Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Tatizo spare moja ikiharibika mfuatano wa kuharibika vitu vingine nao unafuatano, unaweza kupata kichaa!

Yeah spare zake ukifunga huwazi tena!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili tatizo sijawahi kukutana nalo mkuu.
Labd kama spea ikizingua uendelee kutumia kibishi, hapo lazima uzalishe matatizo mengine, ila ukifunga kwa wakati ni mwendo mdundo, mwendo mchubuyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio ghali tu ata upatikanajinwake sometimes ni kipengelee..nakumbuka kuna mzee mmoja alikuwa anatafuta CV joint ya Nissan libert mbona alijutaa alizunguka maduka ya spare yote jijin dsm haikupatikana iyo Cv joint ikabidi aagize dubenga
Alikosa hata zile spea za kufananisha??
Cv joint ikishakubaliana meno ya nje na ndani na ukubwa kipenyo ukafanana unafunga bila tatizo....nimeshafanya hivi kwenye nissan..
Huyo hakujiongeza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesi kama hii imemkuta rafiki yangu...yeye ana Nissan xtrail....mambo ya ushkaji yakamponza.
Kuna mshkaji wake akaja akamuazima gari jamaa akaenda Sehemu inaitwa mbuguni karibia na ukuta wa Magufuli...kumbe njiani kuna tatizo lilitokea rejeta ikawa inavijisha jamaa yeye akakanyaga mafuta tu...si unajua tena gari la kupewa, unalifanyia sifa.
Injini ikapata moto sana jamaa haelewi yeye na gia tu, kwa bahati akafika safari yake..anafika anataka kupaki gari likazima lenyewe...malaika alimuongoza hakuliwasha...akafanya yaliyompeleka kwa muda mrefu huku gari linapoa ila boya haelewi chochote.
Alipomaliza mishe zake akaja kwenye gari, kupiga jino moja gari likawaka..kama kawaida mzee na gia anafika tu home kwa mwenye gari, gari likazima...sasa hapa wote wawili walikutana vichwa maji...hawakujishughulisha kutafuta tatizo ni kwa nini gari limezimika..Ikawa usiku, ikawa asubuhi...mwenye gari akawasha ,likawaka akenda mtaa wa jirani kama Km 2 hivi akaeguza kurudi home wakati anaiacha barabara ya vumbi aingie kwenye lami gari ikazima na kulikwa na kamteremko pale so usukani ukafeli na brake zikawa ngumu gari likamshinda jamaa coz naye ni lena lena...likaserereka kwenye lami likagonga gari lingine ubavuni....wakaongea sijui walielewanaje...ila wakayamaliza..
Akaita break down kufikishwa garage mafundi kufungua bonnet engine imekaangika to the maximum...rejeta haina maji hata tone....wakamsimulia fundi tangu mwanzo kule mbuguni gari ilivyozima...akawaambia wangeongeza maji wangenusuru Injini..
Kulikuwa hakuna namna hata ya kureface cylinder head....
Jamaa akanunua injini nyingine maisha yakaendelea..from that day, anakagua maji kuliko kitu kingine kwenye lile gari.
Haya ni madhara ya kupeana gari na washkaji wazembe na mwenye mali kuwa mzembe kutokukagua gari mara kwa mara

Mimi huwa nina desturi...rafiki yangu ni rafiki yangu mimi...ila si rafiki wa mali yangu hata kama nimeinunua 750/=

Bongo tunarudishana sana nyuma kisa ushkaji usio na mashiko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina swali kuhusiana na hii gari.

Kwa nini sokoni, kwa iliyotumika hapa nchini, Bei yake huwa chini sana??

Je huwa zinatatizo gani common hizi gari??
Tanzania tunakariri magari. Yan tuna kama ile taste ya magari flani. Tazama bei za magari yakiwa bado JAPAn. Unakuta lava 4 mpaka dola 800 ila kufika juku unaikuta unauziwa million 15.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namiliki Nissan Dualis, changamoto niliyopata na baadhi ya wamiliki ni Navigation System (Nissan Carwings) kuwa kwa Kijapan. Mpaka sasa hatujapata mtu ambaye anaweza kubadilisha language from Japenese to English. Otherwise gari iko vizuri sana
Badilisha Radio funga yenye android 7.1.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingi engine kuharibika inasababishwa na nini?

Je kupiga pasi engine ni sahihi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaahaaa[emoji1787][emoji1787]...hapa mbavu sina hivoo!

Na Mimi nilikuwaga zwazwa hivo kipindi mgeni na gari[emoji16][emoji1787]...naaambiwa kila siku kagua gari kabla hujaondoka mi aaah wapi! Kwanza kufungua boneti ya gari mvivu kinomazz!...

Siku moja rejeta ikapasuka full kuvuja mi mziki mkubwa mwendo mrefu sina habaree...gari likanizimikia bagamoyo road! Tena main road...asee siku hiyo niliangua kilio watu wananishangaa! Niliogopa nilidhani nimeharibu gari[emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sitakaa nisahau!

In a nutshell toka nipate sekeseke hilo miaka minne imepita jamani mi nakagua gari kabla ya kuondoka utafikiri fundi, maana nilishafikia kipindi cha kuwa nabeba watoto wa paka kwenye boneti, kumbe walikuwa wanaishi mle[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Inashauriwa kukagua under the hood angalau kila baada ya siku mbili....si maji tu...unaweza kuta panya wameingia wakala nyaya gari lipige shoti liwake..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aaaaaa wewe kiboko, hadi watoto wa paka unabeba !
 
No wonder Nissan Civilian City Buses zimekuwa nyingi kuliko Toyota Coaster sahivi. Hongera wapenzi wa Nissan!

Yaani nilikuwa nawashangaa sana wanaoshobokea Toyota coaster. Unakuta na madereva plus matajiri wao wanadanganyana eti civilian mbovu, haziwezi daladala.... ona sasa zimejaa tele na spea nyomi! Sijui ni tune ya mzee baba ndo imewafanya wahamia civilian...
 

Toyota tupa kule.....afu zimekuwa nyingi kama uniform aaaaahaaa
 
Aseee!...sipati picha gari kuwaka moto[emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…