Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Nilikwenda kutafuta gari show room nikaona Nissan x-trail nikaona bei yake bahati nilikwenda na fundi mzoefu.Nikatoka hapo nikaenda show room ingine nikakuta RAV4 nikaona bei yake.Nikagundua tofauti ya Nissan x-trail na RAV4 ni million 5.Kwa maana hiyo Nissan x-trail bei yake ili upate RAV4 unaongeza mil5.

Nikashikwa na ubahili nikataka kwenda kule kwenye x-trail yule fundi akaniambia mzee kama hela ipo chukua hii haraka kwa umri wako hustahili kuwa na x-trail itakutesa.

Nikachukua ile RAV4. Niliporudi jioni nikakutana na rafiki yangu kwa umri Nampa shikamoo kanizidi miaka 7 akaniambia mdogo wangu ungechukua hiyo X-trail ningekupiga makofi leo.

Hadi leo sijajua alikuwa na maana gani ila niwaambie hadi leo sijajutia kuchukua ile RAV4. Jamaa yangu mmoja siku moja akaniambia Nissan x-trail ni nzuri ila zina matatizo mawili 1.Spares za Nissan ni ghali sana ila ukiweka unasahau 2.Nissan zina mifumo ya umeme wenye electronics sana hivyo itakupa shida sana iki fail kitu kidogo RAV4 kidogo imekaa ki manual manual wadau changieni.

Ila ushauri wangu ukienda chukua gari au kuagiza usifuate mkumbo kuwa niwe na la kama flani kikubwa tafuta fundi na mzoefu wa magari uende naye
Unajua mentality ya Kibongo kuhusu Toyota ni mbaya sana...yaani kuanzia mafundi mpaka wamiliki huwaambii kitu kuhusu toyota.....

Mfano mrahisi nchi nyingi za west Africa magari kama VW na mengine ya Ulaya yanatawala hizo toyota hazina nafasi..

Kuke unakuta VW zimejaa mpaka zinapiga kazi kama taxi....

Toyota kukubalika Tz haimaanishi kuwa ndiyo gari bora zaidi ya yote, kuna ukanda mwingine hazikubaliki unaweza kuta mazda ndiyo inakubalika
 
Iridium Spark Plug. [emoji5]
IMG_20201112_144822.jpg
 
Ninataka kulipia nissan xtrail hii milioni 167,00,000 ushauri wenu kabla ya yote
BH608980_73a73b%20(1).jpeg
Screenshot_20201128-122609_Chrome.jpeg
 
Nazipenda gari za Nissan kutokana na kazi zangu za SITE.

ukweli nissan wana gari nzuri sana yaani zinavumilia mikiki sana maporini.

first nilikuwa na X-trial but now NINA TERRANO II yani raha tu aiseee now nataka ya kukatia misere "Nissan Skyline" 2021 january naikamata.

but tatizo kwenye pedal ya mafuta na spare tu kama vijisenti vya mawazo basi tumia toyota tu.

spare nilishawahi hangaika mpk nilimaliza kariakoo nzima hahahah......
 
Nazipenda gari za Nissan kutokana na kazi zangu za SITE.

ukweli nissan wana gari nzuri sana yaani zinavumilia mikiki sana maporini.

first nilikuwa na X-trial but now NINA TERRANO II yani raha tu aiseee now nataka ya kukatia misere "Nissan Skyline" 2021 january naikamata.

but tatizo kwenye pedal ya mafuta na spare tu kama vijisenti vya mawazo basi tumia toyota tu.

spare nilishawahi hangaika mpk nilimaliza kariakoo nzima hahahah......
Wauzaji wengi wa spea ukiwaambia unataka spea ya Nissan fulni, wanakujibu tu kirahisi hakuna...ika ukienda na sample wanakutolea stoo.
 
Mimi nimekuwa nazo mbili, moja niliuza nikanunua nyingine. Kwa kifupi ninaiamini sana kwa safari zangu.

IPO stable sana pamoja na udogo wake na inachanganya haraka sana. Huwezi kuamini kuwa inazipita gari nyingi sana kwa suala la mwendo.

Katika safari ina uwezo wa kutumia lita 1 kwa km 30 hasa ukiwa spidi kati ya 50 - 100 hapo.
kwahivyo mkuu litre 30 unafika mbeya bila utata 🤣
 
Back
Top Bottom