Kwa wale wanaolalamika kupanda kwa gharama za vifurushi vya internet hii ndio mitandao ya kuhamia kwa sasa

Kwa wale wanaolalamika kupanda kwa gharama za vifurushi vya internet hii ndio mitandao ya kuhamia kwa sasa

Habari ya wikiendi wana JF wenzangu.

Jana baada ya kutoka mishemishe jioni si nikasema ngoja nitumbukie vocha nichungulie kinachoendelea mitamdaoni.

Nikapita dukani nikanunua Zantel ya 500 dhumuni nijiunge cha chuo ambacho ni MB 500 kwa siku 7 maana sina matumizi mengi ya data.

Ile kupiga *148*05# nakuta kuna MB 250 pozi likaniishia nikajisemea ngoja nichungulie kwenye mitandao mingine kupoje. Eni wei ifuatayo ni mitandao ambayo ina vifurushi pengine ni nafuu kwa mteja

1. HALOTEL
Hawa jamaa ili upate MB za maana unatakiwa uweke salio kwenye Halopesa kisha piga *150*88# kisha chagua namba 3 utachagua Mega Bando
Tsh 1000 = GB 1 kwa siku 7
Tsh 3000 = GB 3 kwa siku 7
Tsh 500 = GB 1 saa 6 usiku mpaka 12 asubuhi

2. TTCL
Wana bando lao linajulikana kama BANDO TAMTAM sharti uwe na salio kwenye T PESA yako
Tsh 1000= Dk 10, SMS 50 na GB 1.2 kwa siku 5
VIpo vipo vingine ni
Tsh 500= 300 MB

3. VODACOM
Wazee wamepunguza bando mpaka basi yaani hata zile ofa za DAR SUPA UNI wamezibadilisha kabisa.

4. TIGO
Hawa sijui huko hali yako ipoje?
Kw wale mnaojiungaga na SAIZI YAKO najua mnafahamu kilichobadilishwa huko.

5. ZANTEL
Hawa ni Tigo waliochamgamka. Walikuwa na vifurushi vizuri mno, walipigiwa sana chapuo na bwana Extrovert mpaka ikanipelekea kusajili laini yao.
Lakini walichokifanya ni balaa.

6. AIRTEL
Hawa jamaa hata ukipiga *149*81# wamebadilisha kila kitu, hata kile kifurushi chao cha USIKU kuanzia saa 6 hadi 12 asubuhi ni mazingaombwe tu.
Weew vuta picha yaani ukae mpaka saa 6 usiku kwa ajili ya kujiunga MB 375 just imagine!


Mwisho kabisa nawashauri mrudi HALOTEL tu maana hakuna mambo mengi kule MB kama zote.
Tigo saizi yako, 2,000 gb 1.3, dkika 250 mitandao yote siku saba
 
Voda nilikuwa nateleza kwa buku napata Gb leo wameitoa sasa majeshi yangu nahamishia kwenye mtandao wa Halotel .
 
Nadhani halotel wapo vizuri zaidi kuliko mitandao mingine hao Voda GB zao ni kama wanatoa nusu zinakimbia kama upepo..
 
Wazee wa IT Mliopo humu.
Is it possible raia wa kawaida tu aka hack mitandao let's say tiGO na kumuunganishia mtu GB kibao kwa Bei poa?
Kuna hacker kanipa ofa ya 10 Gb kwa wiki kwa elfu tatu. Sharti lake kuu nimtumie pesa ndio aniunganishe.
I am asking for a foreign friend.
 
Sasa huku kanda ya ziwa hio zantel ata vocha tu kuzipata ni tabu.

Ngoja tujikongoje na halotel tu
 
Na idea ya kujirecord navunja line flan nasajili line ya upande wa pili mwenye 📷 nzuri ya smartphone tuonane
 
Halotel wana vifurushi nafuu sana. Kama sina ishu serious, najiunga kifurushi chao cha 5,000 napata GB 7.

Lakini speed yao ni ndogo, hivyo bora niendelee kutumia tu Vodacom pamoja na ughali wao.
 
Hata namjua basi huyo mmiliki mkuu,, mwenzio mie najua kutumia tu
Ahahhaahaa noma sana, Jamaa ni true icon ya "mpambanaji". Ashawahi kupambana na mugabe mahakamani miaka ya nyuma huko daaah ana historia ngumu sana huyu mzee. Lakn badae alikuja kufanikiwa na ndo anamiliki hili kampuni.

Anaishi zake London huko na
Wanamwita "Zimbabwean billionaire based on London".
 
Ahahhaahaa noma sana, Jamaa ni true icon ya "mpambanaji". Ashawahi kupambana na mugabe mahakamani miaka ya nyuma huko daaah ana historia ngumu sana huyu mzee. Lakn badae alikuja kufanikiwa na ndo anamiliki hili kampuni.

Anaishi zake London huko na
Wanamwita "Zimbabwean billionaire based on London".
Ohk ahsante mkuu nilikuwa sina hili
 
Back
Top Bottom