Kama akili ya mwanadamu ina ukomo, umewezaje kujua kwamba Mungu ni perfect?
Je, Huo sio ukomo wako mwenyewe wa kufikiri kama ulivyosema?
Kama binadamu tungekua na ukomo sawa wa kufikiri tusingetofautiana kimitizamo, falsafa na itikadi?
Conclusion: Binadamu hatuna ukomo sawa wa kufikiri.
Kama unakataa jiulize unauwezo wa kufikiri sawa kabisa na Albert Einstein?
Swali lako la kwanza, nimejua kwa kutumia viumbe vyake, kwa kutumia akili, kwa kutumia mazingira, na kwa kutumia ufunuo.
Swali lako la pili, ukisoma historia ya Falsafa ya kale ya Magharibi, utaona hili jambo liko wazi sana, pale ambapo walipo kosa majibu sahihi juu ya chanzo Cha kila kitu, wakaja na mawazo yao, wapo walio sema chanzo ni hewa, wapo waliosema chanzo ni moto, wapo waliosema chanzo ni Moshi, bali wapo walio sema chanzo ni kisicho mpaka, wapo waliosema Kuna Prime Mover, bali po walio sema ukamilifu ni namba 10. Swali kwanini walitofautiana juu ya majibu ya swali Moja ? Sababu walitumia akili na hawakuwa na ala ya kuwapa majibu sahihi. Ndio ukawepo ufunuo kutoa majibu ya pale ambapo akili inakomea.
Swali lako la tatu, ukomo wa kufikiri unaletwa na sababu kadhaa, Kuna uvivu, kufata mkumbo, ubishi, ujuaji na ujinga. Hapa lazima tutofautiane.
Hitimisho lako ni hitimisho la kitoto ambalo halina uhalisia, ingekuwa hakuna ukomo wa kufikiri ungeijua kesho yako mzee au baadae kingetokea nini. Labda utakuwa hujui maana ya AKILI, ukijua maana ya AKILI huwezi kuhutimisha kama ulivyo andika.
Swali la lako la tano, nilishawahi kusema huko mwanzo zaidi ya miaka miwili nyuma katika mada hizi hizi, na hapa nasema tena, Eistein achilia mbali kufikiri tu bali kwa akili na utambuzi wa mambo hanifikii, hili ni kwa kinywa kipana. Kwanini nasema hivi, sababu hakuna katika alivyo wahi kuyasema ambayo ni kweli hata moja. Rejea kwanza upingamizi wa Albert Michelson dhidi yake Eistein, Eistein katika ujinga wake aliwahi kuwaambia watu ya kuwa na kufanya ya kuwa Dunia inazunguka kwa maana ipo katika motion, na hakufanya jaribio lolote la Kisayansi. Kwangu Eistein kilaza tu na muongo, sababu hakuna uhalisia wowote katika yote aliyo wahi kuyasema.