Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa



No wonder Nissan Civilian City Buses zimekuwa nyingi kuliko Toyota Coaster sahivi. Hongera wapenzi wa Nissan!
 
Hahahahaa ah funika sura Wewe mega tu
 
Kama una hela za mawazo usijiingize huku
Utapaki gari nyumbani
Hasa upande wa maintenance

Japo mi sitoki nishafikaa...sanasana ntahamia BMW,Audi au Benz
Toyota am soleee kwa kweli..
Ttz la Toyota nyingi(ofcz naexclude vitu km Majesta,Camry,MarkX hivii na SUV nzuri nzuri zile) taste ziko basic tu wkt hizi brand zina touches of luxury kwny design na interior
 
We mjanja kumbe
 
Mkuu nina nissan patrol y61 gari safi na zuri saana nimepiga mnoo safar za dar tabora, dar urambo, dar mwanza, huu mwaka wa 5 gari haisumbui japo sasa hiv vyuma vimenikaza siitembelei najichanga nipate fuba la maana nizungumze na jamaa wanajiita capitalzone4*4 nimeona kazi zao instagram wanafufua mpaka magari yaliyokufa na kupimp mazima lakin naona wamebobea kwenye landrover zaidi.

Hii gari ni safi saana mkuu, siwez kufananisha na gari nyingime sababu hii ni gari yangu ya kwanza, ndio nimeanza kujifunzia humo humo na kuwa konki liquid humo humo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Arusha kwa ujumla ni wataalam wa kupimp magari japo wale jamaa ni wataalam zaidi kwenye mandolin ila hata Nissan wanazipiga fresh tu. Mi walinichongea front and rear bumper gari imekuwa mpya kabisa.
 
Duh!! Huyu jamaa ni gegedu kweli mpaka kuua engine ya nissan si mchezo kidogo, kesi kama yako ilinitokea morogoro natokea tabora kumbe rejeta ilikuwa na tobo inavujisha taratibu, naanza kuiacha morogoro mjini nipo kwenye mashamba ya mkonge, napanda tuta gari ikazima yenyewe nikashuka kufungua bonet ni mvuke tu!! Wakatokea washikaj na canter wakanitisha humo ndio basi tena, dah!! Presha ikapanda nikikumbuka nyumban kuna canter dereva kakaanga engine ipo juu ya gogo na hii nayo tena engine nimekaanga mwenyewe na vyangu sina nikawa napiga mahesabu ya kuuza screpa tu, kwakuwa tulikuwa mbali na maeneo ya watu tukasukua kurudi nyuma tukafika sheli kuna mlinzi tukamuelezea akasema anamfahamu fundi akampigia simu fundi akaja mie nikawa nachungulia game nakumbuka walikuwa atletico madrid vs celta vigo, fundi kuja akaicheki kidogo akatupa matumain akasema km ilijizima yenyewe kisa maji basi engine nzima, labda ingekuwa oili akasema nissan engine si nyepesi kufa kwa maji huwa zinawahi kujizima, ila itakapozima usiifosi, akatuagiza maji tukaenda kuchota msikit fulani upo karibu, tukaacha ipoe kabisa, kuweka maji akasema tuwashe, kuwasha jino moja tuu!! Mnyama kaunguruma nikapata matumaini kucheki ndio akasema rejeta inavujisha ila taratibu saana na kadri muda unavyokwenda tatzo linaongezeka, so tutembee na madumu ya maji, akasema ikizima njiani tumshitue, basi na kweli mpka tunafika uraian ilikuwa kazi ni moja tu kuongeza maji kila mara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…