Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Sasa mkuu kama chochote kinawezekana basi inawezekana Ulimwengu ni eternal au sio eternal, AU Mungu ambaye ni eternal pia yupo au hayupo.
Kwa nini usifungie breki na kusimamia hapo badala ya kesema una uhakika hayupo huyo mungu??
Chochote kinawezekana kidhahania, lakini, dhahania nyingine zipo mbali sana na uhalisia uliothibitishwa kiasi kwamba kuzikubali kunahitaji uthibitisho.

Pia, nyingine zinakinzana na haziwezi kuwa kweli kwa pamoja.

Ukweli kwamba chochote kinawezekana kuwa kweli haumaanishi kuwa chochote ni kweli.

Inawezekana Mtanzania yeyote aliyefikisha miaka 40 akawa ni rais wa Tanzania.

Lakini, ukweli huu haumaanishi kuwa Mtanzania yeyote aliyefikisha miaka 40 ni rais wa Tanzania.

Rais wa Tanzania yuko mmoja tu.

Mtanzania aliyefikisha miaka 40 akisema yeye ni rais wa Tanzania, itabidi tuhakiki habari zake zaidi kujua kama kweli yeye ni rais wa Tanzania au siye.
 
Nyumba yako si perfection.

Itahitaji maintenance, votu vitaharibika itabidi ubadilishe.

Ikipigwa tetemeko kubwa itaanguka.

Mpaka hapo ushakosea kusema nyumba yako ni perfection.
Mkuu Kuna k2 hujakielewa navotumia neno "perfection" hata ww unahitaji viatu na nguo n.k perfection ni kwamba Kuna kiumbe mwenye akili nyuma ya hiyo nyumba , ndio mana Ina sifa hizo , ingekua nature ambayo chaotic isingekua na sifa
 
Maneno mengi lakini hujathibitisha Mungu yupo.
Papa Francis yeye anatetea dini ndio mana alishindwa kujib , mm nlishakuambia Muumba yupo ila sio kama dini znavomuongelea , kwasabb dini zenyewe misingi yake ni siasa za uongo na maandishi ya kuungaunga. Lkn Muumba yupo na anaendelea na kazi ambazo Zina umuhimu kwake sio kukufuatilia ww an insignificant being in the vastness of this universe.
 
Mkuu Kuna k2 hujakielewa navotumia neno "perfection" hata ww unahitaji viatu na nguo n.k perfection ni kwamba Kuna kiumbe mwenye akili nyuma ya hiyo nyumba , ndio mana Ina sifa hizo , ingekua nature ambayo chaotic isingekua na sifa
Mungu gani mwenye "Perfection" anaumba watoto wenye kasoro za kimwili kama vichwa vikubwa, njiti, wenye shida za akili, usonji?

Ninyi si ndio mna amini Mungu anaumba binadamu?

Sasa kama huyo Mungu ni "perfect" iweje watoto anao waumba wanazaliwa wakiwa imperfect?
FB_IMG_1732732380005.jpg
 
Mkuu Kuna k2 hujakielewa navotumia neno "perfection" hata ww unahitaji viatu na nguo n.k perfection ni kwamba Kuna kiumbe mwenye akili nyuma ya hiyo nyumba , ndio mana Ina sifa hizo , ingekua nature ambayo chaotic isingekua na sifa
Neno sahihi zaidi lingekuwa kwamba nyumba ina order, ina complexity, ina complex order.

Si perfection.

Nyumba haina perfection kwa sababu nilizozitoa hapo juu.

Tukija huko kwenye complex order, hoja yako kiukweli, kiundani kabisa, ni hoja ya kupinga uwepo wa Mungu.

Ila wewe hujajua tu.

Ulichosema hapo ni kwamba Mungu muumba vyote hawezi kuwapo. Ila hujajua tu, kwa sababu hujaichambua hoja yako kwa kina.

Twende polepole.

Kimsingi, nimekuelewa kuwa unajenga hoja kwamba, ukiona kitu kimepangika vizuri, kina order, kina complexity, kina complex order, basi lazima kuna aliyekiumba na kukiweka hivyo.

Unajenga hoja kwamba hii complex order huwa haitokei tu yenyewe, ni lazima iwe imewekwa na complex order kubwa zaidi yake, iwe imeumbwa. Wewe unahitimisha kuwa huyo aliyeiumba order ya ulimwengu ni Mungu (this is logical non sequitur fallacy, but let us entertain it to follow the logic)

Kwa hoja yako hiyo, nikikukubalia (kwa kutaka kuichunguza hoja zaidi), tutafika kwenye swali.

Kama ulimwengu ni complex order, na complex order haitokei tu, ni kazima iwe na muumbaji mwenye complex order zaidi, na muumbaji huyo ni Mungu, basi na Mungu naye ana complex order, na yeye pia atahitaji kuwa kaumbwa, hawezi kuwa yupo tu (kwa mujibu wa hoja yako mwenyewe kwamba complex order haiwezi kutokea tu, ni lazima iwe imeumbwa).

Kwa hoja hii, Mungu naye ni lazima atakuwa kaumbwa, hawezi kuwepo tu.

Na Mungu wako akishakuwa kaumbwa tu, anapoteza uungu wake wa kuumba kila kitu, maana kaumbwa.

Hivyo, hoja yako inaonesha huyo si Mungu. Na pia inaonesha Mungu hawezekani kuwapo.

Sijui kama umeelewa hoja.

Kifupi, ukisema nyumba haiwezi kuwepo tu ni lazima iwe na mjenzi unasema hata Mungu hawezi kuwapo tu, ni lazima awe na muumba wake, na akishakuwa na muumba wake basi ndiyo anakuwa si Mungu.

Umeelewa?
 
Papa Francis yeye anatetea dini ndio mana alishindwa kujib , mm nlishakuambia Muumba yupo ila sio kama dini znavomuongelea , kwasabb dini zenyewe misingi yake ni siasa za uongo na maandishi ya kuungaunga. Lkn Muumba yupo na anaendelea na kazi ambazo Zina umuhimu kwake sio kukufuatilia ww an insignificant being in the vastness of this universe.
Kusema "Mungu yupo" si uthibitisho kwamba yupo.

Thibitisha kwamba yupo.
 
Kingine nachoamin mungu yupo ni ishara na miujiza anayotenda inatosha kuthibitisha yupo
Ishara gani?

Miujiza ipi?
FB_IMG_1722976782305.jpg
Huyo Mungu Ameshindwa na Anashindwa kuwasaidia maelfu ya watoto wachanga na wanawake wanaokufa kwa njaa, vita, magonjwa na majanga mbalimbali ya asili yanayotokea duniani. Halafu unasema huyo Mungu anatenda miujiza!!!!

Huyo Mungu kama yupo ni Mungu muovu, mkatili, muuaji na bandidu.

Hafai kabisa kuwa Mungu na anastahili kufurushwa huko alipo.
 
Kingine nachoamin mungu yupo ni ishara na miujiza anayotenda inatosha kuthibitisha yupo
Unajuaje hayo mambo unayoita ishara na miujiza ya Mungu kweli ni ishara na miujiza ya Mungu, na si kitu kingine chochote tofauti?

Hili ni swali la falsafa ya epistemology.

Unajuaje unachofikiri kuwa ni kweli ni kweli kweli?
 
Ishara gani?

Miujiza ipi?
View attachment 3163680Huyo Mungu Ameshindwa na Anashindwa kuwasaidia maelfu ya watoto wachanga na wanawake wanaokufa kwa njaa, vita, magonjwa na majanga mbalimbali ya asili yanayotokea duniani. Halafu unasema huyo Mungu anatenda miujiza!!!!

Huyo Mungu kama yupo ni Mungu muovu, mkatili, muuaji na bandidu.

Hafai kabisa kuwa Mungu na anastahili kufurushwa huko alipo.
Mungu tulimuhasi kwenye bustan ya Eden akasema mwanamke utazaa kwa uchungu mwanamme utatafuta kwa jasho
 
Kama hayupo

thibitisha
Madai ya uwepo wa Mungu yametoka kwenu nyie waamini huyo Mungu.

Ninyi "Waamini Mungu" ndio mnadai na ndio mnasema kuna Mungu.

Hivyo nyie waamini Mungu ndio mnapaswa kuthibitisha madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu mnayedai na kusema yupo.

Mkishindwa kuthibitisha madai yenu ya kusema "Mungu yupo" ni kwamba madai yenu ni ya uongo, Na huyo Mungu mnayedai yupo, HAYUPO.
 
Mungu tulimuhasi kwenye bustan ya Eden akasema mwanamke utazaa kwa uchungu mwanamme utatafuta kwa jasho
Thobitisha kuwa hii habari ni kweli na si mapokeo ya hadithi tupu za kiimani zilizotungwa na watu tu.
 
Mungu gani mwenye "Perfection" anaumba watoto wenye kasoro za kimwili kama vichwa vikubwa, njiti, wenye shida za akili, usonji?

Ninyi si ndio mna amini Mungu anaumba binadamu?

Sasa kama huyo Mungu ni "perfect" iweje watoto anao waumba wanazaliwa wakiwa imperfect?
View attachment 3163672
Alianzisha process ambayo ni self replicating, chukulie kama virus ya computer ambayo ni program lkn ajireplicate yaani inatengeneza copy zake yenyew kulingana na instructions za programer lkn huko mbele programer wengne wanaeza kuidukuwa ikaanza kubadilika kdogo, The Creator started the process but we're going to experience so many changes along the way. Kesho kutwa tu sisi wenyew tutakua na uwezo wa kudukua vinasaba ( Genetic manipulation and gene editing ) lkn hiyo haimanishi mtengenezaji wa program ya awali hayupo
 
Huyo Mungu Hakujua kwamba binadamu watakuja kumuasi, Awadhibiti na kuwazuia mapema wasimuasi?

Huyo Mungu Hakujua kwamba binadamu watakuja kumuasi, Awadhibiti na kuwazuia mapema wasimuasi?
Bada ya hawa na adamu kumuasi mungu alienda bustann akawaita wakwap walikuwa wamejificha labda wangeomba msamaha mungu angewasamehe
 
Madai ya uwepo wa Mungu yametoka kwenu nyie waamini huyo Mungu.

Ninyi "Waamini Mungu" ndio mnadai na ndio mnasema kuna Mungu.

Hivyo nyie waamini Mungu ndio mnapaswa kuthibitisha madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu mnayedai na kusema yupo.

Mkishindwa kuthibitisha madai yenu ya kusema "Mungu yupo" ni kwamba madai yenu ni ya uongo, Na huyo Mungu mnayedai yupo, HAYUPO.
Hata uzi wameanzisha wao.
 
Mungu tulimuhasi kwenye bustan ya Eden akasema mwanamke utazaa kwa uchungu mwanamme utatafuta kwa jasho
Kwaiyo sisi vitukuu vya adamu tuna makosa gani mpaka na sisi tuzae kwa uchungu na kula kwa jasho tulikuwapo bustanini?
 
Alianzisha process ambayo ni self replicating, chukulie kama virus ya computer ambayo ni program lkn ajireplicate yaani inatengeneza copy zake yenyew kulingana na instructions za programer lkn huko mbele programer wengne wanaeza kuidukuwa ikaanza kubadilika kdogo, The Creator started the process but we're going to experience so many changes along the way. Kesho kutwa tu sisi wenyew tutakua na uwezo wa kudukua vinasaba ( Genetic manipulation and gene editing ) lkn hiyo haimanishi mtengenezaji wa program ya awali hayupo
Thibitisha kwamba alianzisha.
 
Back
Top Bottom