Kwa wale wenye tatizo la kusikia tupeane ushauri mbinu za matibabu na changamoto tunazokabiliana nazo

Kwa wale wenye tatizo la kusikia tupeane ushauri mbinu za matibabu na changamoto tunazokabiliana nazo

Km ukweli una shida nitafute mkuu nitakupatia 0620552992

Kwakweli nilipata hili tatizo miaka 17 iliyopita. Ila nashukuru sikuwai kupata manyanyaso yoyote mpk namaliza masomo yangu ya IT mpk chuo na hii yote kutokana na kukubali na kutoficha na darasani nilikuwa desk ya mbele kabisa na teacher akiwa anafundisha walikuwa wananijali sana nashukuru sana hadi mtaani pia ingawa wachache hupenda tu kukutest kwa kukutukana makusudi ili mladi tu kukufanyia dhihaka me huwa siwajali na nawahitimishia waone sijasikia...
Mkuu upo Dar es Salaam maeneo yapi aise nimeku txt mda huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenye matatizo kama haya, tusaidianane ni namna gani MNA pambana, je Hali hii inarekebishika? Nina miaka 24 na hili tatizo. Siku hizi ndio kabsa usikivu umeisha Hali ni mbaya, na tinnitus inanitafuna vibaya Sana.

Mateso wanayopitia watu wa hivi, sio mchezo.

RIP brother Mpauko
 
Wenye matatizo kama haya, tusaidianane ni namna gani MNA pambana, je Hali hii inarekebishika? Nina miaka 24 na hili tatizo. Siku hizi ndio kabsa usikivu umeisha Hali ni mbaya, na tinnitus inanitafuna vibaya Sana.

Mateso wanayopitia watu wa hivi, sio mchezo.

RIP brother Mpauko
Ni kuendelea kujifariji na kumtanguliza Mungu wa mbinguni mbele..Cha muhimu. kujikubali na kuona kuwa ni hali ya kawaida...
 
thales, Same here mimi ilinianza baada ya kuchoma sindano za quinine kutibu maralia kipindi niko shule ya msingi yakawa yanaziba yanazibuka mpaka naingia sec wazazi wangu sio watu wa kujali nilivyofika form2 ndio wakanipeleka muhimbili nikapimwa usikivu ikaonekana sikio la kulia halisikii kabisa na la kushoto linasikia ila limeanza kuaffectiwa kama anavyosema mkuu hapa nilipewa Bcomplex tu nikaambiwa Mungu akijaalia litazibuka lenyewe niache kukaa kwenye makelele, nisile kisamvu wala mihogo.

nikaendelea tu na shule aisee mkuu asikwambie mtu nimesoma kwa shida nmeishi kwa shida sana unapitia manyanyaso/wakati wmingine unakua kama kichekesho, hio hali imenibadilisha mentality yangu kabisa hadi leo mimi sipendi kukaa na watu nakaa na mtu ambae hajagundua kama nina ilo tatizo akishajua tu anaanza kunitreat tofauti na mm huwa sipendi kabisa kama ni urafiki utaisha na hata kama nilikua nasikilizana nae basi nitakua ndio simuelewi kabisa kwakifupi tatizo liko zaidi kwenye mishipa ya fahamu kadri unavyokata tamaa ndivyo unazidi kuwa husikii.

Nikikaa kwenye maspika makubwa nakua kama nataka kupoteza fahamu wakati meingine navaa earphone isiyokuwa na mziki ili tu kujiepusha kupeana Hi na watu mana inakua kero saa ingine .wakati mwingi sio kwamba sisikii unakuta nasikia ila sielewi mtu anaweza niambia kitu nikamsikia ila sijamuelewa inabidi aongee herufi kwa herufi.

Yotekwa yote nmeshaizoea hali yangu,pia hali ya kuwa sichangamani sana na watu nishaizoea hali ya kupenda kuwa kwenye mazingira ya utulivu sana huwa sipendi kukaa mahala kuna sauti nyingi zinanidisturb ila ili ujue Mungu analipa kuna watu wawili walikuaga wananinyanyasa zamani mmoja shule mwingine om wameumwa sasa wao sio half_deaf ni hawasikii kabisa.mpaka kuizoea hii hali ilinigarimu miaka 6
Pole sana Bro..
 
Back
Top Bottom