Mbona umepaniki... tulia kidogo basi,
kuwa mkubwa sio tatizo,maana kwa kipindi hicho tu kuwa High level inatosha kuonyesha kuwa ulikuwa mkubwa tu,Ila hapa tunakumbushana tu utamu wa Tabora hususani kwa watu tuliokuwa hatujuani .
Haujakosea, akina kalovya ndipo walipokuwa wanakaa, na ni kweli HK alikuwa ana dada zake na kaka yao mkubwa( majina nimesahau).Nilichogundua ni kuwa, ulikuwa shabiki wa Basketball lakini haukucheza.nimekuwekea picha ya miaka hiyo uangalie na kutambua wachezaji( Wengi wao wametajwa kwenye uzi huu.Ukizungumzia High level, walikuwepo akina Salehe Kimenya na wengineo.Hakuna sehemu nimeleta ubishi, rudia post yangu.naamini sote tulikuwa watoto wa "DUGU" PATEL, R.I.P, chini ya mkuu msaidizi Mwl.Mkatakona R.I.P na walimu kama , Mr Mbosori R.I.P, Mr Machibwa,Mr Mrisho (Mtaalam wa Hesabu),Mwalimu mmoja wa Biology, alikuwa na jina gumu tukampa nickname Agama Agama nk hawa wote walikuwa baadhi ya walimu wa O level.