Ntuzu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 17,418
- 10,877
- Thread starter
- #321
Aisee, Andrew alikuwa kama mwehu kabisa, nakumbuka hiyo 504 baba yao aliinunua kwa mwarabu gani sijui, ilikuwa rangi ya blue, hiyo gari ilikuwa kali sana aisee, na huyo dogo alikuwa akiiendesha kwa kasi sana, hakuna ambaye hakumfahamu Tbr kwa fujo zake, kuna kipindi walipata ajali mbaya wakiwa safarini Moshi na Landrover yao 109, huyo andrew alikuwamo, kulikua na dereva wao baba yao na mama yao, mama yao nadhani alipooza kabisa au alivunjika mkono kitu kama hicho. Mimi nilikuwa naishi hapo Kampuni ya sigara kwa juu... opp CRDB.
Pia usimsahau Dr Mhina, alimuoa mtoto mdogo kabisa alikuwa anaitwa Cecilia kama sijasahau jina, alimuoa baada tu ya kumaliza form 4.
Mwanangu Wewe ulikua jirani ya Yule kijana Mweupe aliekua anasoma Kitete Shule ya msingi na Milambo? Jina lake nalihifadhi!

