DAEMUSHIN
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,428
- 120,464
kwangu mimi huwezi kuizungumzia nchi ya Joseon bila ya jeong do jeon(sambong). nikiangalia harakati zake za kupigania usawa kwenye taifa la Goryeo kwa kupambana na waziri mkuu lee I-Nim mpaka akaamua kuwa muasi na kufanya mapinduzi na kutafautiana na rafiki yake kipenzi Jeong mong ju (poeun) great thinker wa kipindi hicho ambaye alikuwa akiamini wao kwa pamoja wana uwezo wa kurudisha heshima ya taifa la goryeo ila bahati mbaya sambong hakuwa tena na mawazo ya goryeo na kwangu mimi urafiki wa sambong na poeun ulikuwa ni zaidi ya urafiki wa lowassa na kikwete.Yule mwalimu kwenye 6flying[emoji236] sambong (jeon do jeon) hyo Series hapo ndo inamwelezea napata kuamini yule ticha alikua noma sana
Sent using Jamii Forums mobile app
ukiangalia drama hii ya jeong do jeon ndipo utapata kufahamu zaidi jinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza kati ya sambong na general yi seong ye mnamo mwaka 1383 kwenye kambi za hamgyong wakati ambao yi seong ye alikuwa anaongoza vita dhidi ya wavamizi wa japan.
mwaka 1388 wakati ambao taifa la mongols lilipoivamia taifa la goryeo ndipo yi seong ye akaamrishwa kuivamia kaskazini mwa liaodong ila cha kushangaza lee seong ye akakataa oda ya mfalme na ya general choi young na akatoa sababu zifuatazo kwa ushauri wa mwanamipango sambong
- taifa la goryeo ni dogo hivyo halina uwezo wa kuvamia taifa kubwa
- hali ya hewa ilikuwa ni ya mvua hivyo basi msafara wa kuelekea kaskazini utakumbana na dhoruba nyingi
- kama nchi itaelekea vitani upande wa kaskazini basi wajapan watavamia upande wa kusini
- kwa kuwa ni wakati wa mvua basi wananchi wanapaswa kulima na si kwenda vitani baada ya majibizano ya muda mrefu yi seong ye akaamua kurudi mji mkuu wa gaegyeong pamoja na jeshi lake na kutokezea vita ya wenye kwa wenyewe jambo lililopelekea general choi young kushindwa vita na ukawa ni mwisho wake wa kuwa na nguvu.
ila siku chache kabla ya kunyongwa kwa sambong lee bang won ambaye alikuwa ni mtoto wa tano wa general yi seong ye alimuua jeong mong jo (poeun) kwenye daraja la sonjukkyo na ukawa ndio mwisho wa harakati zake za kuipigania goryeo.
kabla ya kifo chake aliandika shairi na kumtumia yi bangwon ampelekee baba yake
Though I die and die again a hundred times,
That my bones turn to dust, whether my soul remains or not
Ever loyal to my Lord, how can this red heart ever fade away?
yi seong ye akawa mfalme wa joseon na ukawa ndio mwisho wa utawala wa wang na kuanza kwa utawala wa lee (yi) na sambong akawa waziri mkuu wa joseon na ndiye aliyesimamia ujenzi wa ikulu ya joseon na akaipa jina la Gyeongbokgung palace ambayo mpaka leo inatumika kwa ajili ya kuigizia drama na pia kuwa ni kivutio cha utalii.
vita ya madaraka ikaingia tena kwenye taifa la joseon baada ya yi bang won kutokuchaguliwa kuwa ni mrithi wa kiti cha mfalme ambapo nafasi yake alipewa mtoto wa kwanza wa mke wa pili wa general yiseongye (yi bangseok) na aliamini aliyesababisha yeye kukosa nafasi ni sambong kutokana na bifu la kumuua rafiki yake poeun.
kosa lile lile alolifanya general choi young la kutaka goryeo ivamie nchi ya china kwa ajili ya kuurudisha mji wa liaodong ambao kihistoria ilikuwa ni ngome ya goguryeo kabla utawala wake haujaanguka naye sambong alilirejea tena kwani naye aliamini joseon ina uwezo wa kuipiga china. siku chache baada ya kufa kwa malikia sindeok naye yi bangwon aliitumia nafasi hii kufanya mapinduzi kwa kuwaua ndugu zake ambao walizaliwa na mama wa kambo na pia kumuua sambong na wafuasi wake na akabeba ufalme.
yi bangwon akamtangaza sambong kama ni muasi wa taifa na mwili wake utupwe na pia akamtangaza jeong mong jo kama ni shujaa wa goryeo.
je ninani shujaa kati ya jeong do jeon (sambong) na jeong mong ju (poeun)