Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Aisee, Andrew alikuwa kama mwehu kabisa, nakumbuka hiyo 504 baba yao aliinunua kwa mwarabu gani sijui, ilikuwa rangi ya blue, hiyo gari ilikuwa kali sana aisee, na huyo dogo alikuwa akiiendesha kwa kasi sana, hakuna ambaye hakumfahamu Tbr kwa fujo zake, kuna kipindi walipata ajali mbaya wakiwa safarini Moshi na Landrover yao 109, huyo andrew alikuwamo, kulikua na dereva wao baba yao na mama yao, mama yao nadhani alipooza kabisa au alivunjika mkono kitu kama hicho. Mimi nilikuwa naishi hapo Kampuni ya sigara kwa juu... opp CRDB.

Pia usimsahau Dr Mhina, alimuoa mtoto mdogo kabisa alikuwa anaitwa Cecilia kama sijasahau jina, alimuoa baada tu ya kumaliza form 4.


Mwanangu Wewe ulikua jirani ya Yule kijana Mweupe aliekua anasoma Kitete Shule ya msingi na Milambo? Jina lake nalihifadhi!
 
Nakumbuka familia ya Mwl Kishiki pale Isevya karibia na shule, walikuwapo wasichana warembo sana, Vicky,Edita,Tele na dada yao mkubwa Catherine, sasa wapo Dar. yupo kaka yao maalufu sana Tabora anaitwa Mika, aliisha wai kugombea Udiwani 2005 kupitia CCM,pia alikuwa mfadhili wa timu ya Mirambo enzi hizo ya kina Iddi moshi ,haruna moshi na kakayao.
 
Yule alikuja akawa Mwenyekiti Wa Chawata Tbr na akaacha kz ya ualimu!
Ndo

Huyohuyo, alikuwa anakaa along ile barabara inayotoka isevya kwenda stendi ya mabasi au sokoni, hivi inaitwaje ile barabara? nikumbusheni pliz, kwenye magorofa ya msajili wa majumba enzi hizo.
 
Ndo

Huyohuyo, alikuwa anakaa along ile barabara inayotoka isevya kwenda stendi ya mabasi au sokoni, hivi inaitwaje ile barabara? nikumbusheni pliz, kwenye magorofa ya msajili wa majumba enzi hizo.


Karibia na Duka la bora! Mkuu mtaa na Mimi nimesahau kidogo!
 
Karibia na Duka la bora! Mkuu mtaa na Mimi nimesahau kidogo!

Hahaha umenikumbusha Bora, ni kweli kabisa, unakumbuka zile raba za Morogoro canvas? na chachacha?

kulikuwa pia na Tabora Bazaar kwenye kona ya kwenda bachu, hapa unapata
Suruali za mchemchele na mocassin (vile viatu vyenye mustach).
 
Uyui uwanja-wa-mkutano.jpg round-about-ya-bora.jpg
 
Itaga kulikuwa na bwawa, tulikuwa tunakwenda picnic huko, sijui hata lilikuwa bwawa la nini,


Bwawa la IGOMBE hilo! Ni chanzo kimoja wapo kikubwa cha maji cha mkoa wa Tabora! Ni bwawa kubwa linaextend mpaka ugala na malagarasi kuelekea lake Tanganyika. Tumeogelea sana enzi hizo kwenye matope ya bwawa lile.
 
Bwawa la IGOMBE hilo! Ni chanzo kimoja wapo kikubwa cha maji cha mkoa wa Tabora! Ni bwawa kubwa linaextend mpaka ugala na malagarasi kuelekea lake Tanganyika. Tumeogelea sana enzi hizo kwenye matope ya bwawa lile.


Kweli umenikumbusha linaitwa Igombe, thanks ITEGAMATWI
 
Unambie nini mimi kuhusu Tabora a.k.a Mboka Manyema!!!enzi hizo naenda Tabora Boys,mkikaribia steshen mnaambiwa mchunge mizigo yenu maana mnaingia mkoa wa wezi,kulikuwa na wezi wanaiba mpaka mikate ya boflo iliyotundikwa juu.
Mkoa umejaa vichaa na machizi umwinyi mwiiiingiii,Supa Tall,Athuman Nuna anatembea kajifunga miti mdomoni,Mwajuma Ringa,Rais wa Vichaa Bilali,ukija Ng`ambo unamkuta kichaa Amani..anasoma Quran kama ana akili nzuri.
Vilabu vya pombe vimejaa mitaa ya NG`AMBO,mtaa unaitwa Marando na masempele,usiku ni vibatari na makopa plus karanga,hakuna umeme ni giza...mtaa wa rehani na kwihara,wale Waarabu wa Kwihara kina Nassoro mwarabu...wana kanzu chaafu,wanatembea toka kwihara kwa mguu mpak mjini...Eneo lao wameuza kwa kanisa katoliki Tz.
Waha wanalima miwa mbugani,msimu wa mvua ni uyoga,maembe boribo hadi kipindupindu...karibu na NMB Mihayo branch vijana wanauza samaki,vijana wajanja ni wauza mitumba na dagaa wa mwanza/kg.Mitaa ya mzambaraweni hadi chemchem,ukija Kiyungi unamkuta Digala Fifi,alikuwa na pikpiki na magari ya kubeba mbao yameegesha kwake,alikuwa na kashfa ya ngoma...
Watutsi kibao mtaani...ng'ambo mtaa wa mboya kulikuwa na watutsi weusiii kulwa na dotto,mabucha ya nyama ndio kazi zao,Wapi Samuel mitaa ya National??Wapi Mtaa wa Makaranga na Mpepo meya wa zamani??I miss Mboka Manyema
 
Duh!! Wewe unakumbuka sana shule ya Mazoezi Mwenge. Huyu Mwalimu Chiboni alikuwa headmaster, alikuwa anajua kiingereza kizuri na fasaha sana but alikuwa Mlevi wa Pombe, Alikuwa mwenyeji wa Dodoma(Mgogo) na mara ya mwisho nilimwona 1993 Salanda-Dodoma nikipita na treni akiwa hana chochote.
Pia kulikuwepo na walimu wengine kama:
1/Mwalimu Shigela(Inadaiwa huyu mama alianza kufundisha na Nyerere enzi za Mkoloni, alinifundisha kusoma na kuandika!!)
2/Mwalimu Mihayo.
3/Mwalimu Pongo(Nilisikia huyu mama alikufa kwenye ajali ya Mv Bukoba 1996)
4/Mwalimu Husein.
5/Mwalimu Maduhu.

Sijui kama unakumbuka ile mihogo mizuri ya kupikwa iliyokuwa na Pilipili ikiuzwa wakati wa break?

Mwalimu Shigela pamoja na Mwl Gertaback (RIP wote) hawa walinifundisha darasa la kwanza pale Mwenge Shule ya Mazoezi. Pia, Mwalimu Maduhu huyu fimbo zake zile za mianzi zilikuwa balaa, yaani wiki yake ukichelewa basi unamvizia akiianza tu ile corridor ya kuelekea ofisi ya Mwalimu Mkuu, basi wewe unatoka baru tokea pande za Uwanja wa Vita hadi kwenye zile ngazi zilizopo upande wa Magharibi unapanda fasta unazama class, sasa kuna kipindi alishtukiaga, akawa akiianza ile corridor wanafunzi si wanajua mpaka aimalize ile L utamuwahi tu, basi yeye ilikuwa akifika kati anarudi tena huku alipotoka, basi wewe umetoka baru ili umuwahi, hamadi mnakutana uso kwa uso na wewe upo katikati ya ule Uwanja unakatiza, unakuwa huna jinsi unajisalimisha tu kwa bakora moto moto. Hiyo ilikuwa miaka ya early 90's. Classmets wangu walikuwa akina Haruna Moshi "Boban", Nuru Mchemba, Mustapha Muhando, Noah Kiula, Doto Modest, Daniel Gertabark (Huyu alikuwa ni mtoto wa Mwl. Gertabark R.I.P) etc.
 
Nani anamkumbuka yule mchonga mihuli wa pale karibu na duka la Bora, alikuwa anaitwa Mudi, alikuwa na pikipiki Yamaha, jamaa baadaye alikuja kuwa na hela ghafla, watu wakawa wanahisi alikuwa apiga deal za Bank na mihuli yake, alikuwa anaweka Curl kwenye nywele zake na kuvaa manguo marefu ya gharama enzi hizo (kama ya Ki-Nigeria hivi)
 
Back
Top Bottom