Kwa wale wanaolamika kuhusu Diesel Engine. Uliza chochote nkupe jibu

Kwa wale wanaolamika kuhusu Diesel Engine. Uliza chochote nkupe jibu

Diesel engine nyingi zinawekwa heater plugs kwenye engine block na ziwe zinaelekea ndani ya cylinders, idadi ya heater plugs iko kulingana na idadi ya cylinders...

Kazi ya heater plugs ni kuwarm engine cylinders wakati wote unapojaribu kuwasha gari lako, kwenye haya magari au small engines, wakati wa baridi engine yako inakuwa imepoa sana hasa eneo muhimu ndani ya cylinders zako na kuna wakati kunaweza hata kuwa na unyevu au kuganda kwenye nchi za baridi... unapoingiza hewa na kuicompress (compression stroke) huku cylinders zako zikiwa za baridi basi wakati wa TDC (top dead center) hiyo compressed air itafika hapo ikiwa yabaridi japo umeicompress na at the end hata inapofanyika Diesel injection mlipuko hauwezi kutokea...

Cylinders zako au chemba zinakuwa pre-heated na heater plugs ili kuwa na joto na hata compression ikifanyika basi hapo TDC joto la hewa yako halitaathiriwa na hali ya cylinders zako maana tayari ziko na joto na mlipuko utafanyika kirahisi.

Heavy engines huwa nyingi zinawekwa fuel heater ndani ya fuel tank na kupreheat mafuta yenyewe hivyo yakiwa pumped kwenye combustion chamber tayari yanakuwa na joto na combustion inakuwa rahisi.... kuna baadhi ya heavy diesel engine pia zinakuwa na kitu kinaitwa ether starting aid kwa ajili ya kupasha joto diesel
Nimekupata mkuu, tena kwa hapo ulipozungumzia starting fluid (ether) nikaona kweli haya mambo unayapata vizuri.

Ila huwa wanasema endapo ether ikiwa unaitumia mara kwa mara basi hiyo engine inaweza pata uraibu, yaani pasipo ether inakuwa na hard start. Je hiyo kitu ni kweli?
 
Uko sawa, na ongezea labda kupinda kwa cylinder head.
Mara nyingi hupinda kama ili overheat au wakati wa kuifunga haikufungwa kwa mtiririko unaotakiwa na mtengeneza mashine. Huyu alisema walifungua kwa sababu ilikuwa ikivujisha oil.
 
Shukrani mkuu, ila hujatoa sababu.
Diesel haiunguzwi na cheche kama kwenye gari za petroli. Kwa hiyo hakuna system ya plugs ambazo kwenye petroli huwekwa umeme na kulipua petroli ndio ifanye mzunguko ktk engine. Diesel yenyewe hurushwa katika cylinder kwa mfumo wa mvuke (mfano wa mvuke kutoka kichupa cha pafyumu) na baada ya valvu kufunga piston inagandamiza huo mchanganyo ndio mlipuko hutokea.
Nyakati za baridi wameweka heater plugs ambazo huanza kupasha moto ndani ya cylinder kwa sekunde kadhaa ili kusaidia ule mlipuko wa kwanza na kikawaida gari ikishapata joto huhitaji tena.
 
Mkuu hebu nipe madini kuhusu mfumo wa HE unit injector.
images (67).jpeg
 
Hydraulic Electronic diesel injectors. Kwa urahisi ni kuwa, mifumo ya sasa ya magari inakwenda zaidi kwenye computer based systems, kwa hiyo ili kuweza ku control gari, unahitaji uwe na connection ya umeme, possibly kwenye kila kitu. Tulizoea engine zenye injector pump ambazo ndiyo zilikuwa zinasukuma mafuta-diesel kwa pressure halafu injectors zinanyunyiza ndani ya chemba kwa mfumo wa mvuke. HE injectors sasa zinafanya kazi zote mbili, kusukuma diesel, na kunyunyiza kwa kufuata command ya computer ya gari.
 
Bongo kuna vitu huwa tunavichanganya sana

Qualification na experience

Ni nadra sana kwa mafundi wengi wa bongo kuwa na hivyo vitu viwili kwa pamoja hiyo inatokana na sababu za kimazingira.

Humu jukwaani wengi wana qualification but wamekosa experience believe me or not.

Watu wengi wenye qualification ni wabishi sana kupata experience kwasababu wanaamini walichojifunza kwenye vitabu basi ndio hicho hicho kilichopo kwenye troubleshooting, thats totally wrong.

Ukiwa na qualification jitahidi sana kujishusha nenda garage na kwenye kichwa chako ufute kabisa hicho unachokiamini mpaka pale utakapopata experience ya kutosha,, one day utakuja kunishukuru

Hii kitu nimeisema sio kwakukurupuka, nimepitia nyuzi nyingi sana zinazohusiana na mambo ya ufundi na nimeona hii weakness

Pia watu wengi wenye experience ni wavivu wa kujiendeleza kujua ulimwengu wa engineering unaendaje kwa sasa.

Gari aina ya crown na nyingne nyingi zinawasumbua wabongo wengi kwasababu ya hawa mafundi wenye experience na hawataki kujiendeleza

Bongo magari mengi hayana shida ila shida ipo kwa mafundi (hapa ni wote) wenye experience wakishirikiana na hawa wenye qualification
 
Nakuunga mkono.
 
Mkuu hiyo compressor yako kama umefanya vyote hivyo na tatizo linaendelea, adjust pressure ya upepo kwenye relief valve ya upepo, kinatochotoke hapo engine overload kwa maana upepo kama load yako unaoverload engine... hapo inatakiwa setting..
Sawaa nitajaribu kumuona fundi
 
Diesel inamanisha Nguvu. Ndio maana kwenye Heavyduty Machine nyingi znatumia Diesel
Mmmmmmhmn bro, umeanza kuharibu uzi mapema sana na hili tangopori. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Diesel ni jina la mtu hilo.
 
Je kuna uwezekano wa kuiswap system ya engine inayotumia diesel ili ianze kutumia petrol? Na ya petrol itumie diesel..
Hii niliona imefanywa kwenye engine ya Land Rover 110 na 109. 110 Ilibadilishiwa mfumo chap ikawa inatumia Petrol badala ya diesel.
 
Overhaul inahitaji umakini sana. Ni muhimu sana sana kupata manual ya hiyo mashine ili kujua wao wanahitaji vipimo gani kwenye kila bolt na nati unayofunga, siyo kutumia uzoefu. Maana kwenye cylinder head mfano, engine nyingi wenyewe wanataka zile main bolts za cylinder head kuwekwa mpya kila ukifungua. Na zenyewe zina specification zake siyo kila bolt itafaa.
Nimejifunza kitu
 
Haiwezekan kk. Tofaut btn Diesel na Petrol Engine n.
Diesel kuna Nozzle, Wakat Petrol kuna Spark plug.
So kubadilisha inakuwa ngumu sana mkuu. N bora ubadilishe Engine yote 2
Je nozzle huwa zinasafishwa kama plug au ni kununia mpya tu?
Pili nozzle zikichoka utaona mabadiliko gani kwenye gari?
 
Back
Top Bottom