Kwa wale wenye tatizo la kusikia tupeane ushauri mbinu za matibabu na changamoto tunazokabiliana nazo

Kwa wale wenye tatizo la kusikia tupeane ushauri mbinu za matibabu na changamoto tunazokabiliana nazo

Mm nilipata ajali baada ya mda hali ya masikio kutokusikia vyema ikaanza nikaanza tiba ila haikusaidia nikanunua hearing aid lakini nazo ukivaa zinazingua tu nasikia kama nyenzeee ..Nimeamua kukaa hivyo hivyo
 
Shukurani Sana kiongozi, hearing loss inasumbua watu wengi mno na tinnitus ni balaa, hata kulala vizuri muda mwingine ni changamoto. Bado jamii inayotuzunguka nayo ni changamoto, hii ina sababisha maisha ya watu wenye shida kama hizi,, kuandamwa na depression Kali na social isolation.
Cha muhimu ni kujiamini tu kila mtu anamatatizo yake hakuna ambae hana kabisa.
 
Daah! Nishakujibu vipimo, majibu yake ndio hayo, kuna matundu kwenye Ngoma za masikio
Kuishi na tatizo la kusikia ni ngumu mno kikwazo ni matibabu unajikiuta unapoteza hela na huponi.. kama umeambiwa kuna operation itakusaidia sawa tu mzee! Kwa sababu iko kuwa watu wamepata tatizo la kusikia ikakutwa masikio yamejaa uchafu yani yamezibwa. Yakizibuliwa tu unapona tofauti na hapo ni majaliwa.
 
Cha muhimu ni kujiamini tu kila mtu anamatatizo yake hakuna ambae hana kabisa.
Sio rahisi kihivyo mzee.. tatizo la kusikia lisikie tu kwa mwenzio linatesa sana! Imagine umekaa na wenzio wanaongea ghafla wanacheka wewe upo hujui wameongea nini.. ukienda kutafuta huduma sehemu mbalimbali mfano hospital au benki ni shida tupu. Ukienda kwenye nyumba ya ibada ni shida tupu huelewi kitu. Simu yako mwenyewe ukipigiwa hupokei.. mtu anakuuliza kuhusu "x" wewe unajibu "y". Hebu check hizo scenario utajiamini vipi hapo?
 
Kuishi na tatizo la kusikia ni ngumu mno kikwazo ni matibabu unajikiuta unapoteza hela na huponi.. kama umeambiwa kuna operation itakusaidia sawa tu mzee! Kwa sababu iko kuwa watu wamepata tatizo la kusikia ikakutwa masikio yamejaa uchafu yani yamezibwa. Yakizibuliwa tu unapona tofauti na hapo ni majaliwa.
Miaka flani nilikuwa mkapa walisema hawaniwezi, huwaga wananishangaa Sana kutokana na ukubwa wa tatizo still Nina usikivu kiasi, ila waliniambiaga ukweli kuziba Yale matundu sio guarantee ya usikivu kuongezaka na hii ni kutokana na ukubwa wa tatizo. Changamoto kubwa ni tinnitus

Ila maisha lazima yaende, kikubwa nishajishukuru na Nina jiweza
 
Daah! Poleni sana. Mi nina mdogo wangu wa mwisho naye ana hali hiyo, changamoto anayopitia inamfanya mkiwa mnaongea ya anatabasamu tu.

Pia kwenye kupata ajira imekuwa mtihani kwake mara nyingi anakosa sababu ya hiyo changamoto.

Ye ilimuanza akiwa Primary kwani alikuwa anaanguka sana na ilikuwa akianguka anapigiza kichwa saa ingine anajipigiza upande wa masikio mwishowe ndo akapata hiyo shida.
 
Daah! Poleni sana. Mi nina mdogo wangu wa mwisho naye ana hali hiyo, changamoto anayopitia inamfanya mkiwa mnaongea ya anatabasamu tu.

Pia kwenye kupata ajira imekuwa mtihani kwake. Yaani akiomba kazi ikifikia kwenye Oral Interview basi hapo ni lazima aanguke sababu ya hiyo changamoto.

Ye ilimuanza akiwa Primary kwani alikuwa anaanguka sana na ilikuwa akianguka anapigiza kichwa saa ingine anajipigiza upande wa masikio mwishowe ndo akapata hiyo shida.
Mungu amfanyie wepesi, sababu ya kuanguka ni nini?
 
Sio rahisi kihivyo mzee.. tatizo la kusikia lisikie tu kwa mwenzio linatesa sana! Imagine umekaa na wenzio wanaongea ghafla wanacheka wewe upo hujui wameongea nini.. ukienda kutafuta huduma sehemu mbalimbali mfano hospital au benki ni shida tupu. Ukienda kwenye nyumba ya ibada ni shida tupu huelewi kitu. Simu yako mwenyewe ukipigiwa hupokei.. mtu anakuuliza kuhusu "x" wewe unajibu "y". Hebu check hizo scenario utajiamini vipi hapo?
Ni mtihani Sana ndugu yangu.
Mimi kisa cha brother Mpauko kinaniuma Sana, mshikaji ameteseka mno
 
Hata haikujulikana hasa mana ilianza mfano wa kifafa ila baadae ikabadilika ikawa akianguka anazimia hatoki cha povu wala nini na hapo mnakaa wee mpaka hapo baadae ndo anazinduka.
Itakuwa ni kifafa, hata Mimi sjui ni nanna gani masikio yalianza kusumbua nikiwa mdogo, kama miaka 3, ila Ukubwani nilikuja kuambiwa Nilikuwaga na nakifafa nahisi shida ilianzia huko.

Baada ya hapo niligongwa na infection ya hatari, masikio yanavuja usaha karibu miaka 19.
My take, watu wenye shida kama hizi, kwa namna yoyote wasitumie pamba kusafisha masikio ni hatari mno, Bora uende hospital watumie sunction wavute huo uchafu, bila ya hivyo Mimi masikio yangeendelea kumwaga usaha mpaka Leo.
 
N
Daah! Poleni sana. Mi nina mdogo wangu wa mwisho naye ana hali hiyo, changamoto anayopitia inamfanya mkiwa mnaongea ya anatabasamu tu.

Pia kwenye kupata ajira imekuwa mtihani kwake mara nyingi anakosa sababu ya hiyo changamoto.

Ye ilimuanza akiwa Primary kwani alikuwa anaanguka sana na ilikuwa akianguka anapigiza kichwa saa ingine anajipigiza upande wa masikio mwishowe ndo akapata hiyo shida.
Naskiaga kuna nafasi za ajira Kwa watu wenye mahitaji maalumu, mana hata Mimi niliona ni kupoteza muda vyeti nimevitupia uvunguni
 
Mimi Ni Muhanga Tangu Darasa La 6 Nilipoumwa Maralia kali Na Kuchomwa Quineni Up-to-date Naishi Na Usikivu Hafifu 😢,
Changamoto ni Nyingii Sana ila Huwa Napotezea tuu....

Darasani Nilikuwa Vizuri Kwasababu Akili Ninazo ☺️,

Mtaani Nina Heshimika Coz Kwanza Wakiangalia Mimi Kiziwi nimefika Chuo wao wazima hata Form 4 tuu Wameshindwa Kuvuka 😂 ,,

Kwa Mademu Nina heshimika Coz Nina Mvuto na Muda Wote nipo Smart 😅 Mpaka Mkuu wa Chuo Alinisifia.

Kwasasa Nimejishikiza Kwenye Ngoma za Shughuli Alhamdullilah Hela ya kula Napata 🙏.
Though Nipo Naomba Mungu internship Niifanyie Dar es Salaam ili Niendelee Na Upigaji Ngoma ili Hata Nikimaliza intern December 2027 Niwe Nimepiga Hatua Kadhaa....!!!
 
Back
Top Bottom