Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Cha kuzima hakisitiri makalio.

Ukiona mtu hana hata pikipiki avoid kushare nae gari unless unamuamini kuliko kiwango.

Mara nyingi watu wasio makini huwa wanashida sana......
 
Hili tatizo sijawahi kukutana nalo mkuu.
Labd kama spea ikizingua uendelee kutumia kibishi, hapo lazima uzalishe matatizo mengine, ila ukifunga kwa wakati ni mwendo mdundo, mwendo mchubuyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona ndicho kitu ameelezea hapo. Amesema kuwa ukiona kifaa kimeharibika usitembelee gari ikiwa inaumia na kifaa kibovu sababu itazalisha tatizo kubwa zaidi ya hilo.
 
Na kwann anaweka maji kwenye Radiator......?! Hajui coolant
 
Mkuu nina ka Nissan Cube, 2007 petrol, automatic. Gear hazi change, ni kama naenda na namba moja tu, reverse iko poa, toa msaada mkuu kama wajuwa tafadhali..
Cube kama sikosei intumia CVT...hebu angalia fluid isijekuta imepungua sana, au imechoka sana, au isijekuta fundi kakuwekea ATF za kawaida...

Kama ni cvt , lazima itakuwa inatumia NS 2, au NS 3
 
Mkuu nina ka Nissan Cube, 2007 petrol, automatic. Gear hazi change, ni kama naenda na namba moja tu, reverse iko poa, toa msaada mkuu kama wajuwa tafadhali..
Hiyo gari toleo hilo linatumia transmission ya mfumo wa CVT. Huu mfumo ni tofauti na ule uliozoeleka wa automatic transmission.

Katika mfumo huu tofauti yake na mfumo wa kawaida wa Automatic transmission hakuna gear yaani zile pungili au bangili zenye meno katika chuma moja zinazoitwa Counter Gear. Huu una miduara miwili tu na mechanism yake ya kubadilisha gear ni wa kujibalance kutoka na namna unakanyaga.

So hautasikia ile hali ya gari kubadili mlio au kushtuka ikibadili gear. Hii mfumo wake ni wa kutanuka na kusinyaa kwa muundo wa hizo sahani.

Hautaweza kuelewa vema hadi nikuonyeshe nama inafanya kazi boss.

Ila sidhani kama gari yako ni mbovu kutokana na maelezo yako nadhani unashangaa ukikanyaga unasikia gari inatoa mlio bila kubadilika sauti ya mlio wa gear wala haistuki kubadili gear...... Hiyo ndio namna mifumo ya CVT inafanya kazi. Ni kama gari haina gear kabisa..... Mlio wake ni midhiri ya cherehani..... Yaani ukikanyaga utasikia mlio huo huo mwanzo mwisho. Ntakutumia video utaona.....
 
Hii ndio gear box ya gari inayotumia mfumo wa CVT..... View attachment 1714352View attachment 1714351
Ukitazama hapo unaona vyuma viwili vinavyounganishwa na chain au mkanda wa chuma huo. Hizo sahani ukikanyaga mafuta, hapo katikati inapopita huo mkanda wa chuma panatanuka au kupungua kwa kupokezana wakati unakanyaga pedal ya speed au kuachia.

So sahani moja itatanuka wakati nyingine itasinyaa, then ukiachia pedal ile iliyotanuka itaanza sinyaa na ile nyingine itatanuka.........zinapokezana...... Hii inasaidia sana ulaji nafuu wa mafuta.
 
Mkuu nina ka Nissan Cube, 2007 petrol, automatic. Gear hazi change, ni kama naenda na namba moja tu, reverse iko poa, toa msaada mkuu kama wajuwa tafadhali..
Hii ni gearbox ya automatic ya kawaida..... Tazama yale machuma yenye zile bangili zenye meno, hizo ndio gear zinazobadilisha unapokuwa katika mwendo. Na hizo chuma ndio huitwa counter gear.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…