Kwa wanaodhani Wana nguvu ya Hoja za kutomkubali Rais Samia, hakikisha unajua unachozungumza

Kwa wanaodhani Wana nguvu ya Hoja za kutomkubali Rais Samia, hakikisha unajua unachozungumza

muda mrefu kwa maana gani?umeingia lini?
 
Mkaruka una inaonekana una masilahi binafsi nn?Yaan unataka kusema mama yupo positive Sana.Hauoni mabaya yake Kabisa.
 
Mkaruka una inaonekana una masilahi binafsi nn?Yaan unataka kusema mama yupo positive Sana.Hauoni mabaya yake Kabisa.
Sijasema Rais Samia ni MALAIKA. Vile vile, sidhani hata Kama tungepata huyo MALAIKA kama kweli tungemhitaji.

Sometimes, Rais au Kiongozi anaweza kuwa mwema lakini watu wakamharibu.

Kama Kiongozi anaweza kuwa mwema, na bado watu wakawa hawana shukrani tafsiri yake ni kwamba anaweza kuamua kufanya chochote, watu wakaumia na Hakuna kitu watafanya.

Plain truth.
 
Hiyo paragraph yako ya mwisho, nchi inahitaji katiba mpya,yaani hii ya sasa anaweza kutuhamisha wandendeule wote na kutupeleka Tanga, na hatafanywa chochote!,President must earn a respect sio kulazimisha, yes mafuta yamepanda bei ila kwetu hapa ni udhaifu mkubwa wa serikali, bei ya were inategemea mambo mengine sio soko la dunia pekee
 
Ifahamike kuwa Mimi Mkaruka Niko humu JF kwa muda mrefu sana.

Watanzania wa online na offline nawafahamu vizuri.

Binafsi sipendi kuona mtu akionewa Wala sipendi UFUASI KIPOFU ( Total submission to somebody's thoughts).

Karibu Kama kweli una hoja.

Duuu Leo kazi ipo!
 
Wewe ni mfuasi ACT?
Una tabia kama za Abdul Nondo
Mimi sina chama na siwezi kuwa Mwanachama wa chama chochote Cha siasa Wala mfuasi wa mtu.

Nakubaliana na mawazo ya watu. Lakini sikubaliani na kila wazo la mtu.

Sipendi kuona mtu anaonewa.

Sipendi kuona watu wanaabudu watu kwasababu za kifedha, madaraka au imani.

Sipendi kuona LAWAMA na MALALAMIKO yanategemea ni nani KAFANYA.

Jambo A likifanywa na fulani atapewa LAWAMA TON 200 ila likifanywa na mtu B haina tatizo.
 
Hiyo paragraph yako ya mwisho, nchi inahitaji katiba mpya,yaani hii ya sasa anaweza kutuhamisha wandendeule wote na kutupeleka Tanga, na hatafanywa chochote!,President must earn a respect sio kulazimisha, yes mafuta yamepanda bei ila kwetu hapa ni udhaifu mkubwa wa serikali, bei ya were inategemea mambo mengine sio soko la dunia pekee
Aliyefanikiwa kuwakaririsha kuwa Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi vitapeleka nchi ya Maziwa na asali AMEFANIKIWA sana.

Leo unaambiwa KATIBA MPYA na Tume huru ya uchaguzi ndio DIRA ya Kila kitu kizuri unachofikiria.

What an imagination.

Hao hao wanaokuaminisha hivyo, wao siyo MASIKINI na wametajirika chini ya utawala huu huu wa CCM na Katiba hii ya mwaka 1977!!

Wewe hufikirii hapa?

Katiba Mpya Ni muhimu lakini punguza fantasies na matarajio ambayo hayakuwepo.

- Kwanza Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi HAVIONDOI NJAA Wala UMASIKINI.

- Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi haviwezi kuondoa TABAKA LA KISIASA liliopo na litaendelea kuwa ni HILO HILO.

Na nakuthibitishia, Leo Kuna CCM na kesho kunaweza kusiwe na CCM kikawepo chama kingine lakini AINA YA WATU na MAJINA yatakuwa ni Y'ALL YALE.

Mfano:
- Lowassa wa CCM ndiyo yule yule Lowassa wa CHADEMA.

- KANU haipo Kenya ila watawala na political class iliyokuwa KANU ndiyo hiyo hiyo inayotawala kupitia JUBILEE sasa hivi.

- Hapa Ni Kenya ambako Kuna Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi👇👇👇
 
Sijasema Rais Samia ni MALAIKA. Vile vile, sidhani hata Kama tungepata huyo MALAIKA kama kweli tungemhitaji...
Naona hii thread uliyoanzisha inakuzidi upeo, hata hujui unaposimamia.

Tuanze na hilo jibu lako kwa mdau, nakunukuu; "Sijasema Rais Samia ni malaika" [ ukimaanisha Samia sio malaika, ni mwanadamu ana mapungufu yake].

Lakini mbele kidogo unajichanganya unaposema; "Vilevile sidhani hata kama tungempata huyo malaika tungemhitaji" sasa kwanini tusimhitaji malaika ili atuongoze kwa usahihi bila makosa ya kibinadamu?

Hizo nukuu zako mbili hapo juu zinaonesha vile jambo uliloamua kulitetea haliwezekani, Samia kama mwanadamu atapongezwa anapopatia, na kukosolewa atapokosea, lakini sio kumtetea kwa ujumla kama unavyotaka hapa, unlesa uwe tayari kutetea mpaka makosa, na hapo utageuka chawa.
 
Ifahamike kuwa Mimi Mkaruka Niko humu JF kwa muda mrefu sana.

Watanzania wa online na offline nawafahamu vizuri.

Binafsi sipendi kuona mtu akionewa Wala sipendi UFUASI KIPOFU ( Total submission to somebody's thoughts).

Karibu Kama kweli una hoja.
Mkuu siko kumtetea SSH,na wala siko kuwabeza wenye mtizamo tofauti na yeye.
Mpe muda SSH afanye kazi,tutampima 2025.
Pammoja na hilo fanya upembuzi yakinifu ya demokrasia katika hao walio wahi kuongoza nchi.
Unafiki ni uzandiki labda mjomba Magu ange elewa hilo kuwa amezungukwa na watanzania wakusifia kila jambo hata kama ni hatari kwao na taifa kwa ujumla ,mambo yangekuwa tofauti.
 
Mkuu
Asante KWA uzi
Lini FDR atachukua uskani kutoka KWA mama Samia!!?kama uandishi wa miamba humu jf kama Tumia akili na wengineo!!!?
 
Aliyefanikiwa kuwakaririsha kuwa Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi vitapeleka nchi ya Maziwa na asali AMEFANIKIWA sana...👇👇👇
Mkuu u got it total wrong, mimi sio zuzu na ninaelewa umuhimu wa kuwa na katiba itakayoleta haki miongoni mwetu, na mfano uliotuoa kuhusu kenya sio lazima ufanane na wa kwetu kuna nchi nyingi tu zenye uhuru wa kihaki ,haki ambayo ipo ndani ya katiba yao, Mauritius, ushelisheli na sasa Ghana ni mfano mzuri wa jinsi gani katiba inavyofanya kazi,nchi yetu tunahitaji taasisi imara na zenye kujitegemea kimaamuzi sio strong no 1
 
Ifahamike kuwa Mimi Mkaruka Niko humu JF kwa muda mrefu sana.

Watanzania wa online na offline nawafahamu vizuri.

Binafsi sipendi kuona mtu akionewa Wala sipendi UFUASI KIPOFU ( Total submission to somebody's thoughts).

Karibu Kama kweli una hoja.
Vipi kuhusu gharama ya maisha ?
 
Sijasema Rais Samia ni MALAIKA. Vile vile, sidhani hata Kama tungepata huyo MALAIKA kama kweli tungemhitaji.

Sometimes, Rais au Kiongozi anaweza kuwa mwema lakini watu wakamharibu.

Kama Kiongozi anaweza kuwa mwema, na bado watu wakawa hawana shukrani tafsiri yake ni kwamba anaweza kuamua kufanya chochote, watu wakaumia na Hakuna kitu watafanya.

Plain truth.
Ni Mungu tu ambaye hawezi fanywa chochote wewe.
Walikuwepo magwiji kina Alexaander the great.
Hakuna jeshi la mmoja.|
Unaweza kufuga viumbe vyote lakin sio mwanadamu.
 
Sijasema Rais Samia ni MALAIKA. Vile vile, sidhani hata Kama tungepata huyo MALAIKA kama kweli tungemhitaji.

Sometimes, Rais au Kiongozi anaweza kuwa mwema lakini watu wakamharibu.

Kama Kiongozi anaweza kuwa mwema, na bado watu wakawa hawana shukrani tafsiri yake ni kwamba anaweza kuamua kufanya chochote, watu wakaumia na Hakuna kitu watafanya.

Plain truth.

Wema kama upi ambao unataka watu wawe na shukrani nao?

Kuongezeka kwa TOZO kwenye miamala ya simu?

Kukatwa buku kila mwezi hata kama wewe ni mpangaji tu wa nyumba na si mmiliki?

Kusababisha vitu kupanda bei kwa kauli zake za kipuuzi ?

Kwenda kukaa USA kwa kwa karibu week mbili bila ishu yoyote ya msingi ili hali huku home maisha ya wengi yanazidi kuwa hovyo?

Kuweka watu INCOMPETENTS kwenye mashirika nyeti ya Taifa?

Yaani yapo mengi sana yanayofanya watu WASIMUELEWE huyo CHUI JIKE wa makaratasi

Nb : uongozi si suala la mtu kuwa MWEMA wala MBAYA,uongozi ni kutatua CHANGAMOTO za unaowaongoza ili waweze kufikia malengo waliyonayo na si vinginevyo
 
Kwa nn anakuwa na kauli zakuwavunja moyo raia badala yakuwapa matumaini mf vitu vitapanda bei sana.
Kwa nn hapa Tanganyika vitu bei zipo juu tofauti na Zanzibar mf mafuta hapa yamepanda kule hayajapanda
 
Ifahamike kuwa Mimi Mkaruka Niko humu JF kwa muda mrefu sana.

Watanzania wa online na offline nawafahamu vizuri.

Binafsi sipendi kuona mtu akionewa Wala sipendi UFUASI KIPOFU ( Total submission to somebody's thoughts).

Karibu Kama kweli una hoja.
Hivi tz kuna rais au kuna mama?
Ambaye hajui uchungu wa watz wa kawaida, anayelinganisha uchumi wa marekani na uchumi wa watz wanaokula ubuyu na asali. Taifa linapita kqenye wakati mgumu sana. Ukitaka kujua ukweli nenda (njoo) mahali wanapoishi wananchi wa kawaida ambao ndio hasa wanawakilisha kundi kubwa la watanzania wote.

Huwezi kwenda pamoja na waliokutangulia. Kuna wakati inabidi utembee pekeyako kwenye njia yako(walk on your own path)
Si kila aliye mbele yako anaelekea kule uendako.

Sherehe na hafla zisizo na tija kwa taifa.
Safari nyingi za nje ya nchi kwa viongozi mbalimbali. Huku wananchi wanakatwa tozo za miamala, wanahamasishwa kucheza michezo ya bahati nasibu huku wao wakitumia fedha hizo kwa maslahi yao. Wanannchi wanalia bidhaa bei ghali, gharama za maisha ziko juu.

Kuanzishwa kwa sensa ya makazi kwa lengo la kukusanya kodi ya ardhi na makazi toka kwa wananchi wa hali ya chini ambao hata kula kwao ni shida.
Narudia tena, UKITAKA KUSIKIA VILIO HIVI, NJOO WANAKOISHI WATANGANYIKA!
 
Ifahamike kuwa Mimi Mkaruka Niko humu JF kwa muda mrefu sana.

Watanzania wa online na offline nawafahamu vizuri.

Binafsi sipendi kuona mtu akionewa Wala sipendi UFUASI KIPOFU ( Total submission to somebody's thoughts).

Karibu Kama kweli una hoja.
Lilamba asali tu hili..!
 
Back
Top Bottom