Angalizo muuzaji, angalia usiingie matatani na TCRA wakikushika ndugu kesi utazofunguliwa sijui idadi yake, ungefanya kimya kimya bila kujianika, saiv kuna operation ya kuondoa laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa kufuata taratibu, sasa kuingiza laini za kenya ndio(nakubali kwa lengo jema) ila kuna watu wanaweza tumia kichaka hicho kufanya uhalifu, kesi za mauaji mfano zinaweza tumiwa na watu kwasababu ya usajili kufanyika nchi jirani na hivyo kupoteza ushaidi, hayo ni ya ziada ila tumia akili kidogo unapofanya vitu ambavyo ni strict kwa usalama wako pia.
Umeanika namba zako wakianza ku trace mawasiliano yako ndani ya masaa machache identity yako wanayo, sikutishi ila kuwa makini tu inawezakana hujui consequences za unachofanya.
Goodluck