Kwa wanaume ambao mlikuwa na kazi lakini sasa hamna na wake zenu ndio wanaoendesha familia mliwezaje kutoboa?

Soma vizuri Uzi wng nimekwambia nimejaribu issues nyingi tu hadi za umachinga lkn zimejamba, embu fikiria kutoka kutunza kumbukumbu hadi kuwa machinga na huku kitaa unakuta watu wapo kwenye hizo mishe kitambo tu halafu we wakuja uje utoboe kirahisi tu wanakuangali ..

So skukaa kindezi lkn kitaa kiskie tu ndugu yangu hali sio nzuri sn
 
Ulitumia uamuzi wa busara sana kujifungulia kijiwe kimya kimya!
 
Utafukuza nyumba ikiwa yako! Kama wamepangisha je!?
Kama wamepanga na yeye Mwanaume ndiyo aliingia Mkataba na mwenye Nyumba,basi hana budi kuvunja huo Mkataba! Usikubali kunyanyasika kisa Mwanamke wako ana pesa! Na kuna muda mwingine Wanawake wanaonyanyasa Waume zao mara nyingi inakuwaga Kama payback,wanalipiza Mume aliyokua anafanya akiwa njema!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Yani kama kocha wa Simba Gomez? [emoji1][emoji1]
Eeh mzee baba sasa mkimpondea bila kumpa line kwamba apambane vipi inakuwa haijakaa sawa! Kama hata unachakalika uko mahali unamwita kama anaweza fika bana hapa tunabeba boksi toka shimoni mpaka msimbazi kule tuunge unge kwa day haikosekani 15-20 mbona safi!

Ila sio mnapondea oh tafta hela mara hama hapo aende wapi? Akalale chini ya Kijazi interchange ama?
 
Wewe umefuata huo ushauri? Kwa nini unataka mwenzio aanze ulozi, hujui ataongeza tatizo la 3.
 
Kama anaweza kulisha familia kwa sasa,wewe mwage kuwa unaenda kutafuta sehemu.
Ila usihudumiwe na mwanamke mkuu.Nenda sehemu katafute then utarudi,labda kama una wivu sana kuwa mbali na mkeo.
 
Mwanamke sio payback mwanamke hata ukimnunulia iphone kila ikitoka na kumlisha KfC mwaka mzima siku nguvu ya kumfanyia hivyo ikiwa haipo anaanza dharau automatically! Yupo kwa ajili ya kulishwa na kupewa raha tu yeye ila sio yeye akupe wewe!

Mara moja mbili atavumilia ila kuanzia ya tatu offer itaambatana na madongo! 😂😂😅
 
Wale tulioko mtaani tunakuelewa vizuri sana! Game ngumu sana aisee yani ni nyokest! Ugumu unakuwa mara mbili kama ulishawahi kupatia hela kwenye kiyoyozi na kiti cha kuzunguruka!
 
Wengine tunaishi mjini kwa hesabu kubwa sana na kwa kutumia akili nyingi, kwa mwaka naweza kupata ela mara 4 tu na tunakwenda nazo kwa mzunguko wa mwaka mzima.

Kazi rahisi mjini ndio hizo bodaboda na wanapata sana hela, mademu wa mtaani kina Mwajuma mchokonowe siku hizi hawa bodaboda ndio wanawala sana, wana mzunguko wa hela ndogondogo za kila siku.
 
Kaka kuna kitu watu hawakielewi mpaka labda kiwakute, watu wanaomwambia mtoa mada kwanini amekaa miaka mitano bila kupata kazi kuna kitu hawaelewi, kwanza watu tuko tofauti, kitendo cha kupoteza kazi nitakavyokipokea mimi ni tofauti na utakavyokipokea wewe. Kuna mtu akipoteza kazi anaingia kwenye depression moja kwa moja, mtu kama huyu kuja kupata kazi nyingine anahitaji msaada wa kisaikolojia na kiroho kwanza ili arudi kwenye utimamu wake wa akili ndio ataweza kuwa "functional".

Nilishawahi kumfanikishia mtu interview 3, guess what zote aliboronga, na walionishika mkono wanakuja kunichana kabisa kuwa ameboronga na hatukuwa na chakufanya kumbebea. Unajua kwanini? Ile unatoka nyumbani badala ya kutakiwa heri badala yake unaambiwa "usipopata kazi leo sijui unarudije humu". Matokeo yake unaenda kwenye interview umepaniki na tension iko juu. Hiyo moja interview ya vitendo ilikuja kumbeba angalau akapata hiyo kazi.

Afya ya akili ni jambo la muhimu sana, unapaswa kuilinda kwa kadri uwezavyo.
 
Boda boda ni sawa ila labda apate ya mkataba
 
We Dada mungu akubariki na abariki ndoa yako, it seems u have got a heart, be blecd
 
Unaweza kupata mwanamke anaekupenda hata ukiwa huna kazi yeye akakusaidia mahitaji ya nyumbani yote yakawepo
Lakin bado shida itakuwepo tu ndugu zake hawatakuheshimu watakuchukulia kula kulala au utakua unatumwa sokoni wewe huku wao wanaangalia Tv

Cha msingi ongea nae upate mtaj hata kdogo na upotee hapo nyumban tafuta hata mashamba yakuweke busy itasaidia kulinda heshima yako hata yeye atakumiss na ndugu zake watakuheshm maana unajishughulisha hta kma itskua haina faida kubwa uskubali kukaa tu kama beki 3 Muda huo una plan kufanya mambo mengne
 
Sababu limeshatokea mimi nakushauri vumilia endelea kupambana.

Ila siku nyingine hilo ishi nalo tena ukijaaliwa watoto wako uje kuwaambia ya kuwa "Mwanamke kulisha familia si kazi yake,ndiyo maana wakijaribu kufanya hivyo huwa linawashinda mapema sana".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…