Hapana,
Wewe hata hujui mpagani ni nani.
Neno pagan ni neno lililotumiwa na watu wa dominant culture, hususan wazungu wakristo, kuwadharau watu walioamini miungu tofauti, hususan miungu ambayo ilikuwa haijulikani kwao Ulaya.
Kwa hivyo walivyokuja Africa wakakuta dini za asili wakaziita upagani.
Hata dini za asili za Ulaya waliziita upagani.
Hivyo, utaona kuna watu wengi wameitwa wapagani kwa sababu waliamini miungu ya tofauti na Ukristo/Uislamu tu.
Wapagani wanaamini miungu yao. Wasioamini miungu wala Mungu si wapagani.
Zaidi, kwa watu waliosoma nankuelimika, kwa kiasi fulani, hili neno la mpagani ni neno lisilotumika sana, ni neno offensive, ni kama vike kusema mtu mshenzi, ni neno la kikoloni lenye kubeba maana ya kwamba dini zisizokuwa za wakoloni ni za washenzi.
Ingawa kuna watu wanalitumia kujitambukisha wao wenyewe na kukumbatia miungu yao ya asili.