Mkuu Kuna k2 hujakielewa navotumia neno "perfection" hata ww unahitaji viatu na nguo n.k perfection ni kwamba Kuna kiumbe mwenye akili nyuma ya hiyo nyumba , ndio mana Ina sifa hizo , ingekua nature ambayo chaotic isingekua na sifa
Neno sahihi zaidi lingekuwa kwamba nyumba ina order, ina complexity, ina complex order.
Si perfection.
Nyumba haina perfection kwa sababu nilizozitoa hapo juu.
Tukija huko kwenye complex order, hoja yako kiukweli, kiundani kabisa, ni hoja ya kupinga uwepo wa Mungu.
Ila wewe hujajua tu.
Ulichosema hapo ni kwamba Mungu muumba vyote hawezi kuwapo. Ila hujajua tu, kwa sababu hujaichambua hoja yako kwa kina.
Twende polepole.
Kimsingi, nimekuelewa kuwa unajenga hoja kwamba, ukiona kitu kimepangika vizuri, kina order, kina complexity, kina complex order, basi lazima kuna aliyekiumba na kukiweka hivyo.
Unajenga hoja kwamba hii complex order huwa haitokei tu yenyewe, ni lazima iwe imewekwa na complex order kubwa zaidi yake, iwe imeumbwa. Wewe unahitimisha kuwa huyo aliyeiumba order ya ulimwengu ni Mungu (this is logical non sequitur fallacy, but let us entertain it to follow the logic)
Kwa hoja yako hiyo, nikikukubalia (kwa kutaka kuichunguza hoja zaidi), tutafika kwenye swali.
Kama ulimwengu ni complex order, na complex order haitokei tu, ni kazima iwe na muumbaji mwenye complex order zaidi, na muumbaji huyo ni Mungu, basi na Mungu naye ana complex order, na yeye pia atahitaji kuwa kaumbwa, hawezi kuwa yupo tu (kwa mujibu wa hoja yako mwenyewe kwamba complex order haiwezi kutokea tu, ni lazima iwe imeumbwa).
Kwa hoja hii, Mungu naye ni lazima atakuwa kaumbwa, hawezi kuwepo tu.
Na Mungu wako akishakuwa kaumbwa tu, anapoteza uungu wake wa kuumba kila kitu, maana kaumbwa.
Hivyo, hoja yako inaonesha huyo si Mungu. Na pia inaonesha Mungu hawezekani kuwapo.
Sijui kama umeelewa hoja.
Kifupi, ukisema nyumba haiwezi kuwepo tu ni lazima iwe na mjenzi unasema hata Mungu hawezi kuwapo tu, ni lazima awe na muumba wake, na akishakuwa na muumba wake basi ndiyo anakuwa si Mungu.
Umeelewa?