View attachment 3694127
Same to me mkuu , upande wa sikio la kushoto niliambiwa nahiyo shida ngoma ya sikio imetoboka sababu ya infections za sikio nilizokuwa napata tangu nikiwa mdogo😥.
Olevel nimesoma vizuri tu na sikuwahi kujua kuwa nitakuja kupoteza usikivu ukubwani.
Tatizo likaanza kukolea wakati niko advance japo pia sikuwa nimegundua bali baadhi ya watu walikuwa wakiniambia sisikii vizuri.
Sasa mpaka nafika chuo hali ndo ikazidi kuwa mbaya ,Inshort chuo nimesoma kwa tabu sana japo namshukuru Mungu nimegraduate mwaka huu .
Kwenye vipindi nilikuwa nahudhuria kama mtazamaji tu nikitoka chuo ndo natafuta slides ili nisome vizuri nielewe alichokuwa anafundisha mwalimu.
Sometimes wanafunz wenzangu wamekuwa wakinininyanyapaa kwa kunicheka kuwa mie ni kiziwi ,huwa najisikia vibaya sana.
Unaweza kuniambia sentensi hii mie nikasikia sentensi nyingine kabisa.
Kinachonikatisha tamaa zaidi ni kuona watu wakisema kuwa dawa hamna inabidi kuzoea ndo nachoka kabisa.
Nimeambiwa niende KCMC au Muhimbili kwa ajili ya kuzibwa hiyo ngoma ya sikio sasa sijajua gharama zake zitakuaje