Nyuma ya mzee mwenye kibaraghashia, mwenye shati jeupe, yuko katikati ya polisi wamekaa nae kulia na kushoto.
Sasa unajua kosa lake ? Alikwenda kukaa nyumba ya Kambona wakati Kambona kakimbia.
Kassim Hanga alipotumbuliwa alijiondokea bila bifu, akasimama Egypt akafikia kwa balozi, halafu akaenda Guinea, halafu akiwa njiani kurudi nyumbani akasimama Uingereza, nyumbani kwa Kambona. Kambona anasema akamwita Hanga chumbani kwake, akamwambia unarudi Tanzania, watakukula kichwa. Hanga hakuwa convinced. Kambona akawaita Wazanzibari wawili nyumbani kwake akawaambia hebu ongeeni na huyu mtu, anaenda kuwambwa msalabani huko kwa Nyerere. Hanga akawaambia, jamani mimi nimeondoka sina ugomvi na Nyerere. Haya. Alipofika airport Kiwalani Jet Lumo, akaja rafiki yake mwingine na mke wake, wakamwambia umerudi huku ? Nyerere anatafuta kichwa chako kwenye sinia.
Hanga akaenda kufikia nyumbani kwa Kambona, Msasani, two doors down the block kutoka kwa Nyerere. Kesho yake magazeti yakaandika Hanga kaingia nchini. Gestapo wa Nyerere wakaja kumkwida. Akaenda mahabusu, baada ya siku chache akaletwa Mnazi Mmoja kwenye mkutano wa Nyerere. Toka siku ile mpaka leo anaejua alipo Hanga ni Mungu, shetani na Nyerere.
Ingekuwa Nyerere alikuwa under pressure ya Karume, na kwamba Karume ndio mbaya, basi Nyerere asingemleta Waziri Hanga uwanjani Mnazi Mmoja yeye mwenyewe binafsi Nyerere kumtukana Hanga.
Huwezi kum sanitize Julius Nyerere. Nyerere hasafishiki, alikuwa na yeye ni primitive, ignorant third world despot, masikini ya Mungu.
Baada ya kuwa wakubwa na kupata elimu ya juu inayofundisha kujifunza kwa kutafiti, wengine tulishajiosha majini na maruhani ya ule utoporo wa mwalimu wa siasa wa primary school, ambae nae, tuseme ukweli, alikuwa hazimo, you and I know that.... masikini ya Mungu. Mwalimu wa primary aliyetufundisha hizi historia alikuwa hana uwezo wa kuchambua ule uharo wa propaganda za chama kimoja cha enzi zile, hajui chochote.