Ntuzu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 17,418
- 10,877
- Thread starter
- #41
Duh!! Wewe unakumbuka sana shule ya Mazoezi Mwenge. Huyu Mwalimu Chiboni alikuwa headmaster, alikuwa anajua kiingereza kizuri na fasaha sana but alikuwa Mlevi wa Pombe, Alikuwa mwenyeji wa Dodoma(Mgogo) na mara ya mwisho nilimwona 1993 Salanda-Dodoma nikipita na treni akiwa hana chochote.
Pia kulikuwepo na walimu wengine kama:
1/Mwalimu Shigela(Inadaiwa huyu mama alianza kufundisha na Nyerere enzi za Mkoloni, alinifundisha kusoma na kuandika!!)
2/Mwalimu Mihayo.
3/Mwalimu Pongo(Nilisikia huyu mama alikufa kwenye ajali ya Mv Bukoba 1996)
4/Mwalimu Husein.
5/Mwalimu Maduhu.
Sijui kama unakumbuka ile mihogo mizuri ya kupikwa iliyokuwa na Pilipili ikiuzwa wakati wa break?
Mkuu ile mihongo ilikua inaitwa Kapile Au makapile!
Na kwa wale waliosoma Kazima wanamkumbuka Mwalimu Babu Au Peter!
Vp na wale Wa Chipkizi? Mwamkumbuka Mwalimu Kisanji?