Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee na ITEGAMATWI pia, isije ikawa tulicheza kombolela. Sitaki kuwafahamu aisee. LOL
Karibu na wale waburushi ndugu wa Rostam Aziz wakina kasel-kandis! Huku opposite na geti kuu la kuingilia kazima sekondari.Kwetu ni mtaa wa nyuma ya hao waburushi.
Kaselkandis ni binamu zake Rostam. Hiyo mitas unayoisema kulikuwa na mtu anaitwa Amin Imkana. Alikuwa anacheza mpira ni balaa. Ex Uyui huyo. Alipo kuja Dar mpira akaacha. Tabora ilitoa vipaji vingi sana hasa football na basketball.
Kama sikosei wewe ulikuwa jirani na Jaji Kwikima then alikuwa ni Advocate
ntunga,ntalali, kwa sana maeneo ya urambo,nsenda,imalamakoye,kasisi,wema,mwenge moto,mabatini,usoke,block q, nk
Wewe picchu kama nakujua kwa stories zako
Nakumbuka Ile fainali ya kombe la Mgulunde Kati ya Milambo wanaume na Uyui sec ilichezwa siku mbili na Milambo kuchukua kombe tulitembeza kombe bado tabora boys. Maana macho ya kwanza Uyui tu liwafunga wakatoboa mipira. Acha kabisa.
nakumbuka yalikuwa matatu nitajie mengine mawili
Hahaa unamkumbuka jamaa flani walivaa skiert za uyui siku ya kwanza? Ally Mayai sijui ndiyo huyu alikuwa ni hatari, lkn Milambo tulikuwa na akina Rodrick, Goliath, Kimti, Method na nk team ile ilikuwa hatari sana.
Hao ndo walikua masharobaro Wa mboka wakati ule!
Dah! Enz izo mji uliwaka kilipotimka kivumbi kati ya Mirambo Vs T/boys kuwania T/girls.
Yule mpishi akikuwa akiitwa Msengi kafupi kalikuwa kanajidai kababe ka jikoni. Siku ambayo tulimpiga mwanajeshi tukaambiwa wajeda wanakuja Milambo wanafunzi wote hatukulala na uanaume wetu.
haaaahhaah Taradadi yule wa Urambo?alikuwa na kama mwarabu fulani na ana manyoya kama nyani nakumbuka cc tulikuwa tunamwita taradadi manyoya alikuwa na sifa ya kungonga wasichana sana kipindi cha UMITASHUMTA
Aah nimecheka mpa basi. Taradadi alikuwa ni mwalimu wa primary school sikimbuki jina. Lakini pia alikuwa ni kocha wa mchezo wa riadhaa. Pia alikuwa ni mwalimu kwenye magwaride ya chipukizi. Siku hizi naona yamekufa. Ila mara ya mwisho nilimsikia kwenye radio kipindi cha michezo akiongea kama Afisa Utamaduni nadhani ni Manispaa ya Tabora kuhusu maandalizi ya mchezo wa riadhaa.
kuna mwalimu mwingine mwarabu alikuwa anaitwa Karim, alikuwa na mguu mmoja mlemavu, alifundisha gongoni primary, ndugu yake adam fundikira alias Adam Maroboti.
adam marobiti alikuwa na demu wake anaitwa salama mahewa. nasikia baadaye alimuoa kama mke wa pili.
*TABORA NA MADAKTARI.
Nikiwa Tabora katika miaka ya 1980s na 1990s nilifanikiwa kufahamu mengi kuhusu Madaktari wa binadamu na maishha yao, kwa kifupi nina wakumbuka hawa zaidi. Dr.Kisenge, Dr.Kobello, Dr.Mohamed.
Kwa mfano Dr.KISENGE
Alikuwa na zahanati yake katikati ya mji pembeni mwa jengo la kampuni ya sigara ikitazamana na Jengo la shirika la Bima(NIC) na benki ya zamani ya CRDB(Benki ya ushirika na maendeleo vijijini).
Alifariki 1994.
Watoto wake watatu wakaja kuwa madaktari Dar, Mmoja Dr.Sabuni(Ni daktari bingwa wa watoto pale Muhimbili), Dr.Peter Kisenge(Ni Daktari bingwa wa Moyo pale Muhimbili) na Dr.George(Ni daktari wa Mifugo, yuko Dar akifanya biashara ya vipuri vya Magari Kariakoo).
Yupo mtoto mwingine wa Dr.Kisenge anaitwa Endrew kwa sasa yupo Dar anakula bata tu, yeye ni kupiga hela na kuponda raha, enzi zile kila mrembo mkali aliyekuwa Uhazili jamaa alikuwa anamsaka kwa udi na uvumba, muda mwingi alikuwa akiendesha Kwa kasi Pikipiki Kubwa XL ya Ofisi(Zahanati), Gari ya Baba yake(Pigot 504) na baadaye alinunua Carina yake Nyekundu ili kusaka warembo, jambo la ajabu ni kuwa marafiki zake aliokuwa nao Tabora na baadhi ya warembo wengi wa Uhazili walikufa kitambo sana kwa Ukimwi lakini huyu jamaa inadaiwa mara zote alipopimwa alikuwa yuko Fit kabisa!!
Kwani gharama ya pilau inaweza ikajenga nyumba?au unataka kusema mtu anakula chakula cha aina flani kutokana na aina ya nyumba anayokaa?Nakumbuka nilivyoingia milambo high school nikapita mitaa ya chem chem kila nyumba nasikia harufu ya pilau ukiangalia nyumba zilivyopinda nilichoka.