Nilikwenda kutafuta gari show room nikaona Nissan x-trail nikaona bei yake bahati nilikwenda na fundi mzoefu.Nikatoka hapo nikaenda show room ingine nikakuta RAV4 nikaona bei yake.Nikagundua tofauti ya Nissan x-trail na RAV4 ni million 5.Kwa maana hiyo Nissan x-trail bei yake ili upate RAV4 unaongeza mil5.
Nikashikwa na ubahili nikataka kwenda kule kwenye x-trail yule fundi akaniambia mzee kama hela ipo chukua hii haraka kwa umri wako hustahili kuwa na x-trail itakutesa.
Nikachukua ile RAV4. Niliporudi jioni nikakutana na rafiki yangu kwa umri Nampa shikamoo kanizidi miaka 7 akaniambia mdogo wangu ungechukua hiyo X-trail ningekupiga makofi leo.
Hadi leo sijajua alikuwa na maana gani ila niwaambie hadi leo sijajutia kuchukua ile RAV4. Jamaa yangu mmoja siku moja akaniambia Nissan x-trail ni nzuri ila zina matatizo mawili 1.Spares za Nissan ni ghali sana ila ukiweka unasahau 2.Nissan zina mifumo ya umeme wenye electronics sana hivyo itakupa shida sana iki fail kitu kidogo RAV4 kidogo imekaa ki manual manual wadau changieni.
Ila ushauri wangu ukienda chukua gari au kuagiza usifuate mkumbo kuwa niwe na la kama flani kikubwa tafuta fundi na mzoefu wa magari uende naye