Kwa waliomaliza form 4, kama una roho ndogo usiende kusoma special schools (shule za vipaji maalumu)

Kwa masomo ya arts ni kupoteza muda Ila sayansi hasa PCM siyo level ya kuiruka.
Muhimu sana mbele ya safari huko elimu ya juu. Pia katika maisha ya kawaida ya fundi sanifu au mhandisi.
 
Mimi nilifanya hivi hivi nikienda form 5 nikiwa nimemaliza topics zote niliporudi nusu mhula nilichelewa mwezi mzima nikamalizia za form 6 baada ya hapo nikawa nafundisha wenzangu advance topics za tuition wao wananifundisha/kuelekeza notes shallow za walimu wa shule,namshukuru mungu div 1 ilisimama advance, nilichojifunza advance ni muda mchache sn use it very wise otherwise kwenda na div 1 na kutoka na zero ni rahisi sn.
 
Ha ha ha... Au unamzungumzia teacher philipo wa chemistry pale ilboru?
 
Duuuu hii imenichekesha aisee, just imagine hujaunga ata waya ila umepata data
 
Uliyatimba[emoji23]

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Nilifika shule ya namna hii nimeripoti tuu nikakutana na haya mambo watu wametokea shule kali huko aisee mimi nimetokea shule ya kata duh hakuna walimu hata akija anafundisha kama watu waliokwisha kusoma tayari akiuliza swali watu wanajibu nabaki peke yangu ambae sijajibu. Watu form five anasolve chand, tom duncan.Basi bwana kuna jamaa mmoja alikua anasema physics rahisi sana kwake kwahiyo wale ambao hatujui lolote jamaa akaanza kutufundisha kuanzia topic za mwanzo kabisa. Cha kushangaza ukaja mtihani wa phyisics jamaa nikamkimbiza yeye na majamaa wengi tuu waliokua manakua na kujionesha aisee hahaha sitasahau mimi naenda kwa mwana tuendelee kupiga pindi jamaa akanichana "Sina muda nina mambo mengi" baadae shule ilivokuja kuchanganya hakuna cha aliesoma tuition au umetoka sijui st nani mziki ulikua mzito kwa wote zile mbwembwe huwaga za mwanzoni tuu.
 
Huku kama una roho ndogo sio pa kwenda mi nusura panishinde nilitaka nirudishe mpira kwa kipa(kuhamia private)
Mkuu hongera kwa kupitia shule hizo za vipaji. Maana inasemekana kule ndipo panatoka bongo za kuendesha nchi ( Sina hakika ukizingatia wenye vipaji wanawindwa na wenye wivu ovu). Panatamanisha asikwambie mtu! .
====
Sasa baada ya 4 na 6 linaanzia picha!!!!

Yaani Kasheshe inaanza pale Ukiingia Chuo Kikuu na mihemko ya wani ya Tatu na wani ya saba Hasa shahada za "sayansi asilia au sayansi gumu". Nyote mnakuwa sawa sawa... Divijheni zenu mnaziacha getini!!

Na huyo wa wani kama alikuwa ana meza Maswali na majibu huko A levo na O levo...anaweza kukimbizwa Chuo kwa muhula wa kwanza tu . Maana kule naambiwa ni mwendo wa kosepti na apulikeisheni mbinu katika kukabili changamoto halisi!!!

Kwa maneno mengine vijana mkipata furusa kwenda huko nendeni mkapambane. Maana Kipimo halisi ni huko kwenye Shahada!!!
 
Gifted minds!

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…