Logic msingi wake mkuu ni akili, na akili ya mwanadamu ina ukomo.
Kama akili ya mwanadamu ina ukomo, umewezaje kujua kwamba Mungu ni perfect?
Je, Huo sio ukomo wako mwenyewe wa kufikiri kama ulivyosema?
Kama binadamu tungekua na ukomo sawa wa kufikiri tusingetofautiana kimitizamo, falsafa na itikadi?
Conclusion: Binadamu hatuna ukomo sawa wa kufikiri.
Kama unakataa jiulize unauwezo wa kufikiri sawa kabisa na Albert Einstein?
Mungu hafanani na chochote bali ni mkamilifu mwenye kujua.
Ukisoma hicho kitabu chako kinachokupa jeuri kinakufundisha mwanaume mkamilifu anatimiza majukumu ya familia yake.
Je ukamilifu ni kutuma watu waje kuteketeza watoto wako mwenyewe kwa mapigo tofauti tofauti ili kukwepa majukumu?
Je ukamilifu ni kuwatupia watoto wako maovu, matetemeko, vita, magonjwa, njaa halafu wewe unakimbilia kujificha mahala [mbinguni] unaangalia tu wanavyoumia?
Je ukamifu ni kuwaandalia moto mkali watoto wako mwenyewe ili siku1 uwateketeze na usiwaone kabisa?
kama anafundisha mwanaume mkamilifu hutimiza majukumu halafu yeye anayakwepa, Je ni mkamilifu huyo?
Je, Mimi ni mkamilifu kumzidi? sababu ninatafuta pesa, nina upendo, ninahakikisha familia yangu inakua salama, inapata elimu bora, afya, na ulinzi, sijaitelekeza wala sina mpango mbaya na familia yangu .
Nimeweza kuyatekeleza majukumu ambayo yeye ameyakimbia, Je, mimi ni mkamilifu kumzidi?
Kwa ufupi uwepo wa kitu huonyesha uwepo wa kitu kingine kilicho fanya kitu hicho kuwepo.
Kwa kutumia mfano huu umethibitisha kwamba uwepo wa Mungu unatakiwa usababishwe na kitu kingine, na hicho kitu kingine kisasabishwe na kingine, mtiririko uende hivyo hivyo mpaka kusiko na ukomo infinity.
Uwepo wa Mungu ni uwepo wa lazima ambao hauhutaji uwepo wa kitu kingine zaidi yake kufanya Mungu awepo, huo ndio ukamilifu wake.
Hapo juu umedai kwamba ili kitu chochote kitokee lazima kiwepo na kilichosababisha hicho kitu kitokee.
Hapa unakuja na hoja nyingine tena ukisema Mungu haitaji chochote ili awepo.
Kama haitaji chochote ili awepo basi
hayupo, kwasababu kila kitu lazima kiwe kina sababu yake ya kuwepo.
👇👇
Kwa ufupi uwepo wa kitu huonyesha uwepo wa kitu kingine kilicho fanya kitu hicho kuwepo.