na NMB kwa nyuma imejaa miembe njiani
Pale nmb mihayo au
 
Duh!! Wewe unakumbuka sana shule ya Mazoezi Mwenge. Huyu Mwalimu Chiboni alikuwa headmaster, alikuwa anajua kiingereza kizuri na fasaha sana but alikuwa Mlevi wa Pombe, Alikuwa mwenyeji wa Dodoma(Mgogo) na mara ya mwisho nilimwona 1993 Salanda-Dodoma nikipita na treni akiwa hana chochote.
Pia kulikuwepo na walimu wengine kama:
1/Mwalimu Shigela(Inadaiwa huyu mama alianza kufundisha na Nyerere enzi za Mkoloni, alinifundisha kusoma na kuandika!!)
2/Mwalimu Mihayo.
3/Mwalimu Pongo(Nilisikia huyu mama alikufa kwenye ajali ya Mv Bukoba 1996)
4/Mwalimu Husein.
5/Mwalimu Maduhu.

Sijui kama unakumbuka ile mihogo mizuri ya kupikwa iliyokuwa na Pilipili ikiuzwa wakati wa break?
Wagogo hatuna walimu Walevi ss danganya wengine
 
Duu sitasahau ugomvi wa Tabora boys na milambo wakigombea mademu wa kazima Enzi hizo kazima kulikuwa
na warembo....mwenye no ya evelini kisenge tafadhali....fungulia dog ya mwanaisungu club.tuliopo Dar tutafutane jamani
Lakini mlikuwa hamuwezi kuwabandua
 
Mimi zaidi Tabora naikumbuka timu ya Milambo enzi hizo mwanzoni mwa miaka ya tisini inapanda daraja na kuingia ligi kuu kwa kishindo.

Kupitia juhudi za mkuu wa mkoa wa wakati huo Marehemu Laurence Gama na Mfadhili wa timu, Muasia mmoja aliyefahamika kwa jina la Kanji, Milambo ilikuwa na wachezaji kama Godwin Mashoto, Job Ayubu, Ferez Teru, Mikidadi Jumanne(Bubu), Mrisho Moshi, Ali Manyanya nk.
Nilikuwa sikosi mechi uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na kama siku sina pesa basi ilibidi 'Fungulia Mbwa' itumike!!
Unamkumbuka kumbe Laurence Gama
 
Teh teh teh!
Mkuu mamtonga nimekula saana pale isike primary! Wakati nyerere anafundisha mihayo!

Sasa hapo piga hesabu mi mdingi kiasi gani!

Enzi hizo wale masista wa pale moravian ukiwatizama utafkiri hawa kina dada wa kiislamu!

Yaani huoni chochote kwenye miili yao zaidi ya uso tu!

Na nadhani ile moravian iko mpaka leo. Ya kule mwanza rd.

Na wakati huo igombe ndio ilikuwa beach baab kubwa!

Siku za sikukuu tunabebana kwenye malori tunaenda kucheza SAKAYONSA au Ile miziki ya Tabora Jazz karibu na Viboko wa Bwawa la igombe!

Sii mchezo!
Mhenga mwenzangu. Isevya kwa kwa Ali Maguberi, kina marehemu Hamis Magurdumubna vitumbua vya moto, matapeli wa mwanzooo kina Juma Nkolokosho.

Enzi za Uhazili tulitesa sana, Railway Club. Timu ya basketball kina Kamsululu. Nimekumbuka mbali sana.
 
Back
Top Bottom