Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hii pia umeiangalia ikiwa na subtitle?
Kwa njia gani kamanda
Mara ya kwanza niliishusha kupitia Nkiri ikawa haina subtittle nikaja huku kuomba msaada ila sikupata.

Baadae nikaja kupata namna ya kudownload subtittle kupifia "subtittlecat" kisha naenda kuzipaste kwa VLC
 

View: https://www.youtube.com/watch?v=QjRZooK6nRg

walevi wa zamani tumekumbukwa, KBS wanakuja na hii project itakapofika mwezi novemba 2026.
wanasema itakuwa ni historical drama yenye bajeti kubwa sana.
Inaitwa the great king MUNMU.

kwa aliebahatika kuangalia
dream of emperor (king's dream) ya choi soo jung,
dae jo young ya choi soo jung,
queen seondeok drama,
hata yeon gae somun (sidhani kama kuna alieiona)

mtazamaji atakuwa anarejea kwenye maeneo hayo.

hii inamzungumzia mfalme munmu (alikuwa ni mtoto wa chunchu), huyu bwana alikuja kuhitimisha safari ya kuziunganisha three kingdom (shilla, goguryeo na baekje).

ndani tutakutana na
jang hyuk - ameigiza uhusika wa general yeon gae somun wa goguryeo (history yake inafahamika),
lee hyun wook - ataigiza uhusika wa king Munmu.
Park sung woong - ataigiza uhusika wa general kim yu shin
Kim kang woo - ataigiza uhusika wa chunchu (baba yake King Munmu), huyu bwanaa alipewa heshima ya King Taejo Muyeol wa Shilla..

supporting actors
kim woo dam - uhusika wa Gye baek (historia yake inafahamika)
lee ji hoon - uhusika wa BI DAM (stori yake inafahamika)

kihistoria baada ya kufa queen seondeok, alikuja mtawala mwengine wa kike ambae aliitwa Jindeok,
baada ya kufa Jindeok ndio alikuwa CHUNCHU.
kama nitakuwa sahihi ndani ya tamthilia ya queen seondeok huyu chunchu alikuwa mtoto wa dada yake deokman.

nazungumzia kiuso wa drama

Ulevi wetu huu
Nadhani itakuwa na episode chache
 
Mara ya kwanza niliishusha kupitia Nkiri ikawa haina subtittle nikaja huku kuomba msaada ila sikupata.

Baadae nikaja kupata namna ya kudownload subtittle kupifia "subtittlecat" kisha naenda kuzipaste kwa VLC
Yeon gaesomun umeipata tovuti ya NKIRI..

mbona sijaiona mkuu
 
Thriller genre: SCARECROW

Hii series ni Kali ile mbaya sema ipo underrated sana inahusu muuaji ambaye anafanya mauaji ya watoto wa kike na huwa anavaa kijago cha crow utamu wa hii series unakuja pale ambapo polisi wanaofanya uchunguzi wanavyoteseka kumpata muhusika sahihi watamuhisi fulani mwisho wa siku wanagundua sie wanajikuta heshima yao inashuka kwa jamii, conflicts za wao kwa wao zinaibuka na cha ajabu muhusika sahihi wa mauaji atakuja kujulikana ambaye hakuna mtu aliyetarajia hata wewe unayefuatilia inakushangaza.
 
Ni muda wa kurejea viporo vyangu since 2020.
Now nimeanza na MY SASSY GIRL, niko episode ya 5. Humu ndani kuna wendawazimu kibao. Kama unapenda comedy karibu maana imekusanya wajinga kutoka MORDEN FARMERS
kazi ipo YouTube( SBS World)
 
MADE IN KOREA SEASON 2:
Dude limerejea tena kwa wale tulioangalia season 1, pale mihimili miwili inapoamua kuonyeshana nguvu.
wahuni waliopo idara ya usalama wa taifa pamoja na waendesha mashitaka.
1788953824254.png
 
I am
Alhamdulillah
Niliona hekaheka kuingia na ma vpn
Nikawa najipakulia zangu minyama ya Apps kimya kimyaa.
mimi ni mtu wa udadisi na tafakari zisizo na msingi, If someone akishaingia katika mfumo wangu wa akili halafu ghafla akapotea huingiwa na wasiwasi.
Je ni mzima wa afya,
amepotea,
ametekwa,
matatizo ya kifamilia...

e.t.c
kama upo hai, basi ashukuriwe Mungu
 
mimi ni mtu wa udadisi na tafakari zisizo na msingi, If someone akishaingia katika mfumo wangu wa akili halafu ghafla akapotea huingiwa na wasiwasi.
Je ni mzima wa afya,
amepotea,
ametekwa,
matatizo ya kifamilia...

e.t.c
kama upo hai, basi ashukuriwe Mungu
Ameen Ameen
Hope uko poa pia
Hehehe wasiwasi lazima.
Sikujua kama nimekaa sana ila ilivyofungiwa sikuwa na ujanja wa kuingia, nikiingia inahema tu JF aah mateso nikaifuta…
 
Back
Top Bottom