Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Ameen Ameen
Hope uko poa pia
Hehehe wasiwasi lazima.
Sikujua kama nimekaa sana ila ilivyofungiwa sikuwa na ujanja wa kuingia, nikiingia inahema tu JF aah mateso nikaifuta…
Karibu tena. Tulikumiso 😍
 
Du!? Jukwaa letu siku hizi limepwaya sana
Kazi kali za korea zimepungua mno.

Sikuwahi kuangalia Mr. Sunshine ndo naiangalia hivi sasa naona story yake inaeleweka kirahisi mno, nilivyoona inasifiwa sana nilidhani ni story ngumu.
 
Jang ok Jung anawapa nightmare maadui zake.
(Dong Yi, Jang ok jang na Royal Gambler) zote hizi zina eleza visa wakati wa Mfalme Suk Jeong. But story tofauti.
 
Kazi kali za korea zimepungua mno.

Sikuwahi kuangalia Mr. Sunshine ndo naiangalia hivi sasa naona story yake inaeleweka kirahisi mno, nilivyoona inasifiwa sana nilidhani ni story ngumu.
Sunshine haiumizi kichwa haina twist sana
 
Hahaha, huyu Jang ok Jung ndiye steling mwovu niliyewah kumwona.
She's giving her enemies nightmares
But huyu queen inhyeon kote kaonewa sana na Jang ok Jung. Kwenye Dong Yi na hii jang ok jung the living love
 
Nyingine nimetazama The Affair was just the beginning
Kuna yule dada wa 9.9billion ye anajilipuaga scene za matusi🫣
 
Nimemalizana na JANG OK JUNG, LIVING BY LOVE.
Zamani nikiwa kijana nilidhani drama kuwa nzuri lazima iwe na action nyingi, vita na ubabe, drama iliyokosa hivyo vitu niliiona kuwa mbaya. But baada ya kuitazama DONG YI, THE JEWEL IN THE CROWN ilibadilisha mtazamo wangu kuwa drama inaweza kuwa kali bila hata ya actions. Ilinipa inspiration ya kuitazama YI SAN, WIND IN THE PALACE. DAE JANG GEUM, JEWEL IN THE PALACE, SANDO THE JOSEON MERCHANT, HUR JUN, KIM MANDEOG THE GREAT MERCHANT, THE MERCHANT, HWANGJIN, MY SASSY GIRL, JANG OK JUNG. Hizi ni baadhi ya drama hutoona action huko ndani but utazifurahia mno.

Kwa sasa Naifikiria THE KING AND I. mahala pa kuipata ndio mtihani so msaada tafadhali. pia HORSE DOCTOR, FLOWER IN THE PRISON
 
Six flying Dragons
Tree with Deep roots
Empress ki
Ju mong
Arthridal chronicles
Crowned clown
Mr sunshine

Kama hujaona hizi basi bado hujaona
 
Six flying Dragons
Tree with Deep roots
Empress ki
Ju mong
Arthridal chronicles
Crowned clown
Mr sunshine

Kama hujaona hizi basi bado hujaona
Zote nimeziona kasoro mbili tu Clowned clown na Mr Sun shine , hiyo list uliyoweka ipo 🔥 🔥 🔥

Arthdal Chronicles nilitamani watuoe season 3
 
Jana nimemaliza Hwarang , nimeipenda Ina mwisho mzuri sana .

Huyu Mzee nilipomuona nikajua lazima itakuwa 🔥 , huyu Mzee ndio wale MaKing Makers au wazee wa fitna
IMG_20261014_213257.jpg
 
Back
Top Bottom