Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Sasa kama unataka jibu fupi si usome maneno mawili ya mwanzo tu nimeanza kwa kuandika "Sitaki imani" nikijua kabisa kuna watu wavivu wa kusoma na hawawezi kufuatilia mlolongo wa maandishi ya kimantiki.

Tatizo lako lipi ikiwa maneno mawili ya mwanzo kabisa yanasema "Sitaki imani" na huko mbele ni maelezo tu ya kwa nini sitaki imani?

Umeshindwa kusoma hata maneno mawili ya mwanzo ya jibu?
Jibu ndio au sio, ukimuuliza mtu una hela akasiju ndio au hapana , ni sawa na atakejibu hataki hela
 
Umejibu jibu refu my nataka useme ndio au hapana kisha niendelee Sion hutaki Imani sema ndio au sio
Siyo tu sina imani.

Nikikwambia sina imani unaweza kuona hii ni nafasi ya kunihubiria imani yako.

Sina imani ya kidini na sitaki imani.

Umeridhika?
 
Huko kusema Mungu hayupo,ndio kuweko kwake,kisichokuwepo hakisemwi hakipo.Kuweko kwa Mungu,ndiokunakosemwa hayupo,na kwa kuwepo kwake.
Kisicho kuwepo, hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika kipo.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Hivyo Mungu hayupo.
 
Kwahiyo kitu kama hakionekani upaswi kukiamini, una pumzi una roho na unaviamini na nasfi unaamini kama unayo ushawai kuona hivyo vitu? lakini unaamini unavyo wewe uko timamu kweli, au unasema hivyo uliufanye vitu vyako pendwa bila kufata utaratibu
Akili pia hainekani,lakini anasema ana akili,joto hali0nekani,lakini anasema anahisi joto,baridi na upepo haonekani lakini,anasema anahisi baridi au upepo.
 
Kwahiyo kitu kama hakionekani upaswi kukiamini, una pumzi una roho na unaviamini na nasfi unaamini kama unayo ushawai kuona hivyo vitu? lakini unaamini unavyo wewe uko timamu kweli, au unasema hivyo uliufanye vitu vyako pendwa bila kufata utaratibu
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika na kuhisika.

Joto na baridi havionekani, ila vipo kwa kuhisika na vina pimika vipo na kufahamika vipo.

Upepo hauonekani, ila unasikika ukivuma, unahisika na kupimika upo.

Sasa huyo Mungu wenu, Hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Huyo Mungu haonekani, hashikiki, hasikiki , haisiki na wala hapimiki.

Mungu huyo ni mawazo yenu ya kufikirika tu, imaginations just an illusion.
 
Akili pia hainekani,lakini anasema ana akili,joto hali0nekani,lakini anasema anahisi joto,baridi na upepo haonekani lakini,anasema anahisi baridi au upepo.
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika, kuhisika na kupimika.

Joto, baridi na upepo havionekani kwa macho. Ila vipo kwa kuhisika, unaweza kuhisi joto au baridi. Upepo hauonekani ila unasikika ukivuma na kujulikana upo.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo. Haonekani, Hashikiki, Hasikiki, haisiki na wala hapimiki.

Mungu huyo ni mawazo ya kufikirika tu, imaginations just an illusion.
 
Huko kusema Mungu hayupo,ndio kuweko kwake,kisichokuwepo hakisemwi hakipo.Kuweko kwa Mungu,ndiokunakosemwa hayupo,na kwa kuwepo kwake.
Kama kusema Mungu hayupo ndiyo uwepo wake, je, kusema Mungu yupo nako ndiyo kutokuwepo kwake?

Kusema hakubadilishi ukweli. Kama yupo yupo, kama hayupo hayupo. Haijalishi utasema yupo au hayupo.

Kama yupo, thibitisha yupo.
 
Kwa wanaoamini hakuna mungu, ukiwachunguza kwa makini hawa watu ndiyo ujifanya wao ni majiniazi, kumbe ni wapumbavu wa mwisho katika hii dunia, na hoja yao kubwa ni kwamba kila kitu ni nature hoja hii haina mashiko hata kidogo na ni hoja ya kipuuzi ambayo utolewa na watu ambao kwa kawaida wameshindwa kuamini katika imani zao kwa uthabiti maybe wamechunguza kuwa katika imani zao ambazo wamekuwa na kulelewa umo aziko sawa sawa na azijawapa majibu yakutosha kiasi cha wao kuamini

Kuna wengine majeuri tu na kwakweli katika hii dunia watu hao awawezi kukosekana wanajua na kuona lakini nyoyo zao zimekufa na wauwaji ni wenyewe na matendo yao.

Na rudi katika hii hoja ya kusema kila kitu kipo sababu ni nature, huyu huyu anaesema hivi anaamini kwamba simu anatengeneza mzungu internet mzungu,

ila jinsi mungu alivyoumba kila kitu kwa ustadi wa hali ya juu wanasema ni nature, ushuuzi!
Na kuhusu shetani wanasemaje!?
 
Jibu ndio au sio, ukimuuliza mtu una hela akasiju ndio au hapana , ni sawa na atakejibu hataki hela
Hela ni nini kwanza?

Nikiwa na hela ya zamani isiyotumika tena, halafu ukaniuliza nina hela, nijibu ndiyo au siyo tu, bila maelezo, hapo nakujibu ndiyo au siyo?

Kwa nini unaona jibu kinaloweka muktadha vizuri ni tatizo?

Una akili ndogo hivyo kiasi kwamba mtu akikupa jibu kenye muktadha kidogo tu linakurusha akili?
 
Wewe ukiulizwa umejuaje kuna Mungu?

Unaanza kuleta hadithi za kwenye Quran. Mara ooh! Imeandikwa kwenye Quran.

Ukiambiwa uthibitishe ukweli wa hayo maandishi ya Quran huwezi.

Unabaki kuruka ruka tu.

Kijana twende taratibu hapa tuna taka hoja.

Mimi nimejua juu ya uwepo wa Mungu kwa njia hizi :

1. Maumbile yetu.
2. Mazingira yaani Ulimwengu na vilivyomo.
3. Akili
4. Ufunuo yaani Qur'an.

Usijifananishe wewe na Mimi, yaani tuko mbali sana, Mimi natumia akili kufikiria wewe unatumia nadharia za Wanafalsafa na hisia.

Swali, la msingi je hicho kinachoongelewa kwenye Qur'an ni ukweli au uongo ? Unatakiwa uguse hoja na usikimbie. Mtu mwenye akili anapo letewa andiko lazima kwanza alitafakari na kama ni la uongo lazima uonyeshe uongo wake uko wapi. Hapo utaonekana una akili na unajua nini unachofanya bali ni katika adabu za mijadala. Ila hiki unachofanya ni utoto.

Ukweli wa hayo maandishi uko wazi sana, na Uthibitisho wake kadhalika uko wazi. Mfano wewe unapo dai ya kuwa Qur'an ni Hadithi tu na ukashindwa kuthibitisha unajiweka katika kundi gani ?

Uthibitisho juu ya ukweli wa Qur'an unaoatikana katika Qur'an yenyewe. Sababu walio ipinga hawakuanza Leo bali wenzenu walikuwa mabingwa wa hoja na lugha pia, Qur'an ikawapa "Challange (Mtihani)", walete walau mfano aya moja tu kama wao wanasema kweli. Sasa wewe upo mbali sana katika ujinga, walau wenzako walikuwa wanapinga na kashkash walikuwa wanaleta, ila wewe unaishia tu kusema na huonyeshi wapi Kuna shida. Kwa maana nyeoesi ni kuwa huijui.

Nimekuwekea aya hapo kutoka kwenye Qur'an, je kile kilichomo humo ni uongo ? Kama ni uongo onyesha hilo.
 
Uwepo wangu hauonyeshi, uwepo wowote wa kwamba Mungu yupo.
Sio kweli, bali unaonyesha uwepo wa nini ?

Isiwe unaandika tu ilimradi umeandika, andika vile vya maana.

Wewe tuambie Sasa, ilikuwaje uliwengu ukawa hivi ulivyo ? Kama hujui kwanini ukane juu ya uwepo wa aliyefanya ukawepo huu Ulimwengu ?

Baada ya hapa tutakuja Sasa kujadili vitu specific yaani hasa, tena vile vidogo vidogo, ili uone uwepo wa Mungu.
Ni wewe tu unafosi na kulazimisha iwe hivyo.

Nakwambia hivi, Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe ajiongelee na kujielezea sio wewe unahangaika kumwelezea na kumtetea.

Hili swali nilishakujibu katika mada mfano wa hii, na ukashindwa kukosoa nilicho kujibu.

Mola sababu ni muweza wa yote na mwenye nguvu, hapangiwi na kiumbe chake afanya hivi, bali anafanya anavyo taka. Kwahiyo hili halionyeshi ya kuwa Mungu hayupo.

Pili, kupitia viumbe vyake amethibitisha juu ya uwepo wake ila kwa watu wenye kutumia akili na kufikiria.

Tatu, chochote unachokiona hapa duniani kina thibitisha juu ya uwepo wake, hakuna kinyume chake, sababu hata akili iliyo salama inakubali hilo.
 
Unachokiafanya wewe ni mahubiri tu ili watu waamini Mungu yupo kupitia Qur'an ambayo pia imeandikwa na watu tu.

Safi kabisa, unaposema kwamba mahubiri unamaanisha ni kitu kisicho kuwa na maana au ni vipi ?

Sababu hata hayo mahubiri ni fact na uhalisia, Sasa unatakiwa upinge kile ninachokiandika na kuonyesha udhaifu wake, na usikimbie hoja.

Mfano, ni huu nakuuliza swali la msingi, je huu Ulimwengu umetokea pasi na chochote au umejiumba ? Bali au ni nyinyi ndio mmeumba mbingu na ardhi ? Karibuni kunakishi hoja na msikimbie hoja, ili muonekane walau mna akili. Kinyume chake mnaendeleza na kuweka sifa zenu wazi za udhaifu wa kujenga hoja, kukosoa hoja na kukimbia maswali.
 
Kama akili ya mwanadamu ina ukomo, umewezaje kujua kwamba Mungu ni perfect?

Je, Huo sio ukomo wako mwenyewe wa kufikiri kama ulivyosema?

Kama binadamu tungekua na ukomo sawa wa kufikiri tusingetofautiana kimitizamo, falsafa na itikadi?

Conclusion: Binadamu hatuna ukomo sawa wa kufikiri.

Kama unakataa jiulize unauwezo wa kufikiri sawa kabisa na Albert Einstein?

Swali lako la kwanza, nimejua kwa kutumia viumbe vyake, kwa kutumia akili, kwa kutumia mazingira, na kwa kutumia ufunuo.

Swali lako la pili, ukisoma historia ya Falsafa ya kale ya Magharibi, utaona hili jambo liko wazi sana, pale ambapo walipo kosa majibu sahihi juu ya chanzo Cha kila kitu, wakaja na mawazo yao, wapo walio sema chanzo ni hewa, wapo waliosema chanzo ni moto, wapo waliosema chanzo ni Moshi, bali wapo walio sema chanzo ni kisicho mpaka, wapo waliosema Kuna Prime Mover, bali po walio sema ukamilifu ni namba 10. Swali kwanini walitofautiana juu ya majibu ya swali Moja ? Sababu walitumia akili na hawakuwa na ala ya kuwapa majibu sahihi. Ndio ukawepo ufunuo kutoa majibu ya pale ambapo akili inakomea.

Swali lako la tatu, ukomo wa kufikiri unaletwa na sababu kadhaa, Kuna uvivu, kufata mkumbo, ubishi, ujuaji na ujinga. Hapa lazima tutofautiane.

Hitimisho lako ni hitimisho la kitoto ambalo halina uhalisia, ingekuwa hakuna ukomo wa kufikiri ungeijua kesho yako mzee au baadae kingetokea nini. Labda utakuwa hujui maana ya AKILI, ukijua maana ya AKILI huwezi kuhutimisha kama ulivyo andika.

Swali la lako la tano, nilishawahi kusema huko mwanzo zaidi ya miaka miwili nyuma katika mada hizi hizi, na hapa nasema tena, Eistein achilia mbali kufikiri tu bali kwa akili na utambuzi wa mambo hanifikii, hili ni kwa kinywa kipana. Kwanini nasema hivi, sababu hakuna katika alivyo wahi kuyasema ambayo ni kweli hata moja. Rejea kwanza upingamizi wa Albert Michelson dhidi yake Eistein, Eistein katika ujinga wake aliwahi kuwaambia watu ya kuwa na kufanya ya kuwa Dunia inazunguka kwa maana ipo katika motion, na hakufanya jaribio lolote la Kisayansi. Kwangu Eistein kilaza tu na muongo, sababu hakuna uhalisia wowote katika yote aliyo wahi kuyasema.
 
Back
Top Bottom