Kwa wale wanaopenda muziki kwenye gari, tukutane hapa

Kwa wale wanaopenda muziki kwenye gari, tukutane hapa

Kati ya mziki ambao unanua woofer ambayo ina inbuilt amplifier na anbao unakuwa ni passive woofer inayounganishwa na booster, ni upi mzuri?
Kwa ushauri wangu Passive speaker ni nzuri zaidi(spika isiyo na amplifier ndani) hii inakupa uhuru wa kuunda Mziki uutakao mfano unapokuwa na amplifier ya nje inayojitegemea tambua iyo Amp inakuwa na channel mfano channel 1,2,3 Hadi 4 Sasa hapo upo HURU kuongeza Spika ama kubadili mfumo wa spika hasa Subwoofer, pili nirahisi kutatua tatizo linalotokea kwa iyo Amp ama spika kuliko Active sp ambayo lazima ufungue lile box ili ujue shida IPO wapi.
 
Je kwa nini woofer ya 2500w ya gari haiwezi kutoa mzki mkubwa kuzidi proffessional woofer ya 1000w mfano kama oppra?
Hapo shida ni UBORA ama ukweli, unaweza kukuta iyo 2500w ni P. M. P. O watts wakati RMS watts ikiwa ni 400 ,Sasa iyo professional Kama oppra unakuta iyo ni real watts Yani 1000 rms
 
Yani music ni kelele kwangu.
Yaani wewe, engekua tunajuana kwa macho, ningekuomba lifti kwenye yako, ila nikiwa na gari yangu, nikukwepa, kutembea na gari yangu ikiwa kimwa, siwezi mziki ni chakula ubongo wangu, ila siyo huu wa kizazi cha akina Diamond na Hamonize. Angala wa kizazi cha akina Lady J.dey, Dataz, Dudubaya, Mwana FA na kurudi nyuma akina Akina Uda jazz, DDC OSS na wenzie.
 
Nina mziki huu kwenye gari...

1. Head Unit: PIONEER (AVH-ZL5150BT);

2. Amp: JVC 1000watt;

3. Speaker/Subwoofer: PIONEER TS-WX306B 1300w MAX;

4. Twitta: PIONEER;

5. Equalizer: Haipo (haikuwekwa, sijuwi kwanini).

Sasa nahitaji UPGRADE...

A. Kuweka head unit 'full android'. Brand gani ni the best na durable? Hizi Chinese au Korean brands.

B. Kati ya AMP na SUBWOOFER (tajwa hapo juu) nataka upgrade kimojawapo ili kusave cost. Niupgrade ipi kwa watt ngapi na brand gani?

Napenda mziki heavy haswa with quality!! ule mkito wa kuusikilizia kwenye moyo kwa walioko nje ya gari. Mziki 'mzito' na siyo makelele.

Naombeni ushauri wenu wakuu na wataalaamu . Gari ni Toyota ist.

Osaba , Extrovert Naligia Mninoi
 
Kama una head unit(radio) tafuta spika ya Sony watts 1800 ukikuta zilizo kwenye tube original ni nzuri zaidi, tafuta amp ya boschmann ya watts 1300 original pamoja na pre amp yake(equalizer) nayo ni iwe kampuni hiyo ya boschmann tafuta na set ya wiring, ukishapata hivyo tafuta fundi umpelekee akufungie huo mziki utakuwa umesave hela nyingi sana maana ukienda mwenyewe kichwa watakupiga hela

Hivi mkuu, EQUALIZER ni kitu cha lazima kuwepo? Mimi nilifungiwa mziki pasipo equalizer. Aliweka vitu vinne tu: head unit; amp; speaker/subwoofer; na twita.
 
Hivi mkuu, EQUALIZER ni kitu cha lazima kuwepo? Mimi nilifungiwa mziki pasipo equalizer. Aliweka vitu vinne tu: head unit; amp; speaker/subwoofer; na twita.
Mziki bila EQ unapiga kweli ila hutaweza kuutwist Mfano mi napenda mziki ule wa kusikika nje kishindo ila bila EQ huupati. Ndani utajaa ila nje huwezi kuutoa ukawa unamwagika kwa vishindo. Unakuwa kama wa subwoofer za kichina
 
Mziki bila EQ unapiga kweli ila hutaweza kuutwist Mfano mi napenda mziki ule wa kusikika nje kishindo ila bila EQ huupati. Ndani utajaa ila nje huwezi kuutoa ukawa unamwagika kwa vishindo. Unakuwa kama wa subwoofer za kichina

That's how it is kwenye huu mziki wangu (head unit: PIONEER AVH-ZL5150BT, amp: JVC 1000W, speaker: PIONEER TS-WX306B 1300W MAX, twita: PIONEER).

Kwa ndani unakita kiasi chake, lakini kwa nje haumwagiki.
 
sana tu, utapata vizuri low freq,mid na hi freq. mi mwenyewe tu mziki wa nyumbani situmii bila EQ

poa mkuu. nitaweka EQ kwenye hii JVC AMP (1000W) & PIONEER SUBWOOFER (1300W) nilizonazo sasa. Na kuna mdau hapo juu alishauri kwamba huwa ni vyema kuweka AMP yenye watts kubwa zaidi kuizidi speaker/subwoofer ili kupata mziki safi mzito wenye kishindo cha kutikisa maini!
 
Back
Top Bottom