Wakuu mie huwa napiga 70, kwa mkupuo, kisha naanza kushuka hadi 20. Nimeanza kupiga toka 2003.
Ila kuna kipindi niliacha km miez sita, nilipokuja kuanza kupiga push up. Sikuweza kufikisha 70 kwa mara moja.
Ila nimekomaa hadi nimeanza kuweza.
Tatizo uzito umeongezeka toka 82kg hadi 89.
Na urefu wangu ni cm 178. Kimsingi huwa napiga zoez ili kilo.zipungue. kwan nataka niwe na 75-80. Ila shida, navyozidi kupiga push up uzito unaongeza sana. Na bado najitahidi niwe nakula sana mchana tu, asubuhi sili, usiku ni matunda tu au karanga.
Je nifanye ili uzito upungue na usiathiri routine yangu?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kaka hakuna kitu kibaya kama ku skip Breakfast au kula kidogo
Muulize mtaalamu yoyote duniani wa mambo ya health and nutrition atakwambia kuna kanuni kubwa 1 ya kupangilia quantity ya chakula nayo ni "Take your breakfast like a KING, take your lunch like a PRINCE and take your dinner like a BEGGAR" Ingawa ni kinyume cha uhalisia wetu wabongo lakini ndio kanuni nayo ni hivi
1. Asubuhi inabidi tule chakula kingi kama vile tufanyavyo kwenye Lunch. Hapa ikiwezekana ugali na ndondo uliwe
2. Mchana inabidi tupunguze iwe kama mazoea yetu yalivyo kwenye Breakfast. Hapa kikombe cha Chai na Bites kidogo sio mbaya.
3. Wataalamu wanasema hapa bilauri ya maziwa au vipande kadhaa vya matunda au Salad vinatosha.
Kiakili ya kawaida ukichunguza sana inakubalika. Ikumbukwe energy kubwa mwili + akili hutumika kati ya saa 1 asubuhi mpaka saa 5 asubuhi hivyo chakula chote kinachotumiwa wakati huo humeng'enywa vizuri muda huo. Kuanzia saa 6 kuendelea kazi huanza kupungua mwili hauitaji energy nyingi na mida hii ukila chakula kingi kama tunavyofanya unaanza kusikia mwili umechoka kausingizi kanaita, lakini kama utapiga kakombe ka chai na bites ule mzigo wa asubuhi unaendelea kumeng'enywa vizuri na mwili bado unaendelea kuwa mwepesi.
Tatizo zaidi linakuja kwenye dinner kwa sababu mida hiyo ndio tunakuwa home, na wapenzi wetu ndio wanapata nafasi ya kutupikia tukipendacho, na inawezekana kabisa milo mingine tuka skip lakini sio dinner maana kesi yake kwenye ndoa inabidi ipelekwe The Hague. Hapa ndio tunapofakamia chakula kingi na mafuta mengi ambacho hakitumiki kabisa kwa sababu baada ya muda huenda kulala. Na si aghlabu ukakuta tunatumia chakula kama appetizer ya usingizi. Inatakiwa gap ya dinner na kulala isiwe chini ya masaa manne ikipungua hapo chakula choote (hasa wanga na protein) hushindwa kumeng'enywa na hupelekwa ktk group la cholesterol au unconverted fats. Hizi unconverted fats ndio hii hujitokeza kama vitambi, makalio makubwa, na manyama uzembe ya mbavuni
Hizi unconverted fats ndio sababu kubwa ya Kisukari, Pressure, Cancer na Figo kuathirika
Hivyo ndugu usipunguze au kuruka Breakfast bali ongeza na punguza hiyo milo mingine
Wakati unakula kumbuka portion 4 za tumbo lako 1/2 chakula + 1/4 maji + 1/4 emptiness au hewa
Kumbuka mboga mboga na matunda kwenye mlo wako navyo ni muhimu
Vile vile usisahau tunakula ili tuishi, hatuli ili tufurahi au turidhike(to enjoy). Na ndio maana vyakula vingi ambavyo vinaupa mwili nguvu, nuru na uhai ladha yake mdomoni imekuwa sio maridhawa sana mdomoni ukilinganisha na mapocho pocho na mahanjumati yanayoharibu miili yetu
Wakatabahu
Sent using
Jamii Forums mobile app