bily
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 8,029
- 5,796
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo.
Dar es Salaam hakuna mzee. uzee mwisho Chalinze. hata mvi moja sina dadangu.
Mbona dr Kamata hana shida alitufundisha mpole au ndo bwebwe zimempungua
Namkumbuka sana Dr
Osoro. Dr Amani. Dr Kasungu. Dr Mbago Dr Anna Tibaijuka. Dr.
Mtatifikolo. bw Karamagi wote sasa nasikia ni ma Professor. Yule wa
jikoni bw Chitanda na hall manager wa hall Three na hall one bw. Ali.
Dr. lipumba daa those were the days. ukitaka kuondoa uhanga una import
KCC kutoka Mwenhe au Ubungo unampa exile room mate wako. enzi zile ni
chumba watu wawili hata kiwe kile kikubwa cha hall five. walimu waliokua
na magari walikua wanahesabika kama Costa Mahalu. dr Lyakurwa. Dr.
masuha. Dr Suleiman Ngware wa Ds. wengine wengi ni uda na daladala....
Siku hizi eti na madenti wanaendesha.......
bila kumsahau Dr. Natu
mwamba sasa ni naibu gavana wa benki kuu , Suleiman ngware namkumbuka
mkuu halafu hivi kama sikosei mkewe au dada ake ni lecturer hapo
udsm.
Hapana, siyo Rich
Mwita. Ni Rich mwingine (bonge) anatokea mbeya na alikuwa ndani ya
Daruso kama waziri wa Shuttle
Kumbe anapenda down the corridor?
bila kumsahau Dr. Natu mwamba sasa ni naibu gavana wa benki kuu , Suleiman ngware namkumbuka mkuu halafu hivi kama sikosei mkewe au dada ake ni lecturer hapo udsm.
Umenikumbusha mbaali sana, enzi za kunji la kukomaa ifutwe 40% kisha kukomaa yasiwepo madaraja. Kipindi hicho Udsm ilikua Udsm kweli siyo hizi nyakati za leo. Odoooong...
Watoto mlosoma CHUO CHA KATA mna tabu sana!kelele nyiingi kichwani 0...karibuni HAVARD.
Watoto mlosoma CHUO CHA KATA mna tabu sana!kelele nyiingi kichwani 0...karibuni HAVARD.
Mkuu nadhani baada ya enzi ya Odong na mtatiro ndio kikaja kizazi cha kipara na Rich. hapo katikati enzi za kina mlowe, kiswaga hali haikuwa tete sana.
Nyoo eti Havard.... Si useme tu unasoma udom?
Hahaahaaaa mkuu umemaliza kabisa haahaaa,,,,John Komba alikua mature entrant..hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaEnzi zole Philip Mulugo ni katibu DARUSO. rais wake Lema Godbless na huyu Amos Makala alikua fresher. enzi zile Professor Maji Marefu ndio amehamishiwa UDSM akitokea SUA. akaja UDSM botany. John Komba aliingia kama mature entrant. alikua mwembamba huwezi kuamini na alikua mlokole.
Mimi namkumbuka kamanda wangu bahati tweve wakati wa mgomo wa kwanza wa bodi ya mkopo mwaka 2005. Rais wa daruso aliogopa kuongoza maandamano lakini tweve akatuhamasisha pale nkurumah tukaanza maandamano tukapigwa mabomu pale mlimani city wakati huo ilikuwa bado mlimani city. Tukarudo chuoni kujipanga tena kila mtu akibeba maji ya viroba tukarudi tena wakatupiga mabomu tena.
Uchaguzi wa daruso uliofuata nao ulikuwa kivutio maana kulikuwa na kambi 2, kambi ya kwanza ilikuwa na mtu anatoka law ambaye alipata support kutoka utawala na ccm akiwemo ridhiwani kikwete, wakati kambi ya pili aliyekuwa anagombea ni mwita mwikabe akipewa support na bahati tweve.
Kambi ya kwanza ilikuwa na hela kwa kampeni zao zilikuwa za kitajiri, wanafunzi wengi walipombeka bure. Wakati upande wa mwikabe support ilikuwa kubwa kwa wanafunzi wenyewe na watu walikuwa na mabadiko ya kweli. Baada ya muda uchaguzi ukafanyika nakumbuka usiku huo kulikuwa na tetesi kuwa kambi ya riz wanataka kuiba kura watu wakaenda kulinda usiku kucha. Mwisho wa siku MWITA MWIKABE akachukua uraisi wa daruso.
enzi za mtungirehi. foe walikuwa hawampendi. waliwahi kumshusha high table nkrumah kwa kichapo chuo kikafungwa.