Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Nina Nissan Cube, 2007, nimeridhika nayo kuliko, kila kilichoandikwa kuhusu Nissan ni kweli, spears ghali kidogo, ila wasahau, iko stable, reliable, nimeka-jazz up basi kako poa sana, tairi pana basi kamenyanyuka hivi, nasikitika sijatumia Turbo/Sport kwa safari ndefu, ila nina mpango huo kwa kuenda samilia mama mikoani, gari zake ziko poa sana hizi Nissan, infact I am so hooked in such nimeanza kutafuta Nissan Cube ya 2011 au zaidi.

Tujipongeze kwa kweli. Bad note : Juzi pale Beachcomber Africana nilitolewa show na katoto fulani kavulana kako kama 8-9 yrs of age, kwa kuiita Nissan Cube ina sura mbaya?!😡😡😡 To make matters worst, nikashuhudia kale katoto kametoka na ndugu zake na wazazi wakapanda Bajaj?! Can you believe it?!

Ndorobo kabisa,,,
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Kuna Nissan Patrol moja Old Model nilipata kwa mzungu mmoja aliyekuwa anafanya research ya wanyama pori ..Yeye alilinunua DT Dobbie
Basi ikafika wakati anaondoka akaliuza kwa bei ya kishkaji sana ...sijawahi badilisha hata bolt zaidi ya kufanya service ya kawaida na kubadilisha Timing Belt

Juzi nasafiri nikamuachia jamaa yangu mmoja sasa sijui alipasulia wapi rejeta bila kujua akaendesha hivyo kilichotokea gari ilizima yenyewe kuja kufungua Bonnet ya gari engine imeoza yote kilicho baki salama ni cylinder head na block ..80% ya engine imekufa ..kuulizia sasa spare na kuifanyia overhaul niliishia kushika kichwa ,nilichofanya ni kutoa matairi nikalifunika mpaka majaliwa tena

Jamaa yangu mwenyewe maisha ya kuunga unga kama yangu ,mke wake mwenyewe sio mzuri maana ningemmegea kupunguza hasira basi ndio hivyo tena

Nissan ni gari nzuri sana ila isije ikaua kitu kikubwa lazima ulie.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Cha kuzima hakisitiri makalio.

Ukiona mtu hana hata pikipiki avoid kushare nae gari unless unamuamini kuliko kiwango.

Mara nyingi watu wasio makini huwa wanashida sana......
 
Hili tatizo sijawahi kukutana nalo mkuu.
Labd kama spea ikizingua uendelee kutumia kibishi, hapo lazima uzalishe matatizo mengine, ila ukifunga kwa wakati ni mwendo mdundo, mwendo mchubuyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona ndicho kitu ameelezea hapo. Amesema kuwa ukiona kifaa kimeharibika usitembelee gari ikiwa inaumia na kifaa kibovu sababu itazalisha tatizo kubwa zaidi ya hilo.
 
Kesi kama hii imemkuta rafiki yangu...yeye ana Nissan xtrail....mambo ya ushkaji yakamponza.
Kuna mshkaji wake akaja akamuazima gari jamaa akaenda Sehemu inaitwa mbuguni karibia na ukuta wa Magufuli...kumbe njiani kuna tatizo lilitokea rejeta ikawa inavijisha jamaa yeye akakanyaga mafuta tu...si unajua tena gari la kupewa, unalifanyia sifa.
Injini ikapata moto sana jamaa haelewi yeye na gia tu, kwa bahati akafika safari yake..anafika anataka kupaki gari likazima lenyewe...malaika alimuongoza hakuliwasha...akafanya yaliyompeleka kwa muda mrefu huku gari linapoa ila boya haelewi chochote.
Alipomaliza mishe zake akaja kwenye gari, kupiga jino moja gari likawaka..kama kawaida mzee na gia anafika tu home kwa mwenye gari, gari likazima...sasa hapa wote wawili walikutana vichwa maji...hawakujishughulisha kutafuta tatizo ni kwa nini gari limezimika..Ikawa usiku, ikawa asubuhi...mwenye gari akawasha ,likawaka akenda mtaa wa jirani kama Km 2 hivi akaeguza kurudi home wakati anaiacha barabara ya vumbi aingie kwenye lami gari ikazima na kulikwa na kamteremko pale so usukani ukafeli na brake zikawa ngumu gari likamshinda jamaa coz naye ni lena lena...likaserereka kwenye lami likagonga gari lingine ubavuni....wakaongea sijui walielewanaje...ila wakayamaliza..
Akaita break down kufikishwa garage mafundi kufungua bonnet engine imekaangika to the maximum...rejeta haina maji hata tone....wakamsimulia fundi tangu mwanzo kule mbuguni gari ilivyozima...akawaambia wangeongeza maji wangenusuru Injini..
Kulikuwa hakuna namna hata ya kureface cylinder head....
Jamaa akanunua injini nyingine maisha yakaendelea..from that day, anakagua maji kuliko kitu kingine kwenye lile gari.
Haya ni madhara ya kupeana gari na washkaji wazembe na mwenye mali kuwa mzembe kutokukagua gari mara kwa mara

Mimi huwa nina desturi...rafiki yangu ni rafiki yangu mimi...ila si rafiki wa mali yangu hata kama nimeinunua 750/=

Bongo tunarudishana sana nyuma kisa ushkaji usio na mashiko

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kwann anaweka maji kwenye Radiator......?! Hajui coolant
 
Mkuu nina ka Nissan Cube, 2007 petrol, automatic. Gear hazi change, ni kama naenda na namba moja tu, reverse iko poa, toa msaada mkuu kama wajuwa tafadhali..
Cube kama sikosei intumia CVT...hebu angalia fluid isijekuta imepungua sana, au imechoka sana, au isijekuta fundi kakuwekea ATF za kawaida...

Kama ni cvt , lazima itakuwa inatumia NS 2, au NS 3
 
Mkuu nina ka Nissan Cube, 2007 petrol, automatic. Gear hazi change, ni kama naenda na namba moja tu, reverse iko poa, toa msaada mkuu kama wajuwa tafadhali..
Hiyo gari toleo hilo linatumia transmission ya mfumo wa CVT. Huu mfumo ni tofauti na ule uliozoeleka wa automatic transmission.

Katika mfumo huu tofauti yake na mfumo wa kawaida wa Automatic transmission hakuna gear yaani zile pungili au bangili zenye meno katika chuma moja zinazoitwa Counter Gear. Huu una miduara miwili tu na mechanism yake ya kubadilisha gear ni wa kujibalance kutoka na namna unakanyaga.

So hautasikia ile hali ya gari kubadili mlio au kushtuka ikibadili gear. Hii mfumo wake ni wa kutanuka na kusinyaa kwa muundo wa hizo sahani.

Hautaweza kuelewa vema hadi nikuonyeshe nama inafanya kazi boss.

Ila sidhani kama gari yako ni mbovu kutokana na maelezo yako nadhani unashangaa ukikanyaga unasikia gari inatoa mlio bila kubadilika sauti ya mlio wa gear wala haistuki kubadili gear...... Hiyo ndio namna mifumo ya CVT inafanya kazi. Ni kama gari haina gear kabisa..... Mlio wake ni midhiri ya cherehani..... Yaani ukikanyaga utasikia mlio huo huo mwanzo mwisho. Ntakutumia video utaona.....
 
Mkuu nina ka Nissan Cube, 2007 petrol, automatic. Gear hazi change, ni kama naenda na namba moja tu, reverse iko poa, toa msaada mkuu kama wajuwa tafadhali..
Hii ndio gear box ya gari inayotumia mfumo wa CVT.....
images.jpg
View attachment 1714351
 
Hii ndio gear box ya gari inayotumia mfumo wa CVT..... View attachment 1714352View attachment 1714351
Ukitazama hapo unaona vyuma viwili vinavyounganishwa na chain au mkanda wa chuma huo. Hizo sahani ukikanyaga mafuta, hapo katikati inapopita huo mkanda wa chuma panatanuka au kupungua kwa kupokezana wakati unakanyaga pedal ya speed au kuachia.

So sahani moja itatanuka wakati nyingine itasinyaa, then ukiachia pedal ile iliyotanuka itaanza sinyaa na ile nyingine itatanuka.........zinapokezana...... Hii inasaidia sana ulaji nafuu wa mafuta.
 
Mkuu nina ka Nissan Cube, 2007 petrol, automatic. Gear hazi change, ni kama naenda na namba moja tu, reverse iko poa, toa msaada mkuu kama wajuwa tafadhali..
Hii ni gearbox ya automatic ya kawaida..... Tazama yale machuma yenye zile bangili zenye meno, hizo ndio gear zinazobadilisha unapokuwa katika mwendo. Na hizo chuma ndio huitwa counter gear.
images%20(12).jpg
 
Back
Top Bottom