Umepewa uhuru wa kufanya unachotaka katika ukomo wa ubinadamu wako
Sijapewa uhuru huo, hii ni kauli ya kiimani.
Kila kitu kilichopo ndani ya uwezo wa kibinadamu umepewa uhuru wa kufanya kiwe kizuru au kibaya
Nimepewa na nani? Mungu? Huyu huyu Mungu ambaye hujaweza kuthibitisha yupo?
Hayo unayo Sema wewe sijui urudi nyuma miaka ya 1980 hayo yapo nje ya uwezo wa ubinadamu wako
Nnai kaamua yapo nje ya uwezo wangu? N akama kuna mwingine anaamua mwanzo na mwisho w auhuru wangu, je, ni kweli nina uhuru?
Huo ulimwengu wenye mazuri tupu Kwa Sasa upo ila sio Kwa binadamu ni Kwa malaika ulimwengu wa malaika una mazuri matupu labda kama na wewe unataka uwe malaika
Huu ulimwengu wa malaika huwezi kuthibitisha upo. Ukibisha, thibitisha upo.
Wewe binadamu hapa sio mwisho hapa unapita tu na hapa upo katika mtihani ukifaulu utaenda katika ulimwengu wenye mazuri tupu na ukifeli Jahanamu inakusuburi
Hata kama haya yangekuwa kweli, kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote atupitishe kwenye mapito yenye mabaya wakati aliweza kutupitisha kwenye mapito yasiyoweza kuwa na mabaya?
Kituo chako Cha kwanza
Ulianza maisha katika tumbo la mama yako yalikuwa maisha ya Raha sana Hadi siku uliyotolewa katika hayo maisha ukawa unalia maana mwili wako ulitambua kabisa kuwa Sasa unaingia katika tabu
Bado hujajibu kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote karuhusu viumbe wake anaowapenda waishi kwenye dunia yenye tabu na mabaya mengi?
Kituo chako Cha pili
Ni hapa Duniani hapa Duniani ndio umepewa uhuru wa kufanya unachotaka na kuchagua unataka kuishi maisha gani Baada ya maisha haya ya Duniani
Si kweli, sijapewa uhuru wa kufanya ninachotaka. Nataka an endless source of energy, sina uhuru wa kuwa nayo.
Kituo chako Cha tatu
Ni kaburini utaka ukisubiri siku ya hukumu ifike
Hujathibitisha kwamba baada ya kufa kuna siku ya hukumu, hii ni kauli ya imani tu.
Kituo chako Cha nne
Ni peponi au motoni
Na huko ni maisha ya milele hakutokuwa na kufa tena iwe upo peponi au motoni utaishi milele
Hujaweza kuthibitisha kuwa huko peponi au motoni kupo, hizo ni kauli za imani tu.
Usiweke kauli za imani tu, thibitisha unachoandika.