Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwangu mie drama kama ni mbaya naiona tangu episode ya kwanza
Kuna kale ka-feeling ka kukata stimu dakika 30 tu za episode ya kwanza πŸ˜€

Binafsi kuruka episode najiona kama najiibia hivi
Kuruka episode kama ukichaa Fulani mimi siwezi kamwe raha ya movie uwe na curiosity kuhusu yajayo .

Mimi Sheria yangu mwisho episode 5 kama haikeweki siendelei.
 
Wakorea kweli wanapenda kushindana na bullying halafu wengi hawapo stable psychologically . Yaani kitu kidogo kujiliza na kujipa stress za muda mrefu .

Kuna real show Moja niliona MBC YouTube Kuna mdada Muislamu kutoka Uzbekistan alikuwa anahojiwa kavaa hijabu yake . Huyo Dada anachapa Kikorea full kama wenyewe na mwanae kazaliwa mdogo Kazaliwa Korea na anachapa Kikorea

Yeye alikuja Korea kufanya kazi na alikuwa anapenda Korea kupitia series akaAdapt life style na kila kitu akawa kama mkorea mpaka uraia akachukua , akawa anaeleza Changamoto ya bullying na kuchekwa aliyoipata mpaka akawa analia , eti walikuwa wanamuona wa tofauti kisa mavazi yake (hijabu) na asili yake akawa apate love ya kweli na wengi kama Raia .

Akawa anaomba mwanae mdogo mashuleni na asifanyiwe bullying na asipitie kama aliyopitia yeye .
 
Mfano suala la population ya watu kupungua kwa kasi ni tatizo la mataifa yote yaliyoendelea. Japo Korea hali inatisha sana. Nchi za magharibi nyingi ni multicultural society, zinawatumia wahamiaji kubust population yao japo sio njia ya kudumu lakini kwa ajili ya faida za kiuchumi. Unakumbuka nilikwambia Uchumi wa Japan umekuwa stagnant tangu mwaka 1995 sababu kuwa ya population yao kubwa imezeeka. Wanaozalisha ni wachache, since serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kuwahudumia wazee. Hiki ndio kitu Taiwan, Hong Kong, Singapore na Korea wanakipitia sasa hivi possibly near future China.

CORE DISCUSSION

Kwanini Nchi za Asia Mashariki wasitumie wahamiaji kama njia ya haraka( kutumia wahamiaji) huku wakitafuta suluhisho la kudumu kuhusu maswala ya uzazi?. Kwa sababu hao majamaa ni mono-cultural societies. Mfano wakorea Ni vigumu kukubalika na jamii kuwa kama mtu wao hata kama umekaa nao kwa zaidi ya muhongo, watakuwa wanakuonawakuja. Tena kama hujui Kikorea ndo unabalaa watakuwa wanakuona unadharau hueshimu Tamaduni zao. Ok Sahau kuhusu watu weusi pale Korea. Kunawahamiaji wengi kutoka Ufilipino,India, Malaysia, Vietnam na wengi wanaenda baada ya kuvutiwa na Kpop&Kdrama wakuwatreated kama wanyama baada ya muda wanaondoka.
Wakorea wanadharau, tena wakijua unatoka Nchi ambayo Korea yao inakuzidi Uchumi au maendeleo kazi unayo.

Tunajua tension ya kisiasa iliyopo kati ya China na India lkn Wahindi wanahisi kutendewa vizuri zaidi wakiwa China na Japan kuliko Korea. Ila hao wakorea Nchi za Magharibi especially ni miungu wao wanawabudu sana. Wale wakorea walitembea Nchi zingine they are sweetest people in the world sababu wanakuwa wamejifunza kuishi na watu wa jamii na rangi tofauti. Msingi wa ubaguzi wao ni Tamaduni zao wenyewe na ndio kitu kinawatafuna. Sisi wa ukoo wa Lee tunaheshimika, au ukoo wa Park, Kim. So wao kwa wao wanatambiana sana, social pressure ni hatari huko mzee yaani hata wewe ukikaa miaka 4 unaanza kuwa kama wao stress kibao. Huwezi tena kumudu criticism kwenye jamii au mitandaoni.
Ndio maana wakipata nafasi wanakimbilia Magharibi, huko hali ya kifo inaondoka, hakuna mashindano ya kijinga. Ndio maana wazazi wenye uwezo hawaruhusu watoto wao kusoma korea bora madharibi hata ukipata 50 sio shida no one is going to persecute you, maana mfumo wa Korea elimu ni notorious.

Forget about Natural death and homicide, visa vya kujiua( Suicide) ndio tishio zaidi ndio vinamaliza watu wengi kwa mwaka. Waza jinsi ambavyo hawazaliani it's true 2100 wanaweza kweli kufutika kwenye uso wa dunia msaada wao mkubwa mpk sasa ni kuwa wanaishi miaka mingi, wangekuwa na maisha mafupi kama Africa sidhani kama 2050 wangevuka. NO CHILDREN, NO HOPE, NO FUTURE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…