Kwa wanandoa: nani ana jukumu la kufua nguo zenu za ndani?

Kwa wanandoa: nani ana jukumu la kufua nguo zenu za ndani?

Kwenye ndoa.. Hasa kwa wanaojua maana ya ndoa mambo mengi hayana formula.. Ama formula Ku u ni upendo
Ni vuzuri kufua mwenyewe si za ndani tu hata zinginezo. Haujui ni lini mwenza wako utatengwa naye. Basi ujitayarishe kufua nguo zsko mwenyewe mara kwa mara. Hutajutia hili sawa na kuwa unapika chakula hasa wanaume, jifunzd kupika km chai, ugali, wali na kutengeneza kachumbari mwenyewe.
 
Huko kwenu mnafanyaje? na kwanini?

(A) Kila mmoja anafua underwear yake
(B) Hakuna formula maalum
(C) Mume anafua ya kwake na ya mke
(D) Mke anafua ya kwake na ya mume
(E) Dada/kaka wa kazi
Hapo E pekee ndo halipo kwenye ndoa
 
Nimetebasamuu halafu nikataka kucheka ila kicheko kikapotea....

Haya mambo banaa, na usishangae kuna walioachana kisa kufua nguo za ndani....

Mke anasema mimi sifui boksa zako unavaa wiki nzima unarudia...
Mume anakasirika kwanini hunijali na mimi nispoona boksa safi navaa ya jana...!!!🤔🤔🤔 (ana mkomoa nani...! Mbupuuu au mkee..!!?). Ukurutu unaanzia hapa..

Kuoa au kuolewa ni zaidi ya kufanya harusi, shurti kwanza uwe umepevuka kiakili/maarifa na uwe na busara za kutosha.

Ukiwa na mihemko, hasira za mkizi na maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu, umekwisha.....!!

Jiulize tuu, kutoa/kutolewa mahari ndo sababu ya kubadili mfumo wako wa maisha?

Kama wakati uko mseja ulikuwa unajimudu, kwanini baada ya kuoa/kuolewa uwe mlemavu mwenye viungo vyote? Hii ni hata kina dada, kama ulikuwa unajigharamia kwanini baada ya kuolewa ugharamikiwe...!!

Fanya huduma unayopewa na mwenza kama zawadi/nyongeza isipokuwepo isokuletee masononeko, maumivu au kuona hutendewi haki au kudhulumiwa.

Sikuzote penda maisha ya kujitegemea na si kutegemea flani kwa namna yeyote ile. Atayekupenda kwa dhati atakufata hapo ulipo ukiwa unajimudu na yeye asikufanyie jambo ili umuelekee, afanye bila kutarajia malipo.

Suluhiso la kuondoa hiyo kero tajwa, wekeni bajeti ya luku ya kutosha kwa mwezi, bajeti ya bili ya maji, nunueni mashine ya kufulia, chupi/boksa za kuvaa mwezi mzima bila kurudia.

Siku ya kufua iwe mara moja au 2 kwa wiki mnatumbukiza visinda vyenu humo, vesti, soksi, hendikachifu, brazia, gagulo, skin tite kisha mnaanika kama hamna mashine ya dryer.

Mkishindwa hapo tembeeni wizout. Yaani wewe usivae boksa, nayeye asivae kufuli wala brazia, nawewe usivae vesti wala soksi kukwepa nani afue na pia mtapunguza gharama ya kuzinunua.

NB: Dada wa kazi asifue nguo yeyote ya ndani. Mpeni suruali mashati magauni sketi blauzi basi. Hata hendikachifu asifue.

HYGENE: Usirudie kuvaa nguo ya ndani, vaa nguo ya ndani.mara moja kisha ifue.

Mwenye sikio asikie.

Bibi Kasinde.
Shikamoo bibi. Bibi mimi ili kufanya mambo yasiwe mengi, endapo nikiwa sijachoka sana, ninapokwenda kuoga nahakikisha nafua na boksa niliyovaa siku hiyo.
 
Nimeipenda hii wewe ni baba kwakweli, yaani kuna wanaume wengine hata mke aumwe vipi nguo atakuja kufua akipona hiyo ni haki kweli?
Maisha ni kusaidiana kuanzia nje mpaka ndani .. Kuanzia mchana mpaka usiku chumbani kitandani
 
Maisha no kusaidiana kuanzia nje mpaka ndani .. Kuanzia mchana mpaka usiku chumbani kitandani
Na walalamishi wakutaka kufanyiwa kila kitu kitandani huwa ni shida hapo huwa wanajihami wasionekane wanadharailiwa, mtu hata kama mke kapitiwa kuweka kijiko hawezi chukua duu 😳 jamani, kuna ndoa nyingine ni mitihani juu ya mtihani
 
Yani wewe una undugu na mume wangu, hafui hata iweje....wakati kabla ya kunioa alikuwa ananifulia vibikini anaanika kwenye kamba, afu nyumba ya kupanga hadi nilikuwa namkataza namwambia aache majirani wasije sema nimemroga🤣
Toka amenioa hagusi hata nguo zake, na mimi siwezi kumpa dada wa kazi nguo zake afue.....ndo nafua mwenyewe.
😂😂😂😂😂😂😂😂 Huyo anajitambua, mitano tena kwake
 
Inategemea umeoa Mke wa aina gani.

Ila kiuhalisia ni kazi ya Mke.
Lakini siyo kufua na kusafisha mwiko pia baada ya kusonga ugali (tafsida)
Kweli shez type kabisa yule mke eti anasema pep anawaza mpira tuu...wakati mpira huo ndio ulimfanya aishi vizuri apande private jets na kuenjoy life
Bwana Bwana!!!!
 
Huko kwenu mnafanyaje? na kwanini?

(A) Kila mmoja anafua underwear yake
(B) Hakuna formula maalum
(C) Mume anafua ya kwake na ya mke
(D) Mke anafua ya kwake na ya mume
(E) Dada/kaka wa kazi
Mwanangu ndoa ina siri zake. Nani anafanya nini naona kama haituhusu wala si jambo la kujihangaisha kuweka viwango au fomula.
 
Ikiwa mnadiscuss vitu kama kufua,basi mtadiscuss kupika,kuosha viombo,kuondoa viombo baada ya kula,kufagia nk yaani hiyo nyumba vikao vitakuwa vyingi.
 
Ukienda kuoa Pwani vitu sijui kufua,kupiga,kazi zote za nyumbani wanajua ni wajibu wa nani hamna mashindano na wanajua kupika kweli kweli.

Ila kuna baadhi ya nyumba beki tatu haishii kwenye kufua tuu,bali hadi kumpangia nguo za kuvaa kwamba hii inaenda na hii, ile na hii mke hana time.
😳😳
 
Back
Top Bottom