Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Karibu na wale waburushi ndugu wa Rostam Aziz wakina kasel-kandis! Huku opposite na geti kuu la kuingilia kazima sekondari.Kwetu ni mtaa wa nyuma ya hao waburushi.

Kaselkandis ni binamu zake Rostam. Hiyo mitas unayoisema kulikuwa na mtu anaitwa Amin Imkana. Alikuwa anacheza mpira ni balaa. Ex Uyui huyo. Alipo kuja Dar mpira akaacha. Tabora ilitoa vipaji vingi sana hasa football na basketball.
Kama sikosei wewe ulikuwa jirani na Jaji Kwikima then alikuwa ni Advocate



Uko sahihi kabisa! Watoto wake nimecheza nao tangu enzi za tayari bado mpaka sasa hivi karibia wote wanafamilia zao. Walikuwa jirani zangu.
 
Nakumbuka Ile fainali ya kombe la Mgulunde Kati ya Milambo wanaume na Uyui sec ilichezwa siku mbili na Milambo kuchukua kombe tulitembeza kombe bado tabora boys. Maana macho ya kwanza Uyui tu liwafunga wakatoboa mipira. Acha kabisa.


Hahaa unamkumbuka jamaa flani walivaa skiert za uyui siku ya kwanza? Ally Mayai sijui ndiyo huyu alikuwa ni hatari, lkn Milambo tulikuwa na akina Rodrick, Goliath, Kimti, Method na nk team ile ilikuwa hatari sana.
 
Hahaa unamkumbuka jamaa flani walivaa skiert za uyui siku ya kwanza? Ally Mayai sijui ndiyo huyu alikuwa ni hatari, lkn Milambo tulikuwa na akina Rodrick, Goliath, Kimti, Method na nk team ile ilikuwa hatari sana.


Timu yeni ilikua vzr sn! Hao jamaa walikwenda Chuo cha Reli!

Kuna jamaa mwingine alikua anaitwa George Kifwewe alikua Beki!
 
Yule mpishi akikuwa akiitwa Msengi kafupi kalikuwa kanajidai kababe ka jikoni. Siku ambayo tulimpiga mwanajeshi tukaambiwa wajeda wanakuja Milambo wanafunzi wote hatukulala na uanaume wetu.
 
Yule mpishi akikuwa akiitwa Msengi kafupi kalikuwa kanajidai kababe ka jikoni. Siku ambayo tulimpiga mwanajeshi tukaambiwa wajeda wanakuja Milambo wanafunzi wote hatukulala na uanaume wetu.


Ha ha haaaaa! Kale kafupi keusi kalikua kanakaa mihogoni!

Wale walikua kwa kuiba vyakula vya wanafunzi km maharage! Teh Teh Teh Teh!
 
haaaahhaah Taradadi yule wa Urambo?alikuwa na kama mwarabu fulani na ana manyoya kama nyani nakumbuka cc tulikuwa tunamwita taradadi manyoya alikuwa na sifa ya kungonga wasichana sana kipindi cha UMITASHUMTA
Aah nimecheka mpa basi. Taradadi alikuwa ni mwalimu wa primary school sikimbuki jina. Lakini pia alikuwa ni kocha wa mchezo wa riadhaa. Pia alikuwa ni mwalimu kwenye magwaride ya chipukizi. Siku hizi naona yamekufa. Ila mara ya mwisho nilimsikia kwenye radio kipindi cha michezo akiongea kama Afisa Utamaduni nadhani ni Manispaa ya Tabora kuhusu maandalizi ya mchezo wa riadhaa.

kuna mwalimu mwingine mwarabu alikuwa anaitwa Karim, alikuwa na mguu mmoja mlemavu, alifundisha gongoni primary, ndugu yake adam fundikira alias Adam Maroboti.

adam marobiti alikuwa na demu wake anaitwa salama mahewa. nasikia baadaye alimuoa kama mke wa pili.
 
Yule alikuja akawa Mwenyekiti Wa Chawata Tbr na akaacha kz ya ualimu!

kuna mwalimu mwingine mwarabu alikuwa anaitwa Karim, alikuwa na mguu mmoja mlemavu, alifundisha gongoni primary, ndugu yake adam fundikira alias Adam Maroboti.

adam marobiti alikuwa na demu wake anaitwa salama mahewa. nasikia baadaye alimuoa kama mke wa pili.
 
je matunda ub..oo mmekula pale mbele ya kanisa la roma karibu na shule ya gongoni?
 
*TABORA NA MADAKTARI.
Nikiwa Tabora katika miaka ya 1980s na 1990s nilifanikiwa kufahamu mengi kuhusu Madaktari wa binadamu na maishha yao, kwa kifupi nina wakumbuka hawa zaidi. Dr.Kisenge, Dr.Kobello, Dr.Mohamed.

Kwa mfano Dr.KISENGE
Alikuwa na zahanati yake katikati ya mji pembeni mwa jengo la kampuni ya sigara ikitazamana na Jengo la shirika la Bima(NIC) na benki ya zamani ya CRDB(Benki ya ushirika na maendeleo vijijini).
Alifariki 1994.
Watoto wake watatu wakaja kuwa madaktari Dar, Mmoja Dr.Sabuni(Ni daktari bingwa wa watoto pale Muhimbili), Dr.Peter Kisenge(Ni Daktari bingwa wa Moyo pale Muhimbili) na Dr.George(Ni daktari wa Mifugo, yuko Dar akifanya biashara ya vipuri vya Magari Kariakoo).

Yupo mtoto mwingine wa Dr.Kisenge anaitwa Endrew kwa sasa yupo Dar anakula bata tu, yeye ni kupiga hela na kuponda raha, enzi zile kila mrembo mkali aliyekuwa Uhazili jamaa alikuwa anamsaka kwa udi na uvumba, muda mwingi alikuwa akiendesha Kwa kasi Pikipiki Kubwa XL ya Ofisi(Zahanati), Gari ya Baba yake(Pigot 504) na baadaye alinunua Carina yake Nyekundu ili kusaka warembo, jambo la ajabu ni kuwa marafiki zake aliokuwa nao Tabora na baadhi ya warembo wengi wa Uhazili walikufa kitambo sana kwa Ukimwi lakini huyu jamaa inadaiwa mara zote alipopimwa alikuwa yuko Fit kabisa!!


Aisee, Andrew alikuwa kama mwehu kabisa, nakumbuka hiyo 504 baba yao aliinunua kwa mwarabu gani sijui, ilikuwa rangi ya blue, hiyo gari ilikuwa kali sana aisee, na huyo dogo alikuwa akiiendesha kwa kasi sana, hakuna ambaye hakumfahamu Tbr kwa fujo zake, kuna kipindi walipata ajali mbaya wakiwa safarini Moshi na Landrover yao 109, huyo andrew alikuwamo, kulikua na dereva wao baba yao na mama yao, mama yao nadhani alipooza kabisa au alivunjika mkono kitu kama hicho. Mimi nilikuwa naishi hapo Kampuni ya sigara kwa juu... opp CRDB.

Pia usimsahau Dr Mhina, alimuoa mtoto mdogo kabisa alikuwa anaitwa Cecilia kama sijasahau jina, alimuoa baada tu ya kumaliza form 4.
 
Sikumbuki chochote cha Tabora zaidi ya mabus ya Palaye / Mpalaye (sijui kama spelling nimekosea) yalikuwa yanakwenda Urambo, au ukifika Tabora na train wakati mnabadilisha train kuingia ya Kigoma au ya Mpanda kwa wanaokwenda Urambo, kuna ambao walikuwa wanaibiwa na kila aina ya usanii. Kiukweli Tabora ilitakiwa iwe zaidi hata ya Mwanza kutokana na historia ya kutoa watu wengi mashuhuri kabla na baada ya Uhuru lakini ndio hivyo tena pakasahaulika (huwa nahisi palisahaulika sijui kwa kuwa tangu enzi zile wapinzani wa kweli walitokea pale au sijui wazawa wa pale hawapendi kujenga nyumbani once wanapoenda nje ya mkoa)
 
Back
Top Bottom