Kwa wanaume wanaotarajia kupata watoto

Kwa wanaume wanaotarajia kupata watoto

Kipindi kingine cha muhimu ni ile miezi mitatu baada ya mke kujifungua....
Aisee huwa ni migumu sana na mental breakdown za kutosha
Kama mpo pamoja jitahidi sana kumuweka sawa awe na utulivu wa akili

Shiriki kikamilifu kumsaidia mtoto hata kama ni 2 hours a day, we appreciate that alot
Nimeipenda hii
 
Eti kisa sikuleta nilichoagizwa,akaniambia nimuombe msamaha,kwa kupiga magoti.
Nikamwambia sifanyi huo ujinga,mbona alizaa vizuri tu
Vingine Usipelekeshwe tu kama ling'ombe.
😂😂 huyo alitisha sana au teacher nini😂😂
 
ivi ni kweli kuna wanaume wanaotambua ayo,au nisisi tunaangukia kwa madungaembe🤣🙆🏾
Tupo sana madam,,,ila ndo hivyo kwenye msafara wa mamba na kenge nao wapo
 
Mengine kuendekeza na kujikweza ,,,soda saa nane usiku,,,mara lete hiki sikitaki tena,,,, mbona mabeki tatu, wanafunzi wanapata mimba wanakomaa kigumu mpk kujifungua ? Au kwa vile hakuna wa kumdekea
Nadhani inatokea km tendo lisilo la hiyari. Nina rafiki alipokuwa mjamzito alikuwa msumbufu…Lunch time hataki tuagize au tukale nje, anataka tupike ofisini.

Akiniona ana request ice cream hata km ni asubuhi.

back tu beki 3. Nadhani uwa wanajikaza sana maskini
 
Wanaume wenzangu naomba mtambue kwamba kama kuna kipindi ambacho unatakiwa kuonyesha mapenzi ya kiwango cha SGR / mapenzi ya hali ya juu ya kujali sana ni pale mkeo anapokuwa mjamzito.

Kipindi hiki mke huwa na mambo mengi sana na mpaka mengine unajiuliza hivi hii mimba inavyompelekesha ni yeye tu au wanawake wote wanakuwa hivi pia?

Kuambiwa umletee chakula fulani hlf baada ya kukileta akakitaa ni kawaida tu, kuambiwa usiku wa manane anahitaji soda ya baridi ni kawaida tu na viusumbufu vingi ambavyo havina kichwa wala miguu.

Huu ni wakati ambao mwanamke anapitia changamoto nyingi sana kihisia na mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini mwake,kwahiyo anakuwa katika hali ambayo sio ya kawaida, wengine wanakuwa hawana mambo mengi nawengine wanakuwa na mambo mengi.

Huu si wakati wa kushinda bar na kurudi nyumbani late bali ni wakati ambao uwepo wako ni muhimu sana kwa mwenza wako ili apate kufarijika

Si wakati wa kumpa stress na michepuko yako, ni wakati ambao anahitaji amani ya moyo wake sana,,ni wakati wa kujitoa mazima kwake na kumfanya awe malkia wako.

Kwasisi ambao kwa namna moja au nyingine kwa kipindi fulani tulizua taharuki katika kipindi hiki tuliona pale baby mama anapokuwa na stress mpaka kiumbe tumboni unakisikia kinavyo hangaika kana kwamba kinataka kitoke kimsaidie mama yake ,hii sio nzuri hata kidogo huwa sometime natamani ningerudisha siku nyuma na kuondoa makosa niliyofanya wakati baby mama alipokuwa mjamzito,,sitaki nawe ufanye makosa hayo.

Huu ni wakati wa kuwa mpole na laini sana kwa mkeo,,kwa kifupi jifanye fala sana kwa lengo la kufanya mkeo awe na wakati mzuri katika kipindi hiki,,hapa jishushe sana na uwe mwema sana kwake na uvumilie usumbufu wowote ambao utaupata kutoka kwake,,tambua sio yeye huyo bali ni ujauzito ambao anao ndio umebadilisha kila kitu katika maisha yake.

Onyesha upendo mkubwa sana kwa mkeo na hakikisha hatoi chozi katika kipindi hiki kigumu sana

Kuwa mwanaume na mume bora kabisa kupata kutokea hapa duniani.


Ni hayo tu!
Yote hayo anafanya akijua upo.. sometimes ni makusudi tu..
Siku hizi sikubali kabisa huo usumbufu.. inabidi uweke mipaka la sivyo utadata kuliko yeye.
 
Mbaya zaidi siwezi kuwafukuza, hivi Mimba inaweza kukufanya umchukie mtu?
Yawezekana... mimba zinatofautiana

Ingawa binafsi mimba zangu zote sikumbuki kumchukia mtu wala kuwa na heka heka,

Kuna baadhi tu ya vyakula kama tambi na kiepe yai huwa nakula sana walau once a day kipindi cha mimba, ila nikijifungua siwezi havinibambi kama kiepe yai mpaka nimesahau lini mara ya mwisho nimekula
 
Yawezekana... mimba zinatofautiana

Ingawa binafsi mimba zangu zote sikumbuki kumchukia mtu wala kuwa na heka heka,

Kuna baadhi tu ya vyakula kama tambi na kiepe yai huwa nakula sana walau once a day kipindi cha mimba, ila nikijifungua siwezi havinibambi kama kiepe yai mpaka nimesahau lini mara ya mwisho nimekula
Kumbe mnatofautiana pakubwa sana, HAPO sasa nimekuelewa vizuri
 
Vijana wa siku hizi wana Dhani wao ndio wa kwanza kuzaa hapa Duniani.
Achana na drama za wanawake.
 
Back
Top Bottom