INAUZWA Kwa wale wanaoteseka na maji ya chumvi pata machine ya kuchujia maji chumvi kuwa maji baridi

INAUZWA Kwa wale wanaoteseka na maji ya chumvi pata machine ya kuchujia maji chumvi kuwa maji baridi

kiongoz hujanielewa.. yaan kutumia chlorine kwa ajili ya kusafisha maji ni muhimu kwa ajili ya kuondoa bacteria na parasites...na mara nying inashauriwa mara moja kwa mwaka ...

na pia cholorine inatumika kuua bacteria sio kuondoa chumvi kama itaondoa ni kias kdg sana... maana inategemea maji yako ladha yake ya chumvi ni ya aina gani..

mostly utakuta ni kutokana na madini chuma kuwa mengi.. ndo unakuta maji yanakuwa na ladha kama ya chuma.. au mengine kama magadi.. au unakuta yana rangi ya kutu au kama mayai yameoza.. sasa hapo chlorine haiwez toa hiyo chuma

chlorine ni kwa ajili ya ku purify maji inaua bacteria na parasite sababu kuna uchafu wa kinyesi au mizoga ya wanyama mvua ikinyesha maji yanabeba huo uchafu yanakwenda kuingia kwenye kisima chako .

Ndo maana hata dawasco wanatumia chlorine kwenye vyanzo vyao vya maji ingawa maji yake ambayo ni ya mito hayana chumvi..

so tumia chlorine sambamba na filter za kuondoa chumvi.. na filter hizo hizo ndo zitaondoa chlorine kwenye maji yako na kuyafanya yawe salama kwa kunywa

kama kisima kina maji ya chumvi hakuna dawa ya kutumbukiza kisiman chumvi iondoke hapana kuna filters zinatumika kuondoa chumvi na madini chuma yaliozid ingekuwa hivyo watu

wasingehangaika kupata kisima cha maji yasio na chumvi mtu angechimba tu kisima akaweka chlorine ndan akawa anamimina kwenye kisima na wala hizo system za kuondoa chumvi kwenye maji zisingekuwepo

umeona kuna mdau kataja reverse osmosis ni moja wapo ya teknolojia ku soften hard water na kuyafanya safe for drinking

mi mwenyewe natumia kisima nyumban na niko kwenye process ya kufunga filters ndo maana nimamuuliza huyu mtoa mada filter nazohitaj kama anazo ama niagize nje

do your research kuhakikisha unajua unahitaj nn kutokana na aina ya maji yako .. na pia kumbuka sijasema usitumie chlorine ila jua inashauriwa kufanya chlorination kwenye kisima chako once a year..

kumbuka kuna filter za aina nyingi kutegemea na aina yako ya maji na uchafu au ugumu wa maji yako

filter za uchafu unaoonekana zinaitwa kwa kifupi sed filters ziko kuanzia 20micron na kwenda juu the bigger the number the bigger the holes

za kutoa uchafu wa aina ya vumbi hadi ule usionekana kwa macho ni micro 5 kushuka chini

za kusafisha maji na kuondoa bacteria zinaitwa carbon filters .. na hiz zinaondoa harufu ya maji pia na ndio nazokwambia tumia ili ukiweka chlorine kwenye kisima hizi zitaondoa hiyo chlorine pia ..
hizo filter za kuondoa magadi na chumvi chumvi zinaitwaje mkuu ?Na je kama shida yangu ni chmvi tu naweza kufunga hiyo filter moja?Google inanichanganya
 
Uarabuni wanabadilisha maji ya chumvi yabahari kua fresh water
Uarabuni Nishati ni ya Kumwaga..., Hio njia kwao ndio cost efficient; unadhani wafanye nini mkuu wachimbe dimwi lijae maji ya mvua ambazo ni chache ?
 
hizo filter za kuondoa magadi na chumvi chumvi zinaitwaje mkuu ?Na je kama shida yangu ni chmvi tu naweza kufunga hiyo filter moja?Google inanichanganya



Kaka chumvi unaweza kuiondoa kwa kufunga reverse osmosis.. kuna teknolojia tofauti

Kuna teknolojianya kutumia special
Beads Salt tanks .. kuna ya kutumia magnetci bar.. kuna ya kutumia UV light..

Ila mfumo wa kuondoa chumvi kwenye majo ni expensive .. kwa jinsi unavyotaka kusafisha ujazo mkubwa wa maji na ndo gharama zinakuwa kubwa
 
Mbona hamuweki maelezo na gharama za machine hapo ndio mnaponichoshaga wafanyabiashara za online
Wabongo bana. Wanashindwa kusema kuwa concentration ya kiasi fulani Cha chumvi mashine yake Bei Ni hii
 
Kaka chumvi unaweza kuiondoa kwa kufunga reverse osmosis.. kuna teknolojia tofauti

Kuna teknolojianya kutumia special
Beads Salt tanks .. kuna ya kutumia magnetci bar.. kuna ya kutumia UV light..

Ila mfumo wa kuondoa chumvi kwenye majo ni expensive .. kwa jinsi unavyotaka kusafisha ujazo mkubwa wa maji na ndo gharama zinakuwa kubwa
Kwa maji magumu sana softeners zenye resins ni cost effective sana maana zile resins zinakuwa charged na common salt wakati total hardness inapozidi, then maji yakitoka hapo hupita kwenye Ro to Uv filters.
 
Yeah haya yote wafanyabiashara wabongo huwa hawaweki wanataka mteja awafate huko badala ya kuweka kila kitu Ili mteja akija anafahamu.
Wanafanya hivi maana kitu unakuta bei yake halisi ni elf 10 lakini kinaeza kuuzwa elf 50 kwa mteja wa 1, elf 20 wa pili na elf 15 wa 3

Kiufupi wafanyabiashara wengi wa bongo ni wapigaji hawana bei fixed wanashindwa kujua kua biashara ya kitu cha bei ya chini ukiuza kwa wingi unaeza pata faida zaidi ya kuuza kitu bei ghali kwa watu wachache.

Tatizo ni njaa kali tu. Tuwaelewe na twende nao sambamba.
 
Back
Top Bottom